Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akiwakabidhi kompyuta wanafunzi wa shule ya Sekondari Isuna na ya Shelui zote za Wilaya ya Iramba,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14. Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akiwakabidhi kompyuta Mkuu wa wilaya ya Iramba Mh.Grace Mesack(kulia)Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Isuna Alice Mlumba na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Shelui Mshamu Manyinja,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14 Afisa wa Vodacom Foundation Grace Lyoni akiwakabidhi kompyuta Mkuu wa wilaya ya Iramba Mh.Grace Mesack(kulia)Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Isuna Alice Mlumba na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Shelui Mshamu Manyinja,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh.Grace Mesack akiangalia jinsi kompyuta inavyofanya kazi baada ya kukabidhiwa rasmi kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14 na Vodacom Foundation kwa ajili ya shule za sekondari ya Shului na Isuna zote za Iramba anaeangalia kushoto Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,Mshamu Manyinja na Alice Mlumba.
Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Isuna na ya Shelui zote za Wilaya ya Iramba,Mfuko huo ulitoa msaada wa kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14.
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia Mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation, umetoa msaada wa Kompyuta 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 14 pamoja na kuunganisha mtandao wa internet kwa shule mbili za Sekondari ya Shelui na Isuna zilizoko Lindi Vijijini ili kuboresha sekta ya Elimu katika shule hizo.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Meneja wa Mfuko huo Yessaya Mwakifulefule alisema kwamba msaada huo ni mwendelezo wa awamu ya tatu ya Mradi wa Ugawahi kompyuta kwa shule za sekondari za vijijini. Katika awamu ya kwanza na ya pili jumla ya shule 30 kutoka mikoa tofauti 15 zilifaidika katika mradi huu.

Alisema huu ni mwanzo tu kwani Vodacom Foundation itaendelea kutoa misaada ya kompyuta katika shule za mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwa unalenga kutoa wimbi la uduni wa Teknologia ya kompyuta na kuinua elimu na kuisaidia serikali kama sekta binafsi siyo kuiachia serikali pekee lazima tuwe pamoja kuendeleza misingi iliyobora ya elimu.

Naye Mkuu wa Wilaya, akipokea msaada huo aliishukuru kampuni ya Vodacom kupitia mfuko wake huo na kusema sera ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kutoa misaada mbalimbali ya kuiokoa jamii kama Vodacom ni mfano wa kuigwa na mashirika mbalimbali ili waweze kuisaidia serikali na wananchi wanaopatwa na upungufu wa vitu muhimu katika jamii.

“Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji ili kuhakikisha kwamba uwekezaji una kua na wawekezaji pia wanapata fursa ya kuchangia maendeleo ya sekta ya kijamii nchini’

Alisema hivi sasa bila teknolojia ya kisasa amna maendeleo na alichukua frusa hiyo ya kuwaasa wanafunzi wazitunze kompyuta hizo na kuzitumia vizuri kwani mpo sambamba na shule zailizoko mjini sasa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. kweli thamani ya computer 20 ni mil 14 tsh???? tena sio flat screen au ndio kujikosha?

    ReplyDelete
  2. haya makompyuta yenye uchogo kumbe bado yapo?
    shame on vodacom hata mimi huo msaada naweza kuutoa kila mtu anatafuta sehemu ya kuyatupia they no longer have a monetary value

    ReplyDelete
  3. 14,000,000 DIVIDE BY 20 = 700,000/-@.

    ReplyDelete
  4. Mdau unaesema unaweza kutoa hayo machogo msaada,unasubiri nini? Taifa hili la wadanganyika linahitaji watu kama wewe,Au ni mbwembwe tu za kwenye blogu humu.

    ReplyDelete
  5. Wana approx moja ni $700. Huwezi bisha kwani hujuhi wamenunua wapi lakini kwa hiyo bei unaweza pata laptop nzuri tu. I am hoping kama unanua nyingi hivyo you can definitely save and get some for less than the price tag.

    ReplyDelete
  6. Nyie mliotoa maoni hapo juu nyambafu kabisa,hivi kama huna hela njaa inakuuma,then msamalia mwema akatoa chakula,unaweza kuchagua chakula?
    Mi nadhani kuwa na kitu na bora kuliko kama hauna kabisa.Kompyuta ni computer tu,vitu ambavyo flat screen or laptop inavyo basi zote zinavyo.
    Pili shule nyingi hazina computer,i think kompyuta ni kompyuta tu ,ukitaka latest version tumia hela zako mwenyewe.

    ReplyDelete
  7. HUYU MICHUZ VP BLOG NZIMA KAJAZA MAPICHA YAKE USHAMBA HUO JAMAN TUELIMIKE!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...