moshi ukifuka toka katika dirisha la ofisi ya mhasibu wa Tanesco Kanda ya Kinondoni Kaskazini iliyowaka moto leo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kulipuka kwa kiyoyozi kulikosababisha moto mkubwa ulioteketeza vifaa vya ofisi ikiwemo kompyuta. sefu la nyaraka nyeti na pesa la chuma humo ofisini inaonekana lilisevu. Inasemekana hii ni mara ya pili kwa kiyoyozi kulipuka katika mjengo huo ulio katika barabara ya Bagamoyo road jijini Dar
wafanyakazi na walinzi baada ya kupambana na moto huo kwa kutumia maji
wafanyakazi na walinzi wakiondoa vilivyonusurika
vilivyonusuka vikihamishwa
wafanyakazi wakiwa wametaharuki
baadhi ya vifaa vilivyoteketea
fundi akikata umeme kwa tahadhari.
wafanyakazi wakiwa nje ya jengo hilo
walinzi wa kampuni ya Stemo Security System wanaolinda jengo hilo wakijadiliana baada ya kufanikiwa kuokoa jengo hilo kwa kupambana na moto huo. Toka shoto ni Laurian Ilonganya, Lawrence Mushi, Jeric Ayubu na Daudi Changulula
mlinzi shupavu Laurian Ilonganya akinywa maziwa baada ya kufanya kazi ya ziada kupambana na moto huo akiwa wa kwanza kuvunja mlango na kuingia na ndoo za maji kabla wenzake hawajaja kumsaidia. Inasadikika madhara yangekuwa makubwa zaidi endapo kama asingejitolea mhanga kupambana na moto na kutia moyo wenzake. Wafanyakazi wengine wote katika ofisi hizo walitoka mkuku, huku vifaa vya dharura vya zimamoto vilivyopo mjengoni humo ikisemekana havifanyi kazi. Wengi walidai kuwa Bw. Laurian Ilonganya, aliyeiambia Globu ya Jamii kuwa alipata mafunzo ya dharura ya kuzima moto, anastahili tuzo ya ushupavuHABARI ZILIZOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE ZINARIPOTI KWAMBA JENGO LA MAKAO MAKUU YA SHIRIKIA LA UMEME (TANESCO) KANDA YA KINONDONI KASKAZINI LILILOPO BARABARA YA BAGAMOYOY ROAD JIJINI DAR LINAWAKA MOTO.
RIPOTA MTEMBEZI WA GLOBU YA JAMII ALIYEFIKA MJENGONI HAPO MUDA MCHACHE BAADA YA MOTO KUDHIBITIWA ALIAMBIWA KUWA CHANZO NI SHOTI YA UMEME KATIKA KIYOYOZI KILICHOKUWA NDANI YA OFISI YA MHASIBU NA KUSABABISA MOTO MKUBWA.
WASHUKURIWE WALINZI WA KAMPUNI YA STEMO SECURITY SYSTEM WANAOLINDA JENGO HILO, KWANI WALIPAMBANA NA MOTO HUO NA KUFANIKIWA KUUDHIBITI KABLA HAUJASAMBAA OFISI ZINGINE. MLINZI LAURIAN ILONGANYA NDIYE ALIYEJITOLEA MHANGA KWA KUVUNJA KIOO CHA DIRISHA NA KUINGIA NDANI KUPAMBANA NA MOTO KWA KUTUMIA MAJI YA BOMBANI, KWANI VIFAA VYOTE VYA KUZIMIA MOTO VYA DHARURA ILISEMEKANA VILIGOMA KUFANYA KAZI. IKABIDI ZITUMIKE NDOO
HAKUNA ALIYEDHURIKA KATIKA TUKIO HILO, INGAWA BAADHI YA VIFAA VYA OFISI IKIWEMO KOMPYUTA NA MAKARATASI KADHAA VILITEKETEA KABISA.


Waswahili wana msemo mmoja usemao "Mwosha huoshwa". Hao Taanesiko wamezoea kutuchomea nyumba zetu kwa umeme wao usio na viwango, leo yamewarudia wenyewe nao waonje adha ya kuunguliwa nyumba. Wasisingizie AC. Ni uzembe wao kutojali malalamiko ya wateja. Mungu Ibariki Taanesiko
ReplyDeleteMdau Mbezi Louis
Kweli wewe ni "njanga"! Hayaitwi mabwifu, yanaitwa mabhifu. Ndaga fijo
ReplyDeleteNi yale yalee, Mashine ya A/C ndani ya Ofisi ya Mhasibu yasababisha itilafu,mmmh
ReplyDeleteAsante ankal kutuletea habari mapema, du moto unaanzia kwenye ofisi ya mhasibu, du kuda...dadeki bongo bongoa. La msingi hakuna aliyedhurika na watafunaji wa fedha zetu wataendelea kwani kumbukumbu zimeungua.
