habari yako ankal
nimepatwa na tatizo naomba wadau wanisaidie, hivi fisadi kwa kiingereza wanaitwaje?
nimepatwa na tatizo naomba wadau wanisaidie, hivi fisadi kwa kiingereza wanaitwaje?
Nimehamia kama miezi sita hapa Ilford, UK, na familia yangu tukitokea bongo. Nina mtoto wa miaka 4 ambaye yupo bado pre-school, sasa amepewa swali shule kwamba akiwa mkubwa anataka awe nani? akaandika kwamba anataka awe fisadi,hilo neno fisadi akaandika kwa kiswahili kwahiyo mwalimu wake akashindwa kumuelewa, ndipo aliporudi nyumbani kuniuliza kwa kiingereza fisadi ni nini maana yake maana yeye anataka kuwa fisadi.
Niliishiwa nguvu. Na ili kumuweka sawa ikabidi nimwambie kwamba hauwezi kuwa fisadi mpaka uwe kiongozi serikalini,dactari,mwanasheria na n.k halafu ndio cheo cha ufisadi kinakuja. Amekubali kuwa kuanzia na ubunge,ila bado anataka kujua maana ya fisadi kwa kiingereza na mimi pia sijui hawa watu wanaitwaje.
naomba msaada wenu.
yaani sina mtoto...
Mdau Ilford, UK
Wazungu wanasema an apple doesn't fall far from the tree, Waswahili wanasema mwana wa nyoka ni nyoka.
ReplyDeleteUnaweza kupata tafsiri ya fisadi mtandaoni kupitia hapa:
http://kamusi.org/en/lookup/sw?Word=fisadi
Mafisadi wa bongo ni 'corrupt people'
very creative indeed, either way, that is.nimecheka sana.......wenzangu vipi?
ReplyDeleteHiyo kali mno! Nimesoma hiyo post asubuhi nimecheka sana...siku itakuwa poa sana! Hapo kweli hauna mtoto! Majibu yako pia mazuri.
ReplyDeletenimecheka mpaka mbavu zimeuma na kichwa kilichokuwa kimeanza kuniwanga kwa uchovu kikapata nafuu!
ReplyDeleteCCM hawakuwa na msamiati huu hadi hivi majuzi na kwa hiyo kamusi za TUKI wasingeweza kuliingiza katika kamusi zao.
FISADI ni KLEPTOCRAT
UFISADI ni KLEPTOCRACY
ukigoogle utapata maelezo marefu na yote yanasadifu kabisa hiyo hali tunayoshuhudia katika our beloved bongoland.
Inachekesha .......
ReplyDeleteYaani inachekesha mpaka basi! Na inasikitisha pia kwa kweli. Mtoto unaye bwana, Ila majibu yako yanaweza kumtatiza baadaye.Kwani huwa unamdanganya vitu vingi? Na baba asiyesema kweli naye anaitwa nani kwa kiingereza? ha ha! Ila mara zote penda kuongea na mtoto ukweli kwa lugha rahisi. Kwa mfano hapo tumia nafasi hiyo kwanza; kumpongeza kuwa kumbe anasikiliza habari, pili; kwamba ana kumbukumbu nzuri, tatu; kumuelewesha kwamba fisadi si mtu mzuri ni mtu anayetumia nafasi yake vibaya na pia ni mbinafsi. Kama una mtoto mwingine mkubwa kwa huyo au mdogo tumia mfano namna ambavyo mtu yeyote anaweza kuwa "fisadi" katika nafasi aliyonayo ili yeye aelewe na asipende kuwa fisadi kwa uelewa wake mdogo. Inabidi kuwafundisha watoto kuhusu maisha kwa mbinu kama hizo mara zote. Nafasi kama hizo kwa kiingereza huitwa "Teachable moments" tuzitumie. Nakutakia malezi mema!
ReplyDeleteWasalaam,
Leanji- Dar
Fisadi ni ==> Libertine
ReplyDeleteShughuli!!!!
kwanza nakupa pole kwa mtoto kutaka kuwa hivyo . Huyo mtoto anajua hanacho taka ila uwe makini sana maana umemleta huku akiwa mdogo sana nasujui kama utakuwa na muda nao wa kuwa karibu nao au utawapa kila kitu wanacho taka hasa {INTERNET COMPUTER} maana watoto huku ndio wana haribikiwa sana na mamabo hayo.
ReplyDeletekwa hiyo wewe jitahidi sana kuwa karibu sana na watoto wako OK..
Duh!!
ReplyDeletePole sana,mwanao amekuwa akisikiliza kwa makini radio na mongezi ya kitaa,sasa unaweza kumwambia fisadi ni anayejilimbikizia mali bila kiasi,-Capitalist. ili mwalimu amuelewe,
au umwambie kuwa fisadi ni mtu anayepnda wake za watu,akiwa ameoa,etc
mfano mzuri kwa UK ni King Henry ambaye alioa wake kibao na kuwaua wengine ili apate kuoa mpya.
all in all jiandae na darasa la sex education na Ukimwi,kwani siku hizi darasa linaanza mapema kabla ya practicals.
