habari yako ankal
nimepatwa na tatizo naomba wadau wanisaidie, hivi fisadi kwa kiingereza wanaitwaje?

Nimehamia kama miezi sita hapa Ilford, UK, na familia yangu tukitokea bongo. Nina mtoto wa miaka 4 ambaye yupo bado pre-school, sasa amepewa swali shule kwamba akiwa mkubwa anataka awe nani? akaandika kwamba anataka awe fisadi,hilo neno fisadi akaandika kwa kiswahili kwahiyo mwalimu wake akashindwa kumuelewa, ndipo aliporudi nyumbani kuniuliza kwa kiingereza fisadi ni nini maana yake maana yeye anataka kuwa fisadi.

Niliishiwa nguvu. Na ili kumuweka sawa ikabidi nimwambie kwamba hauwezi kuwa fisadi mpaka uwe kiongozi serikalini,dactari,mwanasheria na n.k halafu ndio cheo cha ufisadi kinakuja. Amekubali kuwa kuanzia na ubunge,ila bado anataka kujua maana ya fisadi kwa kiingereza na mimi pia sijui hawa watu wanaitwaje.
naomba msaada wenu.
yaani sina mtoto...
Mdau Ilford, UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Wazungu wanasema an apple doesn't fall far from the tree, Waswahili wanasema mwana wa nyoka ni nyoka.
    Unaweza kupata tafsiri ya fisadi mtandaoni kupitia hapa:
    http://kamusi.org/en/lookup/sw?Word=fisadi
    Mafisadi wa bongo ni 'corrupt people'

    ReplyDelete
  2. very creative indeed, either way, that is.nimecheka sana.......wenzangu vipi?

    ReplyDelete
  3. Hiyo kali mno! Nimesoma hiyo post asubuhi nimecheka sana...siku itakuwa poa sana! Hapo kweli hauna mtoto! Majibu yako pia mazuri.

    ReplyDelete
  4. nimecheka mpaka mbavu zimeuma na kichwa kilichokuwa kimeanza kuniwanga kwa uchovu kikapata nafuu!
    CCM hawakuwa na msamiati huu hadi hivi majuzi na kwa hiyo kamusi za TUKI wasingeweza kuliingiza katika kamusi zao.
    FISADI ni KLEPTOCRAT
    UFISADI ni KLEPTOCRACY
    ukigoogle utapata maelezo marefu na yote yanasadifu kabisa hiyo hali tunayoshuhudia katika our beloved bongoland.

    ReplyDelete
  5. Inachekesha .......

    ReplyDelete
  6. Yaani inachekesha mpaka basi! Na inasikitisha pia kwa kweli. Mtoto unaye bwana, Ila majibu yako yanaweza kumtatiza baadaye.Kwani huwa unamdanganya vitu vingi? Na baba asiyesema kweli naye anaitwa nani kwa kiingereza? ha ha! Ila mara zote penda kuongea na mtoto ukweli kwa lugha rahisi. Kwa mfano hapo tumia nafasi hiyo kwanza; kumpongeza kuwa kumbe anasikiliza habari, pili; kwamba ana kumbukumbu nzuri, tatu; kumuelewesha kwamba fisadi si mtu mzuri ni mtu anayetumia nafasi yake vibaya na pia ni mbinafsi. Kama una mtoto mwingine mkubwa kwa huyo au mdogo tumia mfano namna ambavyo mtu yeyote anaweza kuwa "fisadi" katika nafasi aliyonayo ili yeye aelewe na asipende kuwa fisadi kwa uelewa wake mdogo. Inabidi kuwafundisha watoto kuhusu maisha kwa mbinu kama hizo mara zote. Nafasi kama hizo kwa kiingereza huitwa "Teachable moments" tuzitumie. Nakutakia malezi mema!

    Wasalaam,
    Leanji- Dar

    ReplyDelete
  7. Fisadi ni ==> Libertine

    Shughuli!!!!

    ReplyDelete
  8. kwanza nakupa pole kwa mtoto kutaka kuwa hivyo . Huyo mtoto anajua hanacho taka ila uwe makini sana maana umemleta huku akiwa mdogo sana nasujui kama utakuwa na muda nao wa kuwa karibu nao au utawapa kila kitu wanacho taka hasa {INTERNET COMPUTER} maana watoto huku ndio wana haribikiwa sana na mamabo hayo.
    kwa hiyo wewe jitahidi sana kuwa karibu sana na watoto wako OK..

    ReplyDelete
  9. Duh!!
    Pole sana,mwanao amekuwa akisikiliza kwa makini radio na mongezi ya kitaa,sasa unaweza kumwambia fisadi ni anayejilimbikizia mali bila kiasi,-Capitalist. ili mwalimu amuelewe,
    au umwambie kuwa fisadi ni mtu anayepnda wake za watu,akiwa ameoa,etc
    mfano mzuri kwa UK ni King Henry ambaye alioa wake kibao na kuwaua wengine ili apate kuoa mpya.

    all in all jiandae na darasa la sex education na Ukimwi,kwani siku hizi darasa linaanza mapema kabla ya practicals.

