Home
Unlabelled
kanali ali mahfoudh
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Marehemu Ali MAhafoudh ni mmoja wa wanajeshi wetu wakakamavu waliopata mafunzo ya pamoja na marehemu Idd Amin Dada, kama sikosei na kiongozi wa libya wa hivi sasa, Muamar Gadaf
ReplyDeleteBingo! Huyu Kanali yupo wapi siku hizi? Sikujua kama Nyerere alikuwa ameenda eji kiasi hicho wakati ule, anyway, 69 was a good year, let the bygones be bygones and so on and so on....RIP mchonga, we still love you big time!
ReplyDeleteHuyu Komando pamoja na Babu walikuwa awkimnyima usingizi rais wa Zanzibar.
ReplyDelete(US Blogger)
Jamani huyu si ndiye aliyetaka kumpindua Nyerere au sio? Anayejua naomba anisaidie ndugu zanguni.
ReplyDeleteHuyo jamaa namkumbuka sana zamani wakati ule mimi bado mdogo sana ila kumbukumbu ninazo..alikuwa anakuja nyumbani,alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa mzee wangu(baba)nakumbuka wakti ule alikuja nyumbani akitokea msumbiji,nakumbuka kuna siku alikuja nyumbani akatupikia msosi kijeshijeshi,ilikuwa ugali(njano)-maharagwe si unajua tena enzi zileeeeeee za baba wa taifa(noma)...anyway ana ndugu yake ambaye ni Doctor yupo Muhimbili ni Gynocologist anaitwa Dk Hamid Mahafudh ambaye pia ni rafiki mkubwa wa mzee...duh enzi zileee!
ReplyDeletemdau- mushty@hotmail.com
MZEE POLISI NI MAREHEMU CHIEF ROBERT SHIJA KASWENDE ALISHAKUWA MKURUGENZI WA JKT ENZI HIZO MKUU WA JKT WANATUMIA JINA LA MKURUGENZI BAADAYE ALIRUDI POLISI NA ALISTAAFU MIAKA YA 1975 AKIWA KAMISHINA WA POLISI WENYE DATA ZAIDI WANISAHIHISHE KAMA NIMEKOSEA
ReplyDeletekatika moja ya hasara zetu tanzania huyu bwana alitiwa ndani sina hakika sababu yake ilikuwa nini marehemu samora machel akamuombea sana aachiliwe na kama tanzania haimtaki yeye yuko tayari kumchukua msumbiji kwani katika vita vya kugombea uhuru wa msumbiji huyu bwana alifanya kazi kubwa sana,
ReplyDeletebaadae akaachiliwa akaenda kuwa mshauri wa rais mambo ya kijeshi chini ya uongozi wa samora machel baada ya samora kufariki akabaki msumbiji akawa mfanyabiashara mara ya mwisho kumuona ilikuwa 1988 baada ya hapo sijamuona tena nikaja kusikia amefariki
Mahfoudh inasemekana was Cuban trained. Alikuwa jasiri na mwerevu katika kuandaa mikakati ya vita. Wakati FRELIMO inapambana na Wareno, Mahfoudh alikuwa Nachingwea akiongoza mapambano. Wareno walimuogopa sana kwa sababu walisikia ukali wake. Mahfoudh alikuwa mzuri wa sura lakini katili sana anapomkamata adui. Kuna masimulizi kuwa alikuwa akiwakamata askari wa Kireno alikuwa anawaweka ndani ya pipa linalochemka mafuta ya kupikia halafu huwafanyia interogation.
ReplyDeleteBaada ya Mozambique kupata uhuru serikali ya huko ilimchukua kama mshauri wa kijeshi.
Hayo ndiyo baadhi ya mambo niliyowahi kuyasikia juu yake.
kanali mahfoudh aliogopwa sana na Karume kiasi akamuondoa zenji na kumleta ktk serikali ya jamhuri na huku nako akawa anapendwa sana na wanajeshi na kuepo uvumi kwamba kauli yake ilisikilizwa sana kuliko hata mkuu wa majeshi na rais pia,ndio akapelekwa msumbiji kwa kumhofia yy....kuna ndugu yake mmoja alisema ktk nyumba ake huko msumbiji kajaza bunduki za aina zt kuanzia kuta za ukumbini hadi chooni,sasa ole wako umkere
ReplyDeleteLATE CHIEF ROBERT KASWENDE NI KAKA YA BIBI YANGU. KIFUPI BABU YANGU ALISTAAFU AKIWA ASISTANT POLICE CHIEF TANZANIA. BAADAYE AKAWA WAZEE WA BARAZA WA MAHAKAMA KUU TANZANIA WANAKWENDA KWENYE KESI ZOTE AROUND TANZANIA. MZEE POA SANA NAMKUMBUKA SANA. KAMA WEWE NI NDUGU TUNAWEZA KUWASILIANA PRIVATE. LAKINI SIKU HIZI KUNA KASWENDE MWINGINE (MJOMBA) AMBAYE NI MKUU WA SHERIA POLICE TANZANIA HUYU ANAWEZA KUKUFAHAMISHA MENGI KUHUSU BABA YAKE MDOGO LATE R. KASWENDE.RIP AMEZIKWA LOHUMBO ITWANGI SHINYANGA KWAO.
