Hello Ankal,
Mambo vp? Kama inafaa hii unaweza kuiweke kwenye blog yetu ya jamii kuonesha wadau wa kanda ya ziwa maendeleo ya huku kwetu.

MV Sengerema ni kivuko ambacho kilipelekwa kwenye ukalavati na sasa kimerudi na mategemeo ni kwamba kitarahisisha sana usafiri kati ya Mwanza na Geita. Ni mategemeo kwamba vitakuwa vikipishana na mwenzake Mv Misungwi na kufanya uvukaji uwe fastafasta.
Wachina nao wanamalizia barabara kama inavyoonekana. Sasa hivi kama unaenda Bukoba ni mkeka yaani ukivuka tu mpaka Kyamyorwa Km 40 hivi kutoka Muleba ambapo utakutana na mkeka mwingine hadi Bukoba na Mtukula.

Tunaipongeza serikali kwa juhudi zinazoendelea.
Ripota wa Globu ya Jamii
Juma Swedi
Sengerema


ubavu wa MV Sengerema
Barabara ikimaliziwa


Mv Misungwi




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mambo ya uchaguzi haya....hamtupati ng'ooo!!

    ReplyDelete
  2. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI ZIDUMU FIKRA ZA BABA YETU WA TAIFA MWALIMU KAMBARAGE NYERERE.

    ReplyDelete
  3. Sawa Juma Swedi Kiweke bila shaka ni wewe kama sijakosea ... James

    ReplyDelete
  4. kwa nini mnatoza "makanyagio" na "ushuru wa kuvuka" kwa wenye magari badala ya kutoza ushuru pekee? wizi mtupu!

    ReplyDelete
  5. Hizi habari njema..hata kama sio CCM lakini haki zao tuwape Hongeleni serikali kwa hili kama lile la MV Magogoni

    ReplyDelete
  6. Hongera Mkapa, hizo zote ni project ambazo zilikuwa za Mkapa, kwa taarifa tu serikali ya awamu ya nne haina barabara mpya ambayo imeanza nayo,zote hizo ambazo zipo ukingoni ni za awamu ya tatu, inawezekana kama angekuwa madarakani hizo barabara zote za Singida-Dom,Dar-Mtwara,Kagera-Mwanza zingekuwa zimeshakamilika chini ya mzee mzima Magufuli.
    Hongera awamu ya tatu


    Mdau Kanyau

    ReplyDelete
  7. DAWASA na Mwanza wapi na wapi??

    ReplyDelete
  8. ngoja wataalam waanza kupakia ndizi, lazima itafubaa siku sio nyingi sana.

    mtaanza kuona baadhi ya hifaa vya kuokolea watu (ubavuni mwa boat hiyo) havionekani baada ya mwezi tu, vyote vitakuwa kwenye boat za binafsi, wabongo bwana!

    ReplyDelete
  9. Afadhali umenisaidia anony,wa 02:25:00, maana hapa nilikuwa najiuliza hii imekaaje?

    ReplyDelete
  10. Kumbe vijamba koti vyetu vilivyoibiwa vimetua Mwanza! Huu ni ushahidi tosha-Mdau DAWASA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...