    :)

    ReplyDelete
  10. Duh...kweli huna mtoto....ila hakikisha unamkatia kadi ya CCM ili aweze kutimiza ndoto yake

    ReplyDelete
  11. Fisadi ni jizi, tapeli, nyangau linalotumia mbinu mbalimbali za udanganyifu(wizi) kujipatia mali ya umma au ya kundi la watu au mtu mmoja mmoja ili kujinufaisha lenyewe.
    Kwa mfano kama ilivyo kwa wafanyakazi wa serikali ya Tanzania tenders zote zinanuka ufisadi!!!! au utapeli au kwa maana nyingine corruption

    ReplyDelete
  12. Abiola Wa Kuchovya, Mikanjuni, TangaMarch 01, 2010

    Mambo ya kudanganya watoto wadogo mwenzio nimekoma, mweh!! Aligombana na watoto wenzake wakati wanacheza wakamwambia toka hapa we Msenge. Alipokuja kuniuliza maana yake nikamwambia asilie MSENGE ni mgeni. Siku nyengine walikuja wageni nyumbani kwangu akawashangilia akiwaita Wasenge hao, wasenge haoo. Akanifuata bustanini akaniambia wasenge wawili wamekuja na amewakaribisha sebuleni, NIMEKOMA

    ReplyDelete
  13. sasa mimi apa ndo nimeshikilia mbavu zangu dah!!

    mtoto anaitaji maombi haraka mdau,unasikia?yani upesi maana kimtokacho mtu ndicho kilicho moyoni mwake na akilini mwake

    na ivi ni mtoto?basi kimemkaa sali.

    ReplyDelete
  14. abiola wa kuchovya,tanga

    ndo shida na tatizo kubwa sana watoto wakilelewa na baba zao,kuliko mama!!wababa wengi sana WAONGO/hudanganya sana watoto...ndo faida yake iyo

    siku ingine jua kukaa na wanao kuwaelekeza kwa ukweli kabisa,,,

    sina hamu,tuliombee taifa la baadae maana mh,,,,

    ReplyDelete
  15. Kwa kweli Abiola umenichekesha hadi machozi yananitoka. Natamani kujua kilichojiri hao wageni uliwatizama vipi? Kwa kweli watoto wa kizazi cha sasa hakuna la kuwaficha wazazi wenzangu. Much better waelezwe ukweli mapema kuliko kuficha kama ni matusi waambie ukweli. tukificha matokeo yake ni kama ya mtoto wa Abiola pole mwaya

    Mama Karen

    ReplyDelete
  16. NENO FISADI NI PIRATES

    ReplyDelete
  17. nakufa hukuuu nahisi mbavu zangu zinataka kuchomoka mh watu mna mambo nimecheka sana

    ReplyDelete
  18. Sasa Abiola wa Tanga wewe ndo umenitoa zaidi! Heri ya Fisadi wa UK! Mi naona fisadi ungemwambia kwa lugha rahisi kuwa ni mwizi asiyetumia siraha ila kalamu na mdomo na hasa akiwa anatoka ccm.

    ReplyDelete
  19. we abiola ni funga kazi jamani hizi mbavu leo zinauma blogu ya jamii idumu

    ReplyDelete
  20. Kwa kuwa tawi la CCM limefunguliwa UK. Ni rahisi sana kwa mtoto huyo kutimiza dreams zake. Labda ungeulizia tawi la London kama wameshaanzisha chipukizi. Ukamwandikishe mwanao hapo.

    ReplyDelete
  21. bi kidude ana miaka kati ya 103 na 106 sikumbuki exactly mingapi, kuna cku nimeisikia kwenye kipindi cha radio cha asubuhi baada ya saa 3 cha akina dina marios.

    Bibi kafika huko, Je vijana tutafikisha mingapi.(Just a Joke, msinishambulie wadau)

    Ikumbi

    ReplyDelete
  22. Safari ya miezi sita tuu umebeba familia!Hii nadhani ni katika kuhakisha unachukua pesa nyingi iwezekanavyo toka kwa mwajiri!Bila kujali kuhamisha watoto kwa safari ya miezi sita tuu kutawachanganya...basi mie nafikiri Fisadi ni mtu kama wewe!
    So mwambie FISADI NI MTU MBINAFSI KAMA MIE BABA YAKO!

    ReplyDelete
  23. mtoto huyu hudodosa sana na ndiyo makuzi, hongera kwa kuwa na waaina hiyo ila linda asiende kwenye ufisadi huyo

    ReplyDelete
  24. neno FISADI linatokana na neno UFISADI ambalo ni equivalent na neno UCHAFU wa kimaadili,kwa kiingereza =INFIDELITY,yaani mwenendo usiostahili mbele ya jamii na mbele ya mwenyezi mungu.
    hivyobasi FISADI ni INFIDEL.
    Sema limeingizwa katika siasa ya tanzania kufuatia uchafu uliofanywa na baadhi ya viongozi na unaoendelea kufanywa. lakini pia mtu anaweza kuwa mfisadi hata katika tabia zake nyumbani katika mahusiano,yaani ni mchafuzi,a cheater.matendo yake sio safi na hayakubaliki katika jamii kwakuwa yamepotoka mbele ya jamii na mbele za mungu pia.
    mdau.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...