wachezaji wa simba wakipiga jalamba kabla ya mechi yao na timu mpya machachari ya Zanzibar Ocean View katika mechi ya kitaifa ya kirafiki iliyofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar. timu hizo zilifungana 3-3Mike Barasa (shoto) akimiliki mpira mbele ya beki wa Ocean View ya Zanzibar, Ismail Khamis wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo jioni kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 3-3 Beki wa timu ya Ocean View ya Zanzibar, Abdallah Mwalim akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Simba, Kelvin Chale wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, leo jioni. Timu hizo zilitoka sare ya 3-3
Kikosi cha simba kwenye mchezo wa leo
Ocean View ya Zanzibar





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. zanzibar_mpyaMarch 09, 2010

    Sahihisho hii ni mechi ya KIMATAIFA si KITAIFA (zanzibr ni nchi mbali na Tanganyika)!

    ReplyDelete
  2. Msianze kuleta mambo ya kututenganisha hapa. Maximo akiita wachezaji wa Ocean View kuchezea Taifa Stars wanaichezea bila matatizo.
    Nawapa heko Simba kwa kuonyesha mtizamo wa kisasa katika soka kwa kujaribu kuendeleza chipukizi wao. Ingekuwa enzi zile timu ingeundwa na wachezaji wa ligi kuu peke yake.

    ReplyDelete
  3. Kuna mtu anaweza kutuandikia majina ya hao wachezaji wa simba tuwajue?

    ReplyDelete
  4. Iweje timu kubwa kama simba icheze na wachezaji wakiwa wamevaa jezi zikiwa zimetofautiana?Ina maana wana upungufu wa jezi? Vitu vidogo kama hivi vinaipunguzia hadhi timu kubwa kama simba..hata kama mechi ilikuwa ndogo, wachezaji walitakiwa kuvaa jezi zinazofanana..Hii imenikera sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...