Dkt. Getrude Mongela akiwasalimia wajumbe wa mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake baada ya kutambuliwa mbele ya wajumbe hao ambao walimshangilia kwa nguvu. Getrude Mongela alikuwa Katibu Mkuiu wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa wanawake uliofanyika Beijing-China, mkutano huu wa 54 unafanyika ikiwa ni miaka kumi na tano tangu kufanyika kwa mkutano wa Beijing mwaka 1995.
Mbunge wa Peramiho na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Jenista Mhagama akifuatilia mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Hali ya Wanawake, kulia kwake ni Mkurugenzi wa jinsia, kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bw Mechack Meliyo Ndaskoi
Wajumbe wa kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakishiriki mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Kuhusu hali ya wanawake. Mstari wa Mbele kushoto ni Bi Rahma Khamisi,Mkurugenzi Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto. Katibu Mkuu Bi Rahma Mshangama, wengine ni Mwanaidi Salehe Abdalla, Bi. Mariam Mwafisi Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi Wahida Mohammed, Mhe. Jenista Mhagama (MB) Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya JamiiWANAWAKE


WANAUWEZO WA KUONGOZA NCHI-MONGELA

Na Mwandishi Maalum

New York - Imeelezwa kwamba, mwanamke wa Afrika anauwezo kwa kushika madaraka makubwa ya kiserikali yakiwemo ya kuongoza nchini.

Maelezo hayo yametolwa na Dkt. Getrude Mongela, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa Nne wa Kimataifa wa wanawake uliofanyika Jijini Beijing China mwaka 1995.

Ametoka kauli hiyo wakati akichangia mjadala kuhusu miaka Kumi na Tano ya Tamko la Beijing –‘ajenda ambayo haijakamilika’.

Akamtaja Rais wa Liberia, Ellen Johson- Sirleaf ambayeni mwanamke wa kwanza barani Afrika kuwa kiongozi mkuu wan chi kwamba ni ni mfano hali wa kwamba wanawake wanaweza.

“ Ninachoweza kutaja kama changamoto, miaka kumi na tano baada ya Tamko la Beijing ni kwamba , wanawake bado hawajashika madaraka makubwa ya kiserikali , serikali nyingi bado zinashikiwana kuendeshwa na wanaume ukiondoa ile ya Liberia. Hili ni tatizo kwa sababu wanaume bado ndio watoa maamuzi wakubwa katika taasisi mbalimbali za kiserikali”. Anasema Dkt. Mongela

Na Kuongeza .“Kabla ya Tamko la Beijing, nani aligetemea kama mimi ningeweza kuwa Spika wa kwanza mwanamke wa Bunge la Umoja wa Afrika. Miaka kumi na tano iliyopita hapa kuwa na Rais Mwanamke katika ardhi ya Afrika lakini leo tunaye Ellen Johnson- Sirleaf ambaye alisimama kidete kwaajili ya Liberia:”.

Dkt. Mongela ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ukerewe, alishangiliwa sana na wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa 54 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake ,wakati alipotambulishwa kama mmoja wa washiriki wa majadiliano hayo.


Mongela ambaye alikuwa mmoja wa wanajopo katika mjadala huyo, ambao ulifanyika mara baada ya Katibu Mkuu Ban Ki Moon kusoma hotuba yake ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mwanamke ambayo imefanyika March Moja hapa Umoja wa mataifa.

Akielezea ni jambo gani linalomfanya mwanamke wa Afrika awe tofauti na wengine. Mongela anasema jambo kubwa linalomtofautisha mwanamke wa afrika ni utu na hadhi yake.

”tofauti kubwa ya mwanamke wa kiafrika ni utu na hadhi aliyonayo, mwanamke wa kiafrika daima husimama kidete na ni mpiganaji. Na tamko la Beijing la mwaka 1995 limewapa fursa na nafasi nzuri ya kupigania na kutafuta haki zao” anabainisha.

Na kuongeza kwamba jumuia ya kimataifa inatakiwa kulitambua . na pia kujifunza kwmaba Tamko la Beijing limempa mwanamke nguvu ya kupiga hodi na kufungua milango ya majadiliano.

Anasema ni tamko ambalo limemuweka mwanamke karibu zaidi na mwanaume na mwanaume kuwa karibu zaidi na mwanamke.

“ Leo hii kila mtu anatambua kwamba mwanamke naye anayohaki ya kuishi katika dunia. Wanatambua kuwa mwanamke na mwanaume lazima washirikiane. Kwa sababu hata wanawake walishiriki katika kupingania uhuru wan chi zao. Wanaume hawana namna nyingine zaidi ya kukubali” anasisitiza Mongela.”

