BALOZI MAALUM WA KAMPENI DHIDI YA AJALI ZA BARABARANI, BI MICHELE YEON RAIA WA MALAYSIA, AKIZUNGUMZA WAKATI BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA, LILIPOUTANGAZA MWAKA 2010-2011 KUWA MWONGO WA KUPUNGUZA AJARI ZA BARABARANI ZINAZOUA MAMILIONI YA WATU KWA MWAKA HUKU ZIKIWAACHA MAMILIONI WENGINE NA ULEMAVU. BI MICHELE YEON NI MCHEZA SINEMA. AKIWA NI MMOJA WA ACTOR MAARUFU KWENYE FILAMU MAARUFU KADHAA ZA JAMES BOND. ANASEMA KATIKA NAFASI ZOTE AMBAZO AMECHEZA KATIKA FILAMU HIZO NA KUJIPATIA UMAARUFU, HAKUNA KATI YA HIZO ZINAZOFANANA NA HESHIMA KUBWA ALIYOPEWA YA KUZUNGUMZIA SUALA YA AJALI ZA BARABARANI, NA KUAHIDI KUIFANYA KAZI HIYO KWA ARI NA JUHUDI KUBWA ILI KUFIKIA LENGO LA KUPUNGUZA AJALI HIZO NA HATIMAYE KUZIFUTA KABISA. ( PICHA NA HABARI KWA HISANI UBALOZI WA TANZANIA UMOJA WA MATAIFA)


NEW YORK-Ongezeko kubwa la ajari za barabarani na zinazopelekea upotevu wa maisha ya ya watu, ulemavu na , ulemavu wa kudumu, kumelifanya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kuutangaza mwaka 2010-2011 kuwa mwongo wa mkakati wa vitendo wa kupunguza ajari za barabarani duniani kote.

Azimio namba A/64/L.44/Rev.1 na ambalo limepitishwa kwa kauli moja na wajumbe wote 192 Baraza Kuu. Pamoja na mambo mengine, linataja hatuka kadhaa zinazopashwa kushukulia ili kupunguza ajari hizo ambazo pamoja na kuwa chanzo vya vifo na ulemavu lakini pia zinaathari kubwa kwa uchumi na maendeleo kwa nchi zenye uchumi mdogo na wakati.

Baadhi ya hatua zinazopendekezwa katika tamko hilo ni pamoja na matumizi ya vidhibiti mwendo, kuacha kutuma ujumbe mfupi wa simu huku ukiendesha, kuvaa kofia za kujikinga na ajali kwa waendesha vyombo vya magurudumu mawili au matatu na kutokunywa pombe huku ukiendesha.

Chimbuko la Azimio hilo ni mkutano wa Mawaziri kuhusu usalama barabarani, mkutano uliofanyika jijini Moscow nchini Urusi mwaka jana.

Katika ripori yake kwa Baraza hilo kuhusu hali ya usalama bararani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, anaeleza kwamba ajali za barabarani zinabaki kuwa tatizo kubwa la kiafya na chanzo kikubwa cha vifo, majeruhi ulemavu wa kudumu duniano kote.

Anasema kila mwaka karibu watu 1.3 milioni hufariki dunia kwa ajari za gari huku watu milioni 20 na 50 wakijeruhiwa. Wengi wa majeruhi hawa ni wa umri wa kati ya miaka 5 na 45 ambayo ni nguvu kazi.

Zaidi ya asilimia 90 ya vifo vyote anabainisha Ban Ki Moon vinatokea katika mataifa ambayo pato lake la kitaifa ni dogo au la kati, ambazo nusu ya magari yote ya dunia yako huko.

Kama hiyo haitoshi Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, anasema katika taarifa yake kuwa ajari za barabarani zinarudisha nyuma mafanikio ya kiuchumi na maendeleo ya binadamu.

Aidha hasara inayotokana na ajari za barabarani duniani kote kwa mwaka ni jumla ya dola za kimarekani 518 bilioni , ikizigharimu serikali kati ya asilimia moja na tatu ya pato lao la taifa.

