
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri nchini (ATE) Dk. Aggrey Mlimuka akitoa Tamko la la chama hicho kuhusu mgomo wa wafanyakazi ulioitishwa na Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA). Kushoto kwake ni Wakili Cornellius Kariwa - Makamu Mwenyekiti ATE na Cisse Mwirabi - Afisa habari Maelezo
Tamko lililotolewa na ATE linasema:
Notisi iliyotolewa ni ya mgomo usiohalali
Notisi iliyotolewa ni ya mgomo usiohalali
kwa kuwa sababu za mgomo hazipo.
(a) Njia za majadiliano bado zipo wazi na wala majadiliano hayajafungwa wala kushindikana.
(b) Mgomo uliotangazwa hauna kipindi maalum kinyume na matakwa ya kisheria.
(c) Mgomo uliotangazwa unahusu sekta zote za uchumi wa nchi ikiwemo sekta binafsi ambayo ina taratibu zake za kuhakikisha na kulinda maslahi ya Wafanyakazi
(d) Mgomo huu utahusu pia sekta ya huduma muhimu kwa jamii (essential servises) ambazo haziruhusiwi kisheria kugoma.
Kwa kuwa mgomo huu si halali, waajiri watakaoathirika watakuwa na haki ya kuwachukulia hatua za kinidhamu wafanyakazi watakaoshiriki mgomo haramu ikiwemo kuwafukuza kazi, kutokuwalipa mishahara kwa kipindi cha mgomo na hata kuajiri wafanyakazi mmbadala.
(b) Mgomo uliotangazwa hauna kipindi maalum kinyume na matakwa ya kisheria.
(c) Mgomo uliotangazwa unahusu sekta zote za uchumi wa nchi ikiwemo sekta binafsi ambayo ina taratibu zake za kuhakikisha na kulinda maslahi ya Wafanyakazi
(d) Mgomo huu utahusu pia sekta ya huduma muhimu kwa jamii (essential servises) ambazo haziruhusiwi kisheria kugoma.
Kwa kuwa mgomo huu si halali, waajiri watakaoathirika watakuwa na haki ya kuwachukulia hatua za kinidhamu wafanyakazi watakaoshiriki mgomo haramu ikiwemo kuwafukuza kazi, kutokuwalipa mishahara kwa kipindi cha mgomo na hata kuajiri wafanyakazi mmbadala.
Ijulikane kwa kwa wadau wote kwamba sheria zilizopo hazilindi Wafanyakazi wanaoshiriki mgomo haramu. Iwapo mgomo huu utatekelezwa waajiri watakaoathirika watakuwa na haki ya kudai fidia kwa hasara itakayosababishwa na mgomo huo dhidi ya TUCTA iliyoitisha mgomo usio halali.
Tunatoa rai kwa TUCTA na wadau wote waliohamasishwa na TUCTA, waachane na harakati za kuitisha mgomo usio halali na ambao utakuwa ni hasara kwa pande zote.
Tunaisihi TUCTA washiriki kwa dhati majadiliano yenye lengo la kuleta muafaka wa pamoja, kwa hili hakuna njia ya mkato. TUCTA itambue kwamba majadiliano baina ya wadau yanajenga hali ya kuaminiana na mahusiano mazuri endelevu.
Ikumbukwe kwamba, amani na utulivu sehemu ya kazi ni nguzo muhimu za kuongeza na kukuza uchumi na tija kazini, kuwepo kwa ajira endelevu na kupambana na umasikini. Vyama vya wafanyakazi ni wadau muhimu katika kuendeleza amani na utulivu mahali pa kazi.
Habari kamili
UKOSEFU WA UMOJA..... DUH
ReplyDeleteNi kweli TZ kuna hitajika chama cha kusaidia maslahi ya wananchi...Badala ya kufungua matawi ya CCM ulajii huu changamkieni kuanzisha umoja wa chama cha maslahi ya watu...UNION huku tunalipa kila mwezi kuwa member lakini zinasaidia sana. Na mwajiri akijua uko kwenye UNION anakutreat better na kwa heshima.