:)
Duh...kweli huna mtoto....ila hakikisha unamkatia kadi ya CCM ili aweze kutimiza ndoto yake
ReplyDeleteFisadi ni jizi, tapeli, nyangau linalotumia mbinu mbalimbali za udanganyifu(wizi) kujipatia mali ya umma au ya kundi la watu au mtu mmoja mmoja ili kujinufaisha lenyewe.
ReplyDeleteKwa mfano kama ilivyo kwa wafanyakazi wa serikali ya Tanzania tenders zote zinanuka ufisadi!!!! au utapeli au kwa maana nyingine corruption
Mambo ya kudanganya watoto wadogo mwenzio nimekoma, mweh!! Aligombana na watoto wenzake wakati wanacheza wakamwambia toka hapa we Msenge. Alipokuja kuniuliza maana yake nikamwambia asilie MSENGE ni mgeni. Siku nyengine walikuja wageni nyumbani kwangu akawashangilia akiwaita Wasenge hao, wasenge haoo. Akanifuata bustanini akaniambia wasenge wawili wamekuja na amewakaribisha sebuleni, NIMEKOMA
ReplyDeletesasa mimi apa ndo nimeshikilia mbavu zangu dah!!
ReplyDeletemtoto anaitaji maombi haraka mdau,unasikia?yani upesi maana kimtokacho mtu ndicho kilicho moyoni mwake na akilini mwake
na ivi ni mtoto?basi kimemkaa sali.
abiola wa kuchovya,tanga
ReplyDeletendo shida na tatizo kubwa sana watoto wakilelewa na baba zao,kuliko mama!!wababa wengi sana WAONGO/hudanganya sana watoto...ndo faida yake iyo
siku ingine jua kukaa na wanao kuwaelekeza kwa ukweli kabisa,,,
sina hamu,tuliombee taifa la baadae maana mh,,,,
Kwa kweli Abiola umenichekesha hadi machozi yananitoka. Natamani kujua kilichojiri hao wageni uliwatizama vipi? Kwa kweli watoto wa kizazi cha sasa hakuna la kuwaficha wazazi wenzangu. Much better waelezwe ukweli mapema kuliko kuficha kama ni matusi waambie ukweli. tukificha matokeo yake ni kama ya mtoto wa Abiola pole mwaya
ReplyDeleteMama Karen
NENO FISADI NI PIRATES
ReplyDeletenakufa hukuuu nahisi mbavu zangu zinataka kuchomoka mh watu mna mambo nimecheka sana
ReplyDeleteSasa Abiola wa Tanga wewe ndo umenitoa zaidi! Heri ya Fisadi wa UK! Mi naona fisadi ungemwambia kwa lugha rahisi kuwa ni mwizi asiyetumia siraha ila kalamu na mdomo na hasa akiwa anatoka ccm.
ReplyDeletewe abiola ni funga kazi jamani hizi mbavu leo zinauma blogu ya jamii idumu
ReplyDeleteKwa kuwa tawi la CCM limefunguliwa UK. Ni rahisi sana kwa mtoto huyo kutimiza dreams zake. Labda ungeulizia tawi la London kama wameshaanzisha chipukizi. Ukamwandikishe mwanao hapo.
ReplyDeletebi kidude ana miaka kati ya 103 na 106 sikumbuki exactly mingapi, kuna cku nimeisikia kwenye kipindi cha radio cha asubuhi baada ya saa 3 cha akina dina marios.
ReplyDeleteBibi kafika huko, Je vijana tutafikisha mingapi.(Just a Joke, msinishambulie wadau)
Ikumbi
Safari ya miezi sita tuu umebeba familia!Hii nadhani ni katika kuhakisha unachukua pesa nyingi iwezekanavyo toka kwa mwajiri!Bila kujali kuhamisha watoto kwa safari ya miezi sita tuu kutawachanganya...basi mie nafikiri Fisadi ni mtu kama wewe!
ReplyDeleteSo mwambie FISADI NI MTU MBINAFSI KAMA MIE BABA YAKO!
mtoto huyu hudodosa sana na ndiyo makuzi, hongera kwa kuwa na waaina hiyo ila linda asiende kwenye ufisadi huyo
ReplyDeleteneno FISADI linatokana na neno UFISADI ambalo ni equivalent na neno UCHAFU wa kimaadili,kwa kiingereza =INFIDELITY,yaani mwenendo usiostahili mbele ya jamii na mbele ya mwenyezi mungu.
ReplyDeletehivyobasi FISADI ni INFIDEL.
Sema limeingizwa katika siasa ya tanzania kufuatia uchafu uliofanywa na baadhi ya viongozi na unaoendelea kufanywa. lakini pia mtu anaweza kuwa mfisadi hata katika tabia zake nyumbani katika mahusiano,yaani ni mchafuzi,a cheater.matendo yake sio safi na hayakubaliki katika jamii kwakuwa yamepotoka mbele ya jamii na mbele za mungu pia.
mdau.