ReplyDeleteMWAKA 1985 NILIKUWA MAPUTO NA NIPOKWENDA KUJIANDIKSHA KATIKA UBALOZI WETU NIKAAMBIWA KUNA CLUB YA WATANZANIA NDANI YA JENGO LETU LA UBALOZI TULIO PEWA NA SAMORA SIKUMBUKI NI GORFA YA NGAPI JIONI NILIPO KWENDA NILIPATA BAHATI YA KUKUTANA NA KANALI MAHAFUDHI MAREHEMU ALIKUWA MTU WA WATU,MKARIMU NA MUUNGWANA BILI KUBAGUA WATU WA RIKA LOTE NIMEFIKA KWAKE WATANZANIA WENGI WALIKUWA WANAENDA KUMTEMBELEA,HUYU BWANA NI KATI YA WANA MAPINDUZI WA KWELI WA AFRIKA CHE GUEVARA KABLA YA KWENDA KONGO ALIKWENDA ZANZIBAR NA ALIKUA NAE BEGA KWA BEGA,ZIA UL HAG NI KATI YA WATU ALIOPATA NAO MAFUNZO NA SIO IDI AMINI.MCHANGO WAKE WA MWISHO KA NI VITA VYA UKOMBOZI WA ZIMBABWE,NAMIBIA,NA SAUTHA AFRICA(ANC),NA ALIKUWA NI KIPENZI CHA BABA WA TAIFA,SERIKALI NA ZANI INASITA KUMUWEKA KWENYE HISTORIA YA MASHUJAA KUTOKANA NA KESI YA KUHUSISHWA NA KESI YA KARUMU UPUMZIKE KWA AMANI KOMANDOO WA KWELI MWA MAPINDUZI WA AFRICA CANAL MAHAFUZI.
ReplyDeletemdau wa Sat May 01, 08:19:00 AM umesemak kweli.
ReplyDeleteNingelipenda kueleza historia yake yote na siri ya huyu jamaa kupelekwa msumbiji lakin nahofia michuzi ataogopa kuiweka hapa.
anyway kupelekwa huyu jamaa msumbiji ilikuwa ni kwa sharti hatorudi tanzania na pia hatomsumbua au kumtia kiherehere nyerere.
Mahfudh hakuwa ni katika wale ambao walipanga kumuangusha Nyerere miaka ya 80?Ulikuwa ukifanyika mkutano pale Kinondoni Mkwajuni!Michuzi hebu tuletee kumbukumbu za kina Uncle Thom kina Zna na wengine.Komandoo Mahfudh alikuwa kiboko ila mambo fulani yakamfanya Mwalimu amuondoe!!Drain in drain out??!!
ReplyDeleteMwalimu, Karume, Kambona, Kawawa,Kasella bantu, Bibi Titi wote ni marehemu sasa.
ReplyDeleteTunaweza kuongea ukweli kuhusu jaribio la kumpindua Mwalimu. Na wale walionyongwa na Mwalimu wakumbukwe!
Kanali Ali Mahfoudh alipata mafunzo ya ukamandoo mwaka 1963 nchini Cuba. Alikuwa karibu sana na Fidel Castro na Che Guevara. Usiku wa kuamkia 12 Januari 1964, John Okello na kina Khamis Darwesh na Sefu Bakari walivamia vituo vya polisi vya Ziwani na Mtoni na kuanza mapinduzi ya Zanzibar. (wakati hou ZBR hakukuwa na jeshi). Saa 4 asubuhi, makada wa Umma Party (cha A. Babu) waliosoma Cuba, walijiunga na kina Okello na kuishambulia Malindi polisi station. Mapigano yalidumu siku nzima. Hatimaye, Malindi pia ilichukuliwa na wanamapinduzi. Kina Kanali Mahfoudh walijiunga na jeshi jipya la TPDF liliondwa 1964 baada ya uasi wa wanajeshi wa Tanganyika 20/1/1964 Colito baracks (siku hizi Lugalo). Mahfudh alipata umaarufu 1964-1972 katika kuwasaidia FRELIMO, ZANU, ZAPU na MPLA na katika mission moja dhidi ya kibaraka Kamuzu Banda. 1972-1978 alikuwa kizuizini TZ bara kwa tuhuma za kutaka kumpindua Karume. Mwalimu Nyerere aligoma kata kata kumrudisha ZBR. Comrade Samora alimwomba aende Msumbiji ambako aliisaidia serikali ya Mozambique kupigana na magaidi ya RENAMO mpaka RENAMO ikashindwa. Makaburu ya South Afrika yalijaribu mara tatu kumuua lakini yalishindwa. Alistaafu huko Mozambique ambako aliishi hadi mauti ilipomkuta kutokana na kisukari. Tunamwomba Mola amlaze pema. Amin. Mzalendo7.
ReplyDeleteGrand pa
ReplyDelete