ankal,
tabia nchi sio bongo tu hata huku dubai mambo ni tambarare kama huko
jamaa kasusa gari
dereva teksi analalamika wakati abiria anaamua kutumia TZ 11
madenti wakiwahi nyumbani
ustaadh anasaka pa kusomea magazeti
ngoja tulibebe....






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. baada ya muda hayo magari utakuta yanauzwa bongo,hapo lazima mtu aliwe.

    ReplyDelete
  2. we michuzi hujatiulia wewe eti ustaadh anasaka pa kusomea magazeti hahahahaaaa,uko juuuuu kaka

    ReplyDelete
  3. MIUNDO MBINU MIBOFU, SIJUI HAWA JAMAA WANAFANYA NINI KAZI KULA MAHELA YA WANAINJI TUUUUU!

    ReplyDelete
  4. HAYA SI MAFURIKO BALI NI MAJI YALIYOTUWAMA BAADA YA KUKOSEKANA MIFEREJI YA KUONDOA MAJI YA MVUA. MSITUJENGEE HOJA YA KUOMBA MISAADA NJE ILI MNEEMEKE.

    ReplyDelete
  5. kimyaaaaa, kina john mashaka mko wapi na lawama zenu.

    ReplyDelete
  6. Mie mbavu sina Ustadhi anasaka pakusomea Gazeti hahaha. Na hii Yangu Jamaa kwenye Taxi anachukuwa Taxi anamwambia mpaka Home ila Bei itabidi ipungue hahaha. Issa.

    ReplyDelete
  7. Sidhani kama hilo ni tatizo la tabia nchi (glubo woming). kinachochangia zaidi ni udhaidu wa kutengeza mipango miji inayo endana na miundo mbinu vizuri zaidi.

    siku zote kunaeza kuwa na mafuriko mahali popote pale lakini unapokuwa unapanga kukua kwa mji ni lazima uweke miundo mbinu itakayoweza kusapoti mjini huo.

    Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni kuwa unapojenga mahali fulani ujue unaharibu uhasilia wa mhali hapo, kwa mfano unaharibu jinsi gani maji yalikuwa yakitiririka pale mvua inaponyesha.

    Kwa hivo basi ni lazima uyaonyesha hayo maji ss yaenende wapi kwa sababu umeyakinga yasiende mahali yalikuwa yanaenda kabla hujajenga eneo hilo.

    Kinachotakiwa na kinachofanywa na miji ya kisasa ni kujenga mifereji mikubwa sana ya kukusanya maji ya mvua (stormwater) na kuyapeleka aidha kwenye bwawa, mtoni, baharini au mahali pengine popote ambako maji hayo hayatasababisha madhara makubwa na pia hayo maji ya mvua mara nyingi huwa hayawi treated kama maji machafu kwa ivo unaeza kuyarelease mtoni salama tu.

    ReplyDelete
  8. Sikujua kama tabia nchi inaitwa Behavior. Kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  9. Tafadhali mleta taswira hizi kuwa makini na mkweli hizo taswira ni Sharjah na si Dubai! tafadhali rekebisha!

    ReplyDelete
  10. Hapo ingenoga zaidi,kama angepita mtoto wa kimanga,lazima angenyanyua hijabu na tungeona mapajazz

    Mdau wa mapajazzzz + matitizzzz

    ReplyDelete
  11. hapo si Dubai, mafuriko hayo yanaonyesha ni Sharjah

    ReplyDelete
  12. Tafsiri ya tabia nchi ni Behavior Country

    Hahahahahaaaa raha

    ReplyDelete
  13. Sasa Ankal unatupa ujumbe gani? Kwamba kwa kua wenzetu nao mitaro imeziba basi na sie tuzisizibue mitaro yetu. Ati wao wakiwa wajinga sie tuwe wajinga zaidi yao?
    Usitetee tabia nchi kwani yale mafuriko ya jana sio tabia nchi ni uchafuzi wetu wa mitaro kwa kushindwa kutunza mazingira yetu na sheria kukosa makali achilia mbali mipango miji mibovu.

    ReplyDelete
  14. pa kusomea gazeti???

    tih tih tih,,,afu ndo zao izo

    ReplyDelete
  15. mwenyeji dubaiMarch 03, 2010

    Hapo si Dubai ni Sharjah....na pia huku ni jangwani mvua ni vitu vya nadra sana na ndio maana hawakuweka mitaro ya kutosha n.k.....huku ni joto na baridi tu mvua ni mara moja kwa mwaka...au pia mnaweza pitisha hata miaka 3 hamna kitu kama hicho.....na si kama uweo hawana....na wala hayo mawazo ati pesa wanakula ni mambo ya viongozi wetu wa africa kwa hawa wenzetu wa UAE...Hata pesa wakila mwananchi hapati tabu .....MTOTO ANASOMESHWA BURE, MATIBABU BURE, KWENYE KAZI NZURI WANAWAWEKWA KWANZA WAO RAIA NA ANALIPWA MSHAHARA MZURI HATA KAMA ELIMU YAKE NI NDOGO...NA KILA MWEZI ANAPATA DOLA 800 KWA KILA MTOTO MMOJA ZINATIWA KWENYE ACCOUNT YA BABA HAPO HATA KAMA WATU WANAKULA PESA UNALALAMIKA KWELI?? MANA PESA UNAYOPATA NI KWA AJILI YA KULA TU NAKUNUNUA NGUO NA MAGARI ....KILA RAIA ANA NYUMBA MAANA NI LAZIMA UKOPESHWE NYUMBA...TUSIJIFANANISHE KABSAA NA HAWA WENZETU.

    NA HAYO MAGARI YANAYOTUMIKA DUBAI NI TOFAUTI NA YA TZ DUBAI MSIKANI UKO UPANDE WA KUSHOTO.

    Watoto wakimanga huwezi kuwaona wanapandisha nguo kwenye maji...kuogelea tu anaogolea na baibui ...

    ReplyDelete
  16. lile jengo lejiao refu ndio limeleta kizazaa limeziba njia za mifer

    ReplyDelete
  17. kutokana na upungufu wa mabwawa ya kuogelea kwa wasio na uwezo{swiming pool} bosi juu {sir god}huona iko haja ya kufanya haki kama lile bango la chama cha wananchi haki sawa{cuf} kila mtu apate japo siku kadhaa za kuogelea katika bwawa huria hakuna upendeleo wala uwezo ndio maana hushusha hii neema kwa wote,hasa kwa wale ambao hawajapata kuogelea katika mabwawa na wale wasio na bahari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...