ReplyDeleteTutakuwa masikini wa kiakili daima.Mtu mzima baba,kiongozi katika jamii na bado haoni umuhimu wa huo mgomo hii inaonyesha jinsi gani tullivyo na wapumbavu wa kimawazo huko juu.Ndugu zetu wenyewe wanatuweka kwenye umasikini.
ReplyDeleteWafanyakazi mumeshanyanyaswa sana, gomeni nami nakuja kuwanunga mkono.
ReplyDeleteBlogger
Angalieni matatizo ya wafanyakazi wa tanzania na maslahi yao halafu mutoe kauli hizi jamani. Mimi ninavyoona ni halali kabisaaaaaaaaaa kugoma.
ReplyDeleteAcheni kuandika upumbavu. Nchi za watu, wafanyakazi wakigoma masilahi yao na mishara yao hulipwa na vyama vyao wafanyakazi. Sasa unaposema au kushabikia mtu agome hapa Tanzania kwa siku tano, halafu tena alipwe mshahara wake uleule, wote na shirika au serikali ni kuendekeza umaskini kwa serikali na kampuni hapa TZ.
ReplyDeleteHatuwezi kuendelea kama tunagoma na tunategemea kulipwa mshahara wote.
Kugoma gomeni lakini mjue kwamba mshahara pia ukatwe kwa siku mtakazogoma.Pia gomeni kwa sababu za msingi, kwamba mna uhakika kwamba mnachogomea mtakipata.
Huwezi goma, kwa kutaka nyongeza ya mshahara wakati unachozalisha kwa ujumla hakionekani, au huduma unayotoa haionekani, au vyanzo vipya vya kupata hiyo fedha hakuna.
Angalieni sana migomo hapa nyumbani haitasiadia kitu bali kurudisha nyuma maendeleo.
Mfano, mtoto kagongwa, wanafunzi wanafunga barabara ya Sam Nujoma, kwa masaa matatu na ndio barabara kuu itokayo bandarini kwenda nje ya nchi na mikoani.
Mwalimu anagoma, kisa mshahara umechelewa, wakati yeye hufundisha mara mbili kwa wiki na siku zingine yuko mtaani katika biashara zake.
Daktari anagoma, kisa hana sehemu ya kukaa, wakati mgonjwa mwenyewe hana hata sehemu ya kuishi au anakula mlo mmoja.
Haya wafanyakazi wanagoma eti hawamtaki boss wao, maana ni mkali na sio rafiki yao.
Migomo mingine mara nyingi ni ya kishenzi na kipumbavu, na hata haina maana ukiiingalia kwa hasara za kifedha zinazoleta kwa Taifa na walipa kodi kwa ujumla.
Narudia tugome lakini tuwe tumeshafanya utafiti kamilifu kabla, tumeangalia manufaa, pia kuhakiki wapi haki tutapata na kweli tukigoma suluhisho tunalo na tunatakiwa kuwaonyesha waajiri kwamba tunajua tunachofanya, na sio kugoma ili bora liende.
Angalia hapa jirani tu, Kenya, ukigoma tu, kwanza umejipa nafasi ya kujifukuzisha kazi mwenyewe, hivyo migomo huwa ni ile kweli yenye manufaa na lazima.
