RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa baadhi ya Wakuu wa Wilaya nchini kwa kuwahamisha na kuwapangia vituo vipya kama ifuatavyo:-
Taarifa ya uteuzi huo iliyosainiwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bw. Aggrey Mwanri imesema pamoja na mabadiliko hayo, Rais Kikwete pia amemteua Bibi Husna Mwilima aliekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Wanawake kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba kuchukua nafasi ya Ndugu Francis Miti ambaye anahamia wilaya ya Ulanga.
Aidha, Rais Kikwete ametengua uteuzi wa Bw. Thobias M. Sijabaje ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kutokana na kutosimamia vizuri zoezi la ugawaji wa vocha za pembejeo za kilimo katika wilaya ya Sumbawanga katika msimu wa mwaka 2009/2010.
Mabadiliko haya yanakusudia kuongeza ufanisi wa kazi, kuimarisha utendaji katika wilaya hizo na yanaanza mara moja.
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S. L. P. 3021
DAR ES SALAAM
Jumanne, Aprili 06, 2010.
1. Gishuli M. Mbegesi - Njombe amepangiwa kwenda Kilindi
2. Leonidas T. Gama - Mbeya amepangiwa kwenda Ilala
3. Frank A. Uhaula - Tarime ameoangiwa kwenda Kiteto
4. Bi. Sarah Dumba - Kilindi amepangiwa kwenda Njombe
5. John B. Henjewele - Kiteto amepangiwa kwenda Tarime
6. Rashid M. Ndaile - Chunya amepangiwa kwenda Mkinga
7. Evans Balama - Ilala amepangiwa kwenda Mbeya
8.Florence A. Horombe -Bukombe amepangiwa kwenda Nzega
9. Bi. Zainab Kwikwega -Kasulu amepangiwa kwenda Makete
10. Bi. Hawa Ngh’umbi -Makete amepangiwa kwenda Bukombe
11. Lt. Col. John Mzurikwao -Mpanda amepangiwa kwenda Sumbawanga
12. Bi Betty Machangu -Nzega amepangiwa kwenda Kasulu
13. Dk. Rajab Lutengwe -Ulanga amepangiwa kwenda Mpanda
14. Francis Miti -Tandahimba amepangiwa kwenda Ulanga
15. Deodatus Kinawiro -Mkinga amepangiwa kwenda Chunya

PONGEZI RAISI KWA BIDII ZAKO ZA KUTAKA KUONGEZA UFANISI KTK UTENDAJI WA MAENDELEO KWA KASI VILE ANAVYODHANI IWE HAIWI. LAKINI KTK KUHAMISHA HAMISHA HUKU GHARAMA ZA UHAMISHO NI KUBWA MNO AMBAZO PESA HIZO ZINGEFAA MAMBO MUHIMU SANA MAANA SI MUDA MREFU UMEFANYA MABADILIKO YA HAOX2 WAKUU WA WILAYA NI AFADHALI KAMA MTU AMEBORONGA AMTEMA AMTEUE MWINGINE KULIKO KUHAMISHA WA HUKU KUMPELEKA HUKU HATA HUKO AENDAKO ATAVURUNDA TU. MFANO ILALA AU DAR KWA MUDA WAKE AMESHABADILISHA ZAIDI YA MARA 3 KAMA SI 4. TUNAZIHITAJI HIZO PESA KWA MATIBABU, KUONGEZA WADI ZA WAGONJWA VITANDA NK, NENDA AMANA, MWANANYAMALA AU MUHIMBILI WAGONJWA WAPO MPAKA KTK KORIDO NI HATARI TUWE WAANGALIFU MZEE KIKWETE
ReplyDeletehope to hear next time pr. jk is going to reshuffle his advising commettee
ReplyDeleteHakikisha Kumbukumbu zako ndugu Anon Apr 06, 02:04:00 PM. Wakati anaingia kwenye uongozi wilaya ya Ilala alimhamisha Capt Mpembenwe akamleta Patrick Tsere. Baada ya miaka 3 Tsere akaondolewa akaletwa Balama. Sasa Balama kaondolewa. Je hiyo ni mara ngapi tangua awe Rais? Si mara mbili. Hiyo mara 4 ni ipi?
