mpiga bezi wa twanga pepeta jojo jumanne (shoto) akiwa hana hamu wakati Muhtaji, bintiye marehemu Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, akikung'uta gitaa hilo kama hana akili nzuri wakati wa onesho la twanga wikiendi hii Mango Garden jijini Dar. Cheki video yake hapo chini


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Wanawake wanaweza sana.
    Hongera dada.


    disminder

    ReplyDelete
  2. ankal mimi dada namzimia sana kwa sanaa yake hiyo.then full respect hata mavazi yake ni yaheshima tu popote pale umuonapo.sasa ankal naomba siku umtafute ufanye nao mahojiano hapa blog ya jamii,ili tujue historia yake kwa ufupi,kama kaolewa,au ana watoto,au kama anamiliki bend kwa sasa na je bado wanafaidika na kazi za baba yao ?
    ntashukuru sana ankal

    ReplyDelete
  3. Ankol Michuzi, nashukuru kwa video hii, maana nilikuomba utuwekee na kwa kweli nimeburudika binafsi. Bila shaka dada yetu kipaji ni cha kuzaliwa nacho kama urithi kutoka kwa gwiji wa mziki marehemu baba yake na huyu dada. Namtakia kila la heri!!

    ReplyDelete
  4. safi sana mama, yaani we acha tu, mimi ni mwanamke niko huku ughaibuni yaani nikiwaona wanawake wenzangu walivyosonga mbele navutiwa sana yaani sina la kusema. yale mambo ya zamani kuwaona wanawake ni wa kukaa nyumbani tu jamani imepitwa na wakati kabisa. nyie wanawake mnaojidai ni wanawake wa ndoa haya shauri zenu sisi tunasonga mbele hata mtuite majina yote siku mkishtuka mmechelewa, wanawake hoyeeee

    ReplyDelete
  5. Mtoto wa Simba ni Simba hongera saaaaana Binti Mwaruka...

    Baba yako alikua NGUZO ya Muziki Afrika Mashariki na Kati...

    Tunakutakia uzidi kusukuma Libeneke la urithi wa BABA #1 Solist

    Wadau wa Scandinavia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...