haya ndio matatizo ya ufisadi maana huyu ahuna alichoongea cha msingi unajua ukivaa suti na kujiona huko kwenye ac kila kona auoni umuhimu wa watu wanaoteseka hawa watu mi najua mungu anawaona kabisa na watachomwa moto kweli huko tuendako kisa anataka ubunge wa kuteuliwa na jk jamani kuna walimu huko vijijini au manesi ukiwaona awanatofauti na mkulima anayetegemea jembe la mkono kwa kuvuna debe zake za kula mwaka mmoja tu
ReplyDeletetanzania tubadilike jamani siku zote huyu mtu alikuwa wapi? mpaka jk ameongea leo ndio anakuja
tanzania tutakuja siku moja kuheshimiana tu nyie leeni hayo magonjwa mukafikiri kila siku ni km enzi zile kizazi kimebadilika sasa
this called "DIVIDE AND RULED PRINCIPLE" serikali baada ya kuona kupitia kwa chama cha wafanyakazi imeshindikana kusitisha mgomo imeamua KUWAPURCHASE hao wanaojiita viongozi wa chama cha waajiri Tanzania ili wawajambishe wafanyakazi waogope kugoma... nchi haiwezi kuendeshwa kwa vitisho kamwe ktk dunia hii ya sasa ni kukaa kwenye meza ya mazungumzo na kufikia muafaka ingawa dokezo la POSHO litaandikwa poa tuu tumesha zoea kunyonywa..
ReplyDeleteMDAU KUTOKA UKANDA WA GAZA
TARIME
Wametumwa na serikari hao... angalia mwanasheria wao anavyoangalia utafikiri ndege kanaswa na mtego... mgomo palepale.
ReplyDeletejamani hivi hii serikali inafikiri kwa mshahara wa shilingi 100,000 kwa mwezi mtu atafanyia nini? mbona serikali ina pesa kibao? kwanini isi zielekeze kuboresh amaslahi ya wafanyakazi badala ya viongozi kujinufaisha wenyewe??? taza ma posho ya mbunge ya siku moja ni zaidi ya mshahara wa mwezi wa mfanyakazi!!!! jamani hii si dharau??? ni pesa kiasi gani zinatumika na mkuu anapofanya ziara nje ya nchi akiwa na msululu wa watu kibao? kwa nini idadi ya wapambe wa rais isipunguzwe na safari zikapunguzwa ili hako ka keki ka taifa kaongezwe ka huyu mlala hoi anayelipwa sh.100,000 kwa mwezi??? jamani ubinadamu upo hapo? TUCTA kaza buti na safari hii lazima muwe serious maana haki ya mtu haipewi bure bali inadaiwa na mgomo ndo njia mwafaka ya kudai haki. Msitishwe na yeyote yule, ati mgomo ni batili!!!! wakati umefuata taratibu zote ikiwepo kutoa notisi na kutangaza mgogoro na serikali. Hayo mazungumzo kama kweli yapo yafanyike haraka huku mipango ya migomo ikiendelea kama kawaida kama mazungumzo hayo hayatafikia mwafaka. wafanyakazi tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha..... tunahitaji haki yetu
ReplyDeletesafi sana.,maana huo mgomo ulikuwa umekaa kisiasa zaidi.serikali ya awamu ya nne imekaa miaka 4 madarakani imeshaongeza mishahara mara mbili,wakati awamu ya tatu imekaa madarakani miaka 10 imeongeza mshahara mara moja,tatizo la watanzania ni ukiwa unawasikiliza na kuwabembeleza na wanaona kama ni weakness.namshauri JK aanze ubabe wa mkapa,washike adabu.wakigoma wfukuzwe wote kama mkapa alivyofanya muhimbili.
