Ankal,
Aina hii ya mkungu wa ndizi unaopatikana kisiwani Pemba pekee. Unafaa zaidi kwa walio wenye familia kubwa au wauza ndizi kwenye Pub
Mdau Pemba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Acha uongo hapo siyo Pemba bali hapo ni Bukoba kaitka kijiji cha Kibeta. Pemba hawana jeuri ya kuwa na mgomba kama huo hapo juu. Hiyo picha niliipiga mimi mwenyewe

    ReplyDelete
  2. uongo bwana, hakuna mkungu kama huo huko zenji.

    ReplyDelete
  3. Asante sana ankal kwa taswira hii ya ndizi kutoka kule Pemba.Je aina hii ya ndizi haiwezi kuwafikia wakulima wengine wa ndizi?

    ReplyDelete
  4. kwa walio wenye familia kubwa mmmm sina hakika kama hiyo sentensi iko sahihi...but huo mkungu ni noma....lichimbwe shimo uendelee hadi utakapojiskia maana hapo naona kama wameukatili

    ReplyDelete
  5. acheni ujinga hayo mambo ya photosssss kwa wale anaojua hawana comenty yoyote, asante michuzi wape shule hao!!!!!

    ReplyDelete
  6. Mh jamani huu sasa mzahaa asee.. si hali ya kawaida hiyo kha!!
    Rabia

    ReplyDelete
  7. Asante wachapishaji.
    Comment zangu: huyo anaesema hakuna ndizi Pemba ziko bukoba tu basi kipofu au hazimo,
    2. basi aseme pia hakuna watu wanaoishi huko ili kumfurahisha. Na ingekua vizuri mtu akiambiwa ndizi hizi kutoka Pemba , asirukie kusema ahhh Zanzibar,kwani ni visiwa vya zanzibar na pemba na lazima ajue tafauti ya majina na maumbile ya ardhi.
    3.Kama mkulima au mtaalamu hili lisingempitia nyuma ya kisogo mtaalam yeyote

    ReplyDelete
  8. Ninavyowajua waganguzi,hapa watakuwa wanadanganya watu kuwa kuna mizimu,mara kuna baraka mara kuna hili ,mara lile.Uongo mtupu nikutaka kuibia watu kwa ujanja ujanja tu.Hii ni hali ya maumbile yasiyokuwa ya kawaida ,kama inavyotokea kwa watu ,wanyama wala haina uhusiano na mizimu wala chochote.MSIDANGANYIKE!!!!!!.

    ReplyDelete
  9. mi nataka kumuuliza huyo aliyesema kuwa Pemba hawana jeuri hiyo.hivi imehusu na nini kufananisha jeuri za pemba na bukobaaa????????????? ama ni kutaka kuonyesha uracist kwenye mkungu wa ndizi? kijana jaribu kutumia ulimi wako vyema usiwe unapayuka tu. wacha kukosoa ardhi wakati hujui madini yake..haya huo umetokea bukoba na huyo aloandika kuwa umetokea huko alikuwa haoni au kagaiwa picture? basi atokee mwengine aseme mkungu huu wa ndizi umetokea Moshi machame..angalia kauli kijana utaumbuka.usiwe na kauli chafu kama mkojo.

    ReplyDelete
  10. Duh kuna haja ya migomba nayo kutumia dawa za uzazi wa mpango.

    ReplyDelete
  11. Ndugu zanguni,
    Huo mkungu hauko Tanzania, Pemba. Uko nchini Malaysia - sehemu inaitwa Kerala. Angalia hapa:-

    http://images.google.com/imgresimgurl=http://www.malayalamrocks.com/fun/wpcontent/uploads/2009/12/keralabanana.jpg&imgrefurl=http://www.malayalamrocks.com/fun/biggest-banana-foundinkerala/&usg=__kOofbktjaA3MAQRhKNR4C5CE0SU=&h=666&w=499&sz=336&hl=en&start=3&sig2=MXAAMjQhplsfnOfwWPbGHg&um=1&itbs=1&tbnid=wBdNTAD-c4T_IM:&tbnh=138&tbnw=103&prev=/images%3Fq%3Dlargest%2Bbanana%2Bbunch%26um%3D1%26hl%3Den%26client%3Dsafari%26sa%3DN%26rls%3Den-us%26tbs%3Disch:1&ei=qgiQS8z5BY3atAOJwNSsCA

    ReplyDelete
  12. JAMANIII TUAMKE SASA. KAMA KWELI HUO MGOMBA UMEANGUSHA HUO MKUNGU, WATU WACHAMGAMKIE KWENYE GUINESS WORLD RECORDS NA KUIWEKA ZENJI KATIKA HISTORIA YA KUWA NA MMEA WA AJABU KAMA HUO. TUAMKE JAMAA WATU WANACHUKUA MISHIKO YA REKODI KWA KUPUNGA MAKAMASI SEMBUSE HUO MGOMBA?

    ReplyDelete
  13. Wadau (Tarehe Thu Mar 04, 04:05:00 PM) na (Thu Mar 04, 06:00:00 PM) acheni JAZBA hapa hakuna tusi ama nini hapa ni katika kuchangia kufurahisha watu tu. Sasa vitisho na matusi ya nini acheni "Inferiority complex" inawaandama mpaka kwenye vitu vidogo. Umaarufu wa ndizi ni Bukoba, Moshi na Mbeya kwa Tanzania,ingawa sehemu nyingine zalimwa pia hii inajulika mahoteli wauliza ndizi za moshi ama Bukoba. Ni sawa na kusema karafuu zatoka Mbeya na Mpemba akitania kuwa ni wa Pemba siyo tusi. JAZBA zawafanya hata msisome vizuri hakuna aliyesema hakuna ndizi pemba, Acheni utoto wa kutishia watu nyau.

    ReplyDelete
  14. Kha jemen,Manyoooooyaaaaa tena!

    ReplyDelete
  15. KWENYE UKURASA WA KWANZA WA GAZETI LA JAMBO LEO LA LEO IJUMAA MACHI 5,2010 IPO PICHA KUBWA YA HUU MKUNGU NA MAADOKEZO YAKE.HII DAHANA YA KUINGILIA UUMBAJI WA MUNGU KWA KUKEJELI MAENEO FULANI SI BUSARA SANA.OMBI LANGU NI AINA HIYO YA MIGOMBA KUSAMBAZWA KWA WAKULIMA ILI IWASAIDIE KWA LISHE NA UCHUMI WA FAMILIA.

    ReplyDelete
  16. Mdau wa Thurs Mar 4 10:45 Mkungu huo ni kutoka India.

    Kerala iko South India na sio Malaysia. Mimi nilishaona picha hiyo kama miezi sita nyuma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...