ReplyDeleteNampongeza Rais kumteua Hasna kuwa DC. Inaashiria kuwa huko UWT wale waliofikiria wamemmaliza sasa wameumbuka. Waende sasa Tandahimba wakasemeseme tena. Hii pia inaonyesha Rais kama Mwenyekiti wa Taifa anamtambua dada Hasna.
KWANINI USIWAHACHISHE KAZI? BADALA YA KUWAHAMISHA! YALEYALE YA MIAKAYA 1970-1980`S MUNGU TUSAHIDIE WAAFRIKA SISI.
ReplyDeleteAnkal, unajua dada Husna Mwilima alikuwa anachukiwa sana na mwenyekiti wake wa UWT na wapambe wake wenye mtindio, hadi wakamtemesha kibarua chake pale UWT. Lakini Mungu ni wa kila mtu, naona Mkuu wa nchi kamwona dada wa watu na kumpa ukuu wa wilaya.
ReplyDeleteBora akawe mkuu wa wilaya, nadhani ataepuka siasa za chuki za akina SS na wenzake. Mungu ampe ujasiri wa kukabili maovu na waovu!
safi sana rais,na polisi wangefanyiwa hivyo pamoja na walimu,wafanyakazi wa serikali hawatakiwi kkuzoea sehemu moja,maana mtu anazoeana na wenyeji mpaka anakuwa hafanyi kazi.kuna kpindi pale arusha,mkuu wa mkoa ,mkuu wa polisi na mkuu wa wilaya walikaa muda mrefu hadi wakawa wanatembea pamoja weekend kwenye mabaa.
ReplyDeleteDaah! Nimekosa ulaji tena!
ReplyDeleteuharibifu wa pesa tuu na hakuna sababu yeytote ya maana kuhamisha hawa DCs wengi kiasi hiki kwa wakati mmoja,hapo unaweza kukuta gharama za kuhama kwa kila mmoja zinazidi milioni 10...ndugu wananchi hapa tunaongelea mamia ya mamilioni kwa huu uhamisho usio na faida yeyote,kama wameshindwa kazi waondoe,sijui kuhamisha inasaidia nini?Raisi punguza siasa na kumbuka upo hapo kwa muda tuu,fanya kazi kusaidia wananchi wako historia itakukumbuka na utastaafu vizuri sana na utakuwa na maisha ya amani na raha kila ukikumbuka jinsi ulivyosaidia watu wako,wape wachapa kazi sio wa kukusaidia kampeni.
ReplyDeleteReforms zinatakiwa ofisi za Ma DC zihuishwe na Halmashauri za wilaya / miji/ manispaa / jiji.
ReplyDeleteNa hawa wanatakiwa waombe kazi na kuajiriwa kwa sifa zao. Tubaki na Ma- RC waendelee kuwa wateule.
Sababu:
1. matumizi makubwa yasiyo ya lazima
2. kuingiliana kimadaraka, kuiongeza mkanganyiko na hata kukosa ufanisi kati ya ofisi hizi na za Halmashauri.
3. Ofisi zote hizo zipo kusukuma maelendeleo ya Wilayani kwa nini zitofautishwe?
karibu mbeya balama...tunakuaminia wewe ni mchapa kazi hodari hongera jk kwa kutufanyia haya mabadiliko..
ReplyDeleteKule Tandahimba DC aliyekuwepo anaitwa Fatma Salum Ally, je amepelekwa wapi? Au alishapigwa chini muda mrefu? Tafadhali nisaidieni niweke sawa kumbukumbu zangu.
ReplyDelete