ReplyDeleteKwanza hao ATE sasa hivi wanawanachama wangapi? Wengi wa waajiri wanaowatumia ni wale wenye kutaka maslahi fulani ya kifisadi serikalini na kwa ILO! ATE wenyewe wamefulia hawana mbele wala nyuma nenda kwenye mkutano wao mkuu wa mwaka utaliona hili! ATE ilikufa pale Maenda alipoondoka! Huyu Dr Mulimuka aende akafundishe sheria chuo kikuu hapa si mahali pake
ReplyDeleteKwanza waajiri wote Tanzania ni makuwadi wa ufisadi
ReplyDeleteRais JK anajua kabisa Prof. Kapuya amekalia bomu la kutegwa na sasa anajaribu kumsaidia kwani ni mtu wake wa karibu, halafu Waziri unapata wapi ujasiri wa kwenda mpirani wakati wizarani kwako kuna jambo zito kama hili. Prof. Kapuya anajua sana mpira na Muziki wanaomjua wanalijua hili. TUCTA wanataka shingo ya Kapuya ili JK abaki salama lakini akiendelea kumbeba hawezi kukwepa lawama zitakazotokana na mgomo huu. Jambo la pili Dr. Mlimuka asisahau kuwa yeye aliondoka UDSM kujiunga ATE alifuata nini, bila shaka ana malengo yake kwa haraka utajua bila shaka ni maslahi mazuri, leo anaona wafanyakazi kudai maslahi mazuri haina mantiki??????
ReplyDeleteMsemakweli amenichefua sana! eti tufanye tathmini sijui nini...utafiti! wa tulicho zalisha eti ndio tudai nyongeza....
ReplyDeleteutazalisha nini wakati unalipwa laki moja kwa mwezi na una mke na watoto
Hivi amejiuliza jaji mkuu, gavana wa BOT wamezalisha nini hadi kupewa shs bilioni1.3 kukarabati nyumba?!
Then eti wenzenu ulaya.....tutagoma kibongobongo..... kama ni kuiga Ulaya kwanini waajiri wasiige Ulaya wanavyolipa wafanyakazi!! yaani kwenye kuumia ndio tuangalie referensi za ulaya?? akili au matope haya?
Jitu zima hata halijui linachoongea! Leo hii ndo unajifanya unaijua sheria!
ReplyDeleteMigomo hata katika nchi zilizoendelea ipo na kwa taaarifa yako ndio njia peekee inayoleta mafanikio katika kupigania maslahi ya mfanyakazi!
Five yrs serikali unayoipigia debe imefanya nini? Hata mkakati tu! Wamekurupushwa ndo wanaanza kusema ooh tutaongeza mishahara!!!
Acha tugome!!
Msemakweli, hivi umefanya utafiti kujua kima cha chini cha mshahara kwa Tanzania ni kiasi gani na pesa wanayopata wabunge kila siku wakiwa kwenye vikao?
ReplyDeletePoland ikiwa chini ya Waleca, kama si chama cha Wafanyakazi na migomo, hadi leo ukoministi ungelikuwepo. Wanaiba na kujilipa mishahara mikubwa. Kila siku safari na kwao pesa zipo ila kwa wengine pesa hakuna. Huu mgomo ni zaidi ya mishahara. Kama Ulaya na wao wanagoma, usitudanganye hapa. Juzi tu British Airways wamegoma na kuleta usumbufu mkubwa. Wafanyakazi ni watu pekee wataoibadili Tanzania na kuwalazimisha viongozi wetu kuwa wanafanyakazi za ziada. Haya ya kumuona Kaka Kapuya anasakata rumba Acudo na sijui kwenda kuangalia mpira, unaona kabisa huu mgomo wao hata hauwashtushi. Wangelikuwa wanafikiri walao kama wewe, basi tusingelifikia huko. TUCTA kazeni buti kwa maslahi ya Watoto wetu. Ukitokea mgomo wa kwanza, mingine itakuwa rahisi. Huyo kaka Mlimuka, naona njaa tu inaumiza. Mdau Sizya.
Duh...we jamaa ivi umetumwa...??
ReplyDeletembona siku zote huwa huonekani...au ndo unatafuta ubunge na wewe kupitia migomo ya wafanyakazi...au umeahidiwa U-DC baada ya uchaguzi?....nina uhakika hujui una/lichokiongea
hata msipotulipa siku zote za mgomo poa, mgomo uko palepale na uache mkwara mbuzi. kama noma na iwe noma, tumechoka.
ReplyDelete