Mwalimu akimvisha medali Kanali Ali mahfoudh mwaka 1969. Mwanajeshi huyu ni mmoja wa askari waliopata umaarufu sana katika JWTZ kwa utumishi wao. Wengi wamesikia jina lake, lakini wachache wamepata kumuona kwa sura. wenye data zaidi msaada tutani tafadhali....


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2010

    Marehemu Ali MAhafoudh ni mmoja wa wanajeshi wetu wakakamavu waliopata mafunzo ya pamoja na marehemu Idd Amin Dada, kama sikosei na kiongozi wa libya wa hivi sasa, Muamar Gadaf

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2010

    Bingo! Huyu Kanali yupo wapi siku hizi? Sikujua kama Nyerere alikuwa ameenda eji kiasi hicho wakati ule, anyway, 69 was a good year, let the bygones be bygones and so on and so on....RIP mchonga, we still love you big time!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2010

    Huyu Komando pamoja na Babu walikuwa awkimnyima usingizi rais wa Zanzibar.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2010

    Jamani huyu si ndiye aliyetaka kumpindua Nyerere au sio? Anayejua naomba anisaidie ndugu zanguni.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2010

    Huyo jamaa namkumbuka sana zamani wakati ule mimi bado mdogo sana ila kumbukumbu ninazo..alikuwa anakuja nyumbani,alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa mzee wangu(baba)nakumbuka wakti ule alikuja nyumbani akitokea msumbiji,nakumbuka kuna siku alikuja nyumbani akatupikia msosi kijeshijeshi,ilikuwa ugali(njano)-maharagwe si unajua tena enzi zileeeeeee za baba wa taifa(noma)...anyway ana ndugu yake ambaye ni Doctor yupo Muhimbili ni Gynocologist anaitwa Dk Hamid Mahafudh ambaye pia ni rafiki mkubwa wa mzee...duh enzi zileee!
    mdau- mushty@hotmail.com

    ReplyDelete
  6. MZEE POLISI NI MAREHEMU CHIEF ROBERT SHIJA KASWENDE ALISHAKUWA MKURUGENZI WA JKT ENZI HIZO MKUU WA JKT WANATUMIA JINA LA MKURUGENZI BAADAYE ALIRUDI POLISI NA ALISTAAFU MIAKA YA 1975 AKIWA KAMISHINA WA POLISI WENYE DATA ZAIDI WANISAHIHISHE KAMA NIMEKOSEA

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 01, 2010

    katika moja ya hasara zetu tanzania huyu bwana alitiwa ndani sina hakika sababu yake ilikuwa nini marehemu samora machel akamuombea sana aachiliwe na kama tanzania haimtaki yeye yuko tayari kumchukua msumbiji kwani katika vita vya kugombea uhuru wa msumbiji huyu bwana alifanya kazi kubwa sana,
    baadae akaachiliwa akaenda kuwa mshauri wa rais mambo ya kijeshi chini ya uongozi wa samora machel baada ya samora kufariki akabaki msumbiji akawa mfanyabiashara mara ya mwisho kumuona ilikuwa 1988 baada ya hapo sijamuona tena nikaja kusikia amefariki

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 01, 2010

    Mahfoudh inasemekana was Cuban trained. Alikuwa jasiri na mwerevu katika kuandaa mikakati ya vita. Wakati FRELIMO inapambana na Wareno, Mahfoudh alikuwa Nachingwea akiongoza mapambano. Wareno walimuogopa sana kwa sababu walisikia ukali wake. Mahfoudh alikuwa mzuri wa sura lakini katili sana anapomkamata adui. Kuna masimulizi kuwa alikuwa akiwakamata askari wa Kireno alikuwa anawaweka ndani ya pipa linalochemka mafuta ya kupikia halafu huwafanyia interogation.

    Baada ya Mozambique kupata uhuru serikali ya huko ilimchukua kama mshauri wa kijeshi.

    Hayo ndiyo baadhi ya mambo niliyowahi kuyasikia juu yake.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 01, 2010

    kanali mahfoudh aliogopwa sana na Karume kiasi akamuondoa zenji na kumleta ktk serikali ya jamhuri na huku nako akawa anapendwa sana na wanajeshi na kuepo uvumi kwamba kauli yake ilisikilizwa sana kuliko hata mkuu wa majeshi na rais pia,ndio akapelekwa msumbiji kwa kumhofia yy....kuna ndugu yake mmoja alisema ktk nyumba ake huko msumbiji kajaza bunduki za aina zt kuanzia kuta za ukumbini hadi chooni,sasa ole wako umkere

    ReplyDelete
  10. LATE CHIEF ROBERT KASWENDE NI KAKA YA BIBI YANGU. KIFUPI BABU YANGU ALISTAAFU AKIWA ASISTANT POLICE CHIEF TANZANIA. BAADAYE AKAWA WAZEE WA BARAZA WA MAHAKAMA KUU TANZANIA WANAKWENDA KWENYE KESI ZOTE AROUND TANZANIA. MZEE POA SANA NAMKUMBUKA SANA. KAMA WEWE NI NDUGU TUNAWEZA KUWASILIANA PRIVATE. LAKINI SIKU HIZI KUNA KASWENDE MWINGINE (MJOMBA) AMBAYE NI MKUU WA SHERIA POLICE TANZANIA HUYU ANAWEZA KUKUFAHAMISHA MENGI KUHUSU BABA YAKE MDOGO LATE R. KASWENDE.RIP AMEZIKWA LOHUMBO ITWANGI SHINYANGA KWAO.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 01, 2010

