kumbe katika msikiti huo kuna timu maalum ya ulinzi amabayo inafanya kazi zake kwa umakini mkubwa na wanajua kabisa nani kaja na nini kwa hiyo ni rahisi sana kwa kuona kama kila aliyeingia na kiatu anatoka nacho na si vinginevyo.
sasa huyu kijana akiwa mgeni maeneo hayo alokwenda kufanya wizi huo alipojitahidi kujifanya kama vile anaelewa taratibu za hapo ilikuwa hali mbaya sana kwake. na kama si askari wa kulinda anmani mitaani hali ya kijana huyo sijui ingekuwaje. Habari na picha na emmanuelly Mgongo wa Globu ya Jamii
me nilitegemea mahali kama msikitini ndio watu wana hofu na Mungu. Nimesikitishwa na kipigo walichompa huyu ndugu kwa kosa dogo kama hili?..hv kweli huyo Mungu mnaekwenda kumuomba anapenda kutoa adhabu za kikatili kama hizi?mbona mmekosa roho ya huruma kwa huyo ndugu kiasi hiki?kwani mngemkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya dola asingepewa adhabu inayostahili?kweli mtu unaenda kumwomba Mungu then hapo hapo unakuwa na roho ya kutaka kumuua ndugu yako kwa kosa dogo kama hili?ni Mungu wa kweli huyu mnaekwenda kumuomba au?.mh kweli ndo maana hata kujitoa Mhanga kwa mabomu ya kujilipua kwa kisingizio cha kwenda peponi inawezekana..!!!
ReplyDeleteubianadamu upo wapi hapa? ndala tuu jamani mnatak kutoa uhai wa mtu?
ReplyDeletewewe hapo wanne acha kuongea upuuzi mungu gani maana yake nini usijaribu kuhusisha kuipigwa kwa huyu mtu na dini acha kabisa usijaribu kuongea hivyo jaribuni kupeleka makanisa yenu mikoani kama musoma mpaka watoto wamechinjwa vichwa sababu ya ng'ombe kama na nyinyi mnamungu wa kweli acha kuonge upuuzi
ReplyDeleteAmekosea mlango ageenda kuiba kwa wakristo kwan wale wana roho za ki tjiri madai yao eti..sisi wakristu atu mukumu mtu kwa kosa kama ilo. lol
ReplyDeleteWe anony wa 05:56pm Naona umeamua kutumia jukwaa la Blog ya Jamii kukashifu dini. Ni kweli Kupiga mtu kwa nana hii ni makoso tena si madogo. Lakini hakuna maahala kwenye dini ya kiislaam kunakofundisha upuuzi huu wa kujilipua. Usifuate unayo yaona kwenye Tv wewe.
ReplyDeleteMbona Mapadri wana lawiti watoto wadogo kwa miaka nenda rudi, lakini hatusemi Dini zao zina wafundisha kufanya hivyo.
Matatizo yako kwa wanaodai kufuata dini na sio dini.
SOMA HISTORY NA DINI UPATE KUJUA NINI KINAENDELEA.
anoiba kanda mbili anapigwa kipigo kikali namna hii. wanaoiba mamilioni na kuwafanya wanyonge kama huyu kuiba ili kujaza tumbo tunawalinda na kuwatunza.
ReplyDeletehuyu jamaa hakupigwa msikitini na wala na waliomsikitini. jamaa alikimbia alipogundulikana na matokeo yake watu wa mitaani walimfukuza na kumpa kipigo kikatifu.
ReplyDeletevibaya watu kuchukua sheria mkononi. Sasa upande mwingine huyo jamaa ina maana hizo kandambili zilizokwishavaliwa anakwenda kuziuza wapi? ama ni za kuvaa njaa imekuwa kali.
ReplyDeleteMungu ana kosa gani hapa?
