
Mambo vp? Kama inafaa hii unaweza kuiweke kwenye blog yetu ya jamii kuonesha wadau wa kanda ya ziwa maendeleo ya huku kwetu.
MV Sengerema ni kivuko ambacho kilipelekwa kwenye ukalavati na sasa kimerudi na mategemeo ni kwamba kitarahisisha sana usafiri kati ya Mwanza na Geita. Ni mategemeo kwamba vitakuwa vikipishana na mwenzake Mv Misungwi na kufanya uvukaji uwe fastafasta.
Wachina nao wanamalizia barabara kama inavyoonekana. Sasa hivi kama unaenda Bukoba ni mkeka yaani ukivuka tu mpaka Kyamyorwa Km 40 hivi kutoka Muleba ambapo utakutana na mkeka mwingine hadi Bukoba na Mtukula.
Tunaipongeza serikali kwa juhudi zinazoendelea.
Ripota wa Globu ya Jamii
Juma Swedi
Sengerema
Mambo ya uchaguzi haya....hamtupati ng'ooo!!
ReplyDeleteKIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI ZIDUMU FIKRA ZA BABA YETU WA TAIFA MWALIMU KAMBARAGE NYERERE.
ReplyDeleteSawa Juma Swedi Kiweke bila shaka ni wewe kama sijakosea ... James
ReplyDeletekwa nini mnatoza "makanyagio" na "ushuru wa kuvuka" kwa wenye magari badala ya kutoza ushuru pekee? wizi mtupu!
ReplyDeleteHizi habari njema..hata kama sio CCM lakini haki zao tuwape Hongeleni serikali kwa hili kama lile la MV Magogoni
ReplyDeleteHongera Mkapa, hizo zote ni project ambazo zilikuwa za Mkapa, kwa taarifa tu serikali ya awamu ya nne haina barabara mpya ambayo imeanza nayo,zote hizo ambazo zipo ukingoni ni za awamu ya tatu, inawezekana kama angekuwa madarakani hizo barabara zote za Singida-Dom,Dar-Mtwara,Kagera-Mwanza zingekuwa zimeshakamilika chini ya mzee mzima Magufuli.
ReplyDeleteHongera awamu ya tatu
Mdau Kanyau
DAWASA na Mwanza wapi na wapi??
ReplyDeletengoja wataalam waanza kupakia ndizi, lazima itafubaa siku sio nyingi sana.
ReplyDeletemtaanza kuona baadhi ya hifaa vya kuokolea watu (ubavuni mwa boat hiyo) havionekani baada ya mwezi tu, vyote vitakuwa kwenye boat za binafsi, wabongo bwana!
Afadhali umenisaidia anony,wa 02:25:00, maana hapa nilikuwa najiuliza hii imekaaje?
ReplyDeleteKumbe vijamba koti vyetu vilivyoibiwa vimetua Mwanza! Huu ni ushahidi tosha-Mdau DAWASA
ReplyDelete