    MWAKA 1985 NILIKUWA MAPUTO NA NIPOKWENDA KUJIANDIKSHA KATIKA UBALOZI WETU NIKAAMBIWA KUNA CLUB YA WATANZANIA NDANI YA JENGO LETU LA UBALOZI TULIO PEWA NA SAMORA SIKUMBUKI NI GORFA YA NGAPI JIONI NILIPO KWENDA NILIPATA BAHATI YA KUKUTANA NA KANALI MAHAFUDHI MAREHEMU ALIKUWA MTU WA WATU,MKARIMU NA MUUNGWANA BILI KUBAGUA WATU WA RIKA LOTE NIMEFIKA KWAKE WATANZANIA WENGI WALIKUWA WANAENDA KUMTEMBELEA,HUYU BWANA NI KATI YA WANA MAPINDUZI WA KWELI WA AFRIKA CHE GUEVARA KABLA YA KWENDA KONGO ALIKWENDA ZANZIBAR NA ALIKUA NAE BEGA KWA BEGA,ZIA UL HAG NI KATI YA WATU ALIOPATA NAO MAFUNZO NA SIO IDI AMINI.MCHANGO WAKE WA MWISHO KA NI VITA VYA UKOMBOZI WA ZIMBABWE,NAMIBIA,NA SAUTHA AFRICA(ANC),NA ALIKUWA NI KIPENZI CHA BABA WA TAIFA,SERIKALI NA ZANI INASITA KUMUWEKA KWENYE HISTORIA YA MASHUJAA KUTOKANA NA KESI YA KUHUSISHWA NA KESI YA KARUMU UPUMZIKE KWA AMANI KOMANDOO WA KWELI MWA MAPINDUZI WA AFRICA CANAL MAHAFUZI.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 01, 2010

    mdau wa Sat May 01, 08:19:00 AM umesemak kweli.

    Ningelipenda kueleza historia yake yote na siri ya huyu jamaa kupelekwa msumbiji lakin nahofia michuzi ataogopa kuiweka hapa.

    anyway kupelekwa huyu jamaa msumbiji ilikuwa ni kwa sharti hatorudi tanzania na pia hatomsumbua au kumtia kiherehere nyerere.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 01, 2010

    Mahfudh hakuwa ni katika wale ambao walipanga kumuangusha Nyerere miaka ya 80?Ulikuwa ukifanyika mkutano pale Kinondoni Mkwajuni!Michuzi hebu tuletee kumbukumbu za kina Uncle Thom kina Zna na wengine.Komandoo Mahfudh alikuwa kiboko ila mambo fulani yakamfanya Mwalimu amuondoe!!Drain in drain out??!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 01, 2010

    Mwalimu, Karume, Kambona, Kawawa,Kasella bantu, Bibi Titi wote ni marehemu sasa.

    Tunaweza kuongea ukweli kuhusu jaribio la kumpindua Mwalimu. Na wale walionyongwa na Mwalimu wakumbukwe!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2010

    Kanali Ali Mahfoudh alipata mafunzo ya ukamandoo mwaka 1963 nchini Cuba. Alikuwa karibu sana na Fidel Castro na Che Guevara. Usiku wa kuamkia 12 Januari 1964, John Okello na kina Khamis Darwesh na Sefu Bakari walivamia vituo vya polisi vya Ziwani na Mtoni na kuanza mapinduzi ya Zanzibar. (wakati hou ZBR hakukuwa na jeshi). Saa 4 asubuhi, makada wa Umma Party (cha A. Babu) waliosoma Cuba, walijiunga na kina Okello na kuishambulia Malindi polisi station. Mapigano yalidumu siku nzima. Hatimaye, Malindi pia ilichukuliwa na wanamapinduzi. Kina Kanali Mahfoudh walijiunga na jeshi jipya la TPDF liliondwa 1964 baada ya uasi wa wanajeshi wa Tanganyika 20/1/1964 Colito baracks (siku hizi Lugalo). Mahfudh alipata umaarufu 1964-1972 katika kuwasaidia FRELIMO, ZANU, ZAPU na MPLA na katika mission moja dhidi ya kibaraka Kamuzu Banda. 1972-1978 alikuwa kizuizini TZ bara kwa tuhuma za kutaka kumpindua Karume. Mwalimu Nyerere aligoma kata kata kumrudisha ZBR. Comrade Samora alimwomba aende Msumbiji ambako aliisaidia serikali ya Mozambique kupigana na magaidi ya RENAMO mpaka RENAMO ikashindwa. Makaburu ya South Afrika yalijaribu mara tatu kumuua lakini yalishindwa. Alistaafu huko Mozambique ambako aliishi hadi mauti ilipomkuta kutokana na kisukari. Tunamwomba Mola amlaze pema. Amin. Mzalendo7.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 20, 2019

    Grand pa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...