ReplyDeletemi naona hawakufata Mungu asemavyo bali mila za kitanzania za kila siku ambazo watu wa dini zote wanahusika: kujichukulia sheria mkonono.
mASIKINI mALILO AMEFIKIA KUWA KIBAKA KIASI HICHO? KWELI KUISHI KWINGI KUONA MENGI
ReplyDeletekuanzia nilipokuwa naishi bongo sijawahi hata siku moja ku support kupiga wezi, kwanza nikinyume cha sheria we raia kuchukuwa atuawa mkononi,na tukija kibinadamu ni nani msafi wa kumuhukumu mwenzake bila kufuata misingi ya nchi, hili nadhani linasababishwa na ukosefu wa kazi wa watu wengi,,,, PERIOD!
ReplyDeleteUkosefu wa akili huu,kwanini utake kumuua mtu kwa kosa kama hili la ndala?hao waumini kwani walishindwa kumuokoa jamaa mpaka askari wafike? sasa mnasali nini kama mnaweza kuacha mtu afe kwa ajiri ya kuiba ndala na wala hakuna uhakika kama ni kweli...inawezekana kusingiziwa tu au alikosea,nimewahi kushuhudia mtu kariakoo kaitiwa mwizi wakati sio mwizi na bahati nzuri kuna wanaume ngangari walisimama kumtetea maana alikuwa anakwisha,tafadhari acheni hizi tabia wananchi la sivyo kuna siku yatawakuta nyie au ndugu/familia/watoto wenu na marafiki zenu sijui mtasemaje?ACHENI huu unyama watu wafikishwe mbele ya sheria
ReplyDeleteAnony wa Tue 05:56:00 PM usianze kuhusisha hicho kipigo na maswala ya mabomu.hilo jambo la kupigwa mwizi si geni hapa bongo na linafanywa na wananchi wenye kuamini dini mbali mbali.Nitajie mtu mmoja tu alietoa kipigo kwa mwizi hapa Tanzania akawa ameenda kujitoa muhanga. Totally unrelated!!
ReplyDeleteMDAU HAPO JUU NAONA UMEFIKA MBALI NA NI WAZI KUWA UMEKUSUDIA KUTUKANA IMANI ZA WATU. JE UNATAKA KUSEMA KUWA YEYE YUKO SAHIHI NA TENDO LAKE! AU KWAKUWA SI PAHALA UFANYIAPO IBADA WEWE.
ReplyDeletePole Ndungu, kandambili ndiyo inafanya mtu apigwe hivi? wakati wa wezi wa EPA wana kura starehe. Kweli Africa kazi.Once again Pole.
ReplyDeleteInasikitisha. Yaani kanda mbili tu ndio mtu apigwe hivi? Hizo kandambili zina gold ama? Halafu mnasema Tanzania tunajivunia amani. Amani yenyewe iko wapi. Hamna cha amani yeyote iwapo watu wanapigwa mitaani na serikali wala haisemi kitu au kuchukulia hatua watu wanaofanya hivi. Hapo watu wamejifanya mapolice na mahakimu hapo hapo. Yaani kama mioyo yenu imetakata kweli mngempa na chakula cha mchana. Mtu anayeenda that law kuiba malapa ujue amefika chini kabisa. Anahitaji msaada.
ReplyDeleteNdio mnasema bongo tambarare...this is too much....
JAMANI WAUMINI ACHENI UKATILI NA UNYAMA HUO YAANI KANDAMBILI AMBAZO GHARAMA YAKE HAIFIKI HATA $ 1 NDIO MNATAKA KUMTOA MTU ROHO TENA AMEKUJA MSIKITINI MNATAKIWA KUMUOMBEA JAMANI SIMUUNGI MKONO KWA WIZI ILA PIA SIUNGI MKONO WAUMINI NEVER HUO SIO UPENDO WALA HAKI BASI NI HERI KAMA MNA TIMU YA WALINZI MNGEMKAMATA NA KUMPELEKA KATIKA VYOMBO VYA DOLA POLISI KISHA MAHAKAMANI NA BAADAYE MAGEREZA,ni mimi mzalendo
ReplyDeleteMUNGU alipomwambia MUSA kuwa vua viatu vyako hapa ni mahali patakatifu alitaka MUSA atubu dhambi zake kwani viatu vina kosa gani kwa MUNGU?