Akatoa wito kwa wanawake kutoka kata tamaa kwani hatua kuna mafanikio ambayo yamekwisha kupatikana baada ya tamko la Beijing. Na kinachotakiwa ni kuongeza kasi ya kutekeleza yale ambayo bado yajafanyiwa kazi.

Aidha anawahamasisha wanawake kujihusisha na kushiriki kikamilifu kuyatafutia ufumbuzi matatizo yatokanayo katika nchi zao.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kwenye mkutano wa kina mama hiyo njemba hapo pembeni inafanya nini?

    ReplyDelete
  2. Wanawake wa kiafrika ndio wanaweza. Lakini kama Tz yetu wnaowezeshwa ni wale tu wasiokuwa na waume. Ina maana wenye waume bado ukandamizaji upo. Kuna makabila yanayoruhusu wake zao kushiriki masuala ya kijamii, lakini kuna mengine kama Wachagga,mkewe akipanda chati ni balaa. wivu kibao tena wivu wa " kwa nini kafanikiwa" na hapo itakuwa sio mme tu hata mawifi , mashemji na wakwe. Wachagga wanahitaji semina ili waweze kuruhusu wake zao ktk masuala ya uongozi

    ReplyDelete
  3. mkataissueMarch 05, 2010

    kichwa kiwe mkutano unahohusu maendeleo ya wanawake na sio mkutano wa akina mama.
    BTW si kila mwanamke ni mama

    ReplyDelete
  4. Tatizo ambalo kwa sasa bado tunalo ni kuwa adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake. Ukweli ni kuwa, wanawake wenyewe bado wana fikra duni ya kuona mwanaume ndie anaeweza. Wanawake hatupendani, wanawake ndio tunaopigana vita, wanawake hatuchaguani kwenye uongozi. hili hasa kwa mtizamo wangu ni fikra finyu ya baadhi ya wanawake kujiona hawawezi kufanya kitu chochote bila mwanaume na hivyo kumuona mwanamke mwenzake hafai. hili lipo sana na ndi maana utakuta hata wachangia mada wameshaanza kusema kuwa WALE WASIO NA WANAUME NDIO WANAPEWA VYEO, hili linatokana na ukweli kuwa wenye wanaume bado wanategemea kauli kutoka kwa waume zao, lakini swali ni kuwa je WAUME ZAO WANATEGEMEA KAULI KUTOKA KWA WAKE ZAO? hapa baaaado sana.

    ReplyDelete
  5. Tatizo la kwanini wanaume wanawakataza wake zao kujitokeza ni mila na desturi potofu zilizojengeka kwenye makabila mengi ya kitanzania. yaani hata mwanamke akienda kusoma tu kila mtu ananyanyua bango ohoo ametawaliwa, ohoo atakoma. Utakuta wanawake wanaosoma wanateseka sana, baba mkwe, mama mkwe, mawifi ah jamani, lakini kijana wao akienda shule basi wanatangaza kila kona mtoto wetu yuko UK, sijui yuko wapi, ila akiwa ni mwanamke utasikia ohoo anasoma ili amkalie kijana wetu. matokeo yake mwanaume anakuwa mkali, mlevi na manyanyaso kibao. SIJUI KAMA TUTAFIKA ILA NYIE MNAOFANYA HIVI ACHENI KABISA KUNYANYASA WAKE ZENU. HAKUNA ANAESOMA ILI AMTAWALE MTU, ELIMU SIO YA KUTAWALA.

    ReplyDelete
  6. mama si unyamaze tu! ukerewe tu imekushinda sembuse tanzania!!

    ReplyDelete
  7. Ninakubaliana na mama momgella. Jamani wakati umefika tuwapeni wanawake urais. wanawake au akina mama huwa ni wakali sana lakini pia wana huruma mwingi. kwa kuwaonea huruma walalahoi watakuwa wakali kwa mafisadi. kama chukua chako mapema (CCM) wanawawekea mizengwe, basi njooni kwetu sisi je? (CCJ) tumewatengea wanawake nafasi ya urais.

    ReplyDelete
  8. Mama yetu huyo mama mogella manake nilifkiria kashastaafu michuzi nishakwambiaga ujiunge twitter tuwe tunakufata kila sehemu unayoenda ila naona bado manake kina mama kama hawa ndio tunapenda kuwaona badala ya kusikia kutoka kwa watu.

    ReplyDelete
  9. mashaallah! hijambo hijabo spread the word ladies mukili mubimba.

    ReplyDelete
  10. bi rahma khamis nakupa tano mwanangu wee.
    mdau wa NY

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...