Takwimu hizo zinaonyesha pia kwamba,katika baadhi ya nchi zenye uchumi mdogo hasara itokanayo na ajari hizo ni zaidi ya misaada ya kimaendeleo ambayo nchi hizo zinapata kutoka kwa wahisani. Na hivyo kuwa mzigo kwa uchumi wa taifa na kuleta athari kubwa kwa huduma za afya.

Mbali ya kuwa na athari kwa serikali, madhara ya ajali za barabarani yanazigusa pia familia, ambapo zinatakiwa kutumia fedha nyingi kugharamia matibabu ya wapendwa wao, gharama za mazishi, na pia ukosefu wa kipato ambacho muathirika wa ajali alikuwa anaingizia familia yake.

Awali wakichangia mjadala wa upitishwaji wa tamko hilo, msemaji kutoka serikali ya Marekani, Bw. John F. Sammis ameeleza kuwa mwaka jana watu 6,000 walipoteza maisha kwa ajari huku nusu milioni wakijeruhiwa.

“ Kama hatutachukua hatua sasa, ni wazi kwamba tatizo hili litaendelea kuwa kubwa kwa kadri idadi ya magari katika barabara zetu inavyozidi kuongezeka, sambasamba na ongezeko la matumizi ya teknolojia za kisasa za mawasiliano kama vile simu za mikononi na vifaa vya kutuma ujumbe mfupi wa maneno” akasema Bw. Sammis.
Naye Bw.Hardeep Singh Puri kutoka India yeye anasema watu 80,000 huathiriwa na ajali za barabarani kila mwaka. Wakati nchini Mexico ambayo ni ya tatu baada ya Marekani na Brazil kwa wingi wa ajali. Kati ya watu 124,000 na 117,000 huathiriwa na ajali kila mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Asante sana ankal kwa taswira hiyo.Hayo mapendekezo ni mema sana na hapa kwetu sasa ni wakati ufaao kufanyiwa kazi na madhamana wetu.Lakini wadau wetu wachangie kwenye suala hili:"JE USAFIRI WA MABASI YA MIKOANI KWA SAA 24 UNAWEZA KUCHANGIA KUPUNGUZA MCHAKAMCHAKA WA MADEREVA WETU?Nauliza hivyo kwa sababu upo msemo usemao nchi inayoendelea kujijenga kiuchumi haipaswi kulala,hivyo mabasi kuacha kusafiri kwa saa 24 ni kulaza uchumi na kujenga misongamano na mchakamchaka kunapokucha.Tafadhali sana wanazuoni mahiri na makini katika tasnia ya usafirishaji karibuni kwenye uwanja wa globu ya jamii.

    ReplyDelete
  2. mwanaume = actor
    mwanamke = actres

    ReplyDelete
  3. Huyu mama ni mcheza sinema tu,lakini kajituma na sasa anafanya makubwa.Anold wa marekani naye alikuwa mcheza sinema lakini leo ni Gavana wa jimbo.Mastaa wetu Bongo, wakivuma kidogo tu,utaanza kusikia vituko vya aibu tupu;mara kaharibu mali za watu kesi iko mahakamani,mara kafumaniwa,mara kavunja kioo cha gari la staa mwenzie,mara kagombana na wazazi wake kakimbilia kwa mpenzie,mara kampiga mwezie jukwaani,mara mimi wa manzese yeye wa morogoro.Nyie ni watu muhimu sana kama mtatambua nafasi yenu katika jamii,acheni sifa za kitoto ,heshimuni kazi zenu,lengeni mbali,jitumeni,iheshimini taaluma,igeni kwa wenzenu mtafika mbali sana.NENO NIMELITOA ,NENO LISHIKENI,NENO LIISHINI,NENO LA HEKIMA,MIMI MTOA NENO ,NENO SIKUWAFICHENI.AMEN

    ReplyDelete
  4. WANAPIGA KELE AJALI ZA BARABARANI...KWELI WAMEKOSA MAMBO MUHIMU YAKUANGALIA...CONGO,AFGHANISTAN , IRAQ, NA SOMALIA HAWASTAHIKI KUANGALIWA KAMA WATU..UKISIKIA ULIMBUKENI NDIO HUU. WANSHINDWA KUZUNGUMZI ABRTION....WATOTO WANGAPI WANAULIWA KWA MWAKA....?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...