ReplyDeleteThe Kalija
Ankal vipi huko bungeni nako kunani? nasikia vipaza sauti vilileta shida sana!! tutafutie ma newss hayoo..
ReplyDeletewaaache na wao waunguliwe. Wamesababisha hasara nyingi zisizo hesabika majumbani mwa watu.
ReplyDeletePapaa Ramses umenusurika?
ReplyDeleteKuna documents zilikuwa zimepangwa kuteketezwa makusudi ama ndio ajali kweli? Au hilo jengo mlikuwa hamlitaki? Kwa vile wana wenzenu wa wizara wamehamia Mafuta House basi na nyie mnataka? Kwani Umeme House ya Ubungo haiwatoshi?
Anyways, poleni.
hebu waache kutuzinhua hapo wamefanya dili la kuiba pesa ili waseme zimeungua hebu watwambie hela zimepona au na kwanini moto uanzie kwa mhasibu hilo tatizo walikuwa hawalioni
ReplyDeleteNo doubt that the causes of that fire is arsenic... period, forensics expert need to nail down these criminals wanaiba na kuharibu mali ya walipa kodi just to get a rid of evidence and cover their tracks.
ReplyDeleteMdau DC
It is high time that TANESCO had a taste of their own medicine!
ReplyDeleteAwali ya yote ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwani hakudhurika mtu...
ReplyDeleteWizi na Ufisadi Mtupu !!!
ReplyDeleteTunashukuru Mungu kusikia wanadamu wamesalimika Tanesco mnaona sasa matatizo yanawagonga wenyewe kwa "ZULMA" wacheni zulma za kuwakatia watu umeme mwisho Vitu vyao vya umeme vinaripuka sasa Jana ilikuwa kwao leo kwenu hatujapenda habari hizi ila muda mwengine tunaona sawa tu. Ndosi.
ReplyDeleteKunradhi, huyo Ndossi aliyechangia hoja hapo ni yule aliekuwa mwalimu wa shule ya msingi ya Muhimbili Primary School?
ReplyDeleteKama ndie mwaga macontacts tafadhali, long time no see!
Sie Ndosi wengi ila yule najuwa alikuwa mwalimu Shule ya Msingi Muhimbili.
ReplyDeleteMie ni Ndosi mshabiki wa Arsenal sio mwalimu wa shule ya Msingi.
ReplyDeleteNdosi
Tatizo la kuwapa kazi watu wasiosoma,Maana elimu ndogo atafanyeje kazi???Kweli bongo tambarale
ReplyDeleteHongera kaka mlinzi uliyejitahidi kupambana na moto huo kwa hali ngumu na ya riski wewe na walinzi wenzio.uskute wenzio walikuwa wanajaribu kupoteza uthuhuda.ukute wamekutolea mijicho,weweee!!tunashukulu sasa i hope havikuteketea ili waumbuke.sasa wale wanaojiita wapelelezi wawajibike hapo.watu waache ujinga bongo tuamke.i like this blog,inaweka mambo open sasa hivi kila mtu ukifanya kitu fikiria the next thing iko michuzi yeee!!
ReplyDeleteHII NI HALI HALISI KILA KIKICHA MAANA HIZO ITILAFU ZA A/C HAZINA WAALAMU KIZIKAGUA MARA KAWA MARA, NAPENDA KIPATA TAARIFA YA MAANDISHI LINI MARA YA MWISHO ILIKANGULIWA NA HATUA GANI ILICHUKULIWA KIMAANDISHI NANANIALITIA SAINI , MAANA RASIRIMALI ZA TAIFA ZINATEKETEA MWISHIWE MWANANCHI NDIO ATALIPA FIDIA KWA UZEMBE WAWACHACHE ,...........................
ReplyDeleteAfadhali hawa wezi Tanesco nao wameunguliwa. Alafu hapo utamsikia yule dada wa mawasiliano eti, "watu hawafanyi service kwenye nyumba zao ndiyo maana wanaunguliwa". Sasa na nyinyi mmefanya service za aina gani?
ReplyDelete"moto umeanzia ofisini kwa muhasibu" No rocket science needed!
ReplyDelete