ReplyDeleteinasikitisha kuona kitendo hiki cha kumpiga mtu nusura kumtoa roho kinafanywa na waumini tena katika nyumba ya ibada kwani mnasema msikiti tayari uliweka ulinzi maalumu sasa kwanini mfanye unyama huo
ReplyDeleteNatamani kipigo hichi angepewa mmoja wa mafisadi wa EPA, Richmond au Kiwira.
ReplyDeleteJE YULE KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 23 MNIGERIA ALIYEBEBA MABOMU KWENYE CHUPI ALIFUNDISHWA NA NANI?
ReplyDeleteninyi wote mlioshiriki kumpiga huyo kijana mna roho sawa na wale wanawake waliojitoa muhanga kule urusi na kuua watu
ReplyDeletewewe mtoa maoni unayepinga kuwa kujitoa muhanga eti sio mafundisho ya dini ni kuwa huijui hiyo dini vizuri ok kaa kimya
ReplyDeletejamani vibaka msiwe mnakwenda kuiba huko kama mtu anabeba bomu kujiua yeye je atakuacha wewe?
ReplyDeleteKipondo kama hiki wangekuwa wanapewa wale wezi wa pesa za umma ingeleta maana. Bongo ukiiba ndala wanakuua, ukiiba mamilioni unasifiwa eti mjanja.
ReplyDeleteAsilimia kubwa naona mnamtetea huyo mwizi.Siku ukiibiwa ndio utajua kuwa ndala ni kubwa au ndogo.kuna watu hata pesa ya kununua ndala kwao ni shida!Huyu anaiba leo ndala kesho anakuibia simu nk!Ukimpeleka polisi hujafika mbali kashaachiwa hasara umeingia,vyombo vya dola haviko pia makini ndo maana "wananchi wenye hasira wanona wamalizane tu kiaina"hata kwa namna hii!
ReplyDeleteMwizi ukimpeleka polisi hana alama wanakugeuzia kibao!kalagabao
Asilimia kubwa naona mnamtetea huyo mwizi.Siku ukiibiwa ndio utajua kuwa ndala ni kubwa au ndogo.kuna watu hata pesa ya kununua ndala kwao ni shida!Huyu anaiba leo ndala kesho anakuibia simu nk!Ukimpeleka polisi hujafika mbali kashaachiwa hasara umeingia,vyombo vya dola haviko pia makini ndo maana "wananchi wenye hasira wanona wamalizane tu kiaina"hata kwa namna hii!
ReplyDeleteMwizi ukimpeleka polisi hana alama wanakugeuzia kibao!kalagabao
kwa annon Wed Apr 07, 04:53:00 AM tafadhali fuata ushauri wako mwenyewe, naam kaa kimya.
ReplyDeleteinfact endelea na kufata danganya danganya za vibarazani.
Anony 5.56 p.m. kwa taarifa yako wanaojitoa mhanga wengi wao ni visasi vya uonevu. Na huyu jamaa alipokuwa anaiba,waumini walikuwa ndani wanaswali, wala hawakujua kinachoendelea nje. Alipigwa na watu waliokua nje baada ya askari kumstukia. Umeelewa wewe?
ReplyDeleteSHIDA NA BANGI MBAYA SANA! SASA NDALA USED ANGEUSA SH NGAPI? KAMA SIO MIA MBILI? DUH TUNAFIKIA HATUA MBAYA SANA...
ReplyDeleteWed Apr 07, 04:38:00 AM,Wed Apr 07, 04:53:00 AM
ReplyDeletenyie maanon wawili yani nimecheka kama kichaa ama kweli mnatafuta watu!!me simo
hahahahaaaaaaaaaaaa