CD Mpya ya singo ya Ngoma Afrika Band

Bendi maarufu ya mziki wa dansi "The Ngoma Africa Band" singo CD mpya iliyobeba jina la "Jakaya Kikwete 2010" CD hiyo inanyimbo mbili moja ni ya mtindo wa "Rumba" na ya pili ni ya "Dansi" Bendi hiyo yenye maskani yake nchini ujerumani, imeamua kutanguliza CD hii ya " JK 2010" kabla ya " Bongo Tambarale, na supu ya Mawe".

Nyimbo hizo ni utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka ras Makunja,akiimba kwa kushirikiana na mchawi wa magitaa (mult-talent) Christian Bakotessa aka Chris-B.

CD hiyo "Jakaya Kikwete 2010" inamajibu yote ambayo wadau na wananchi wangetaka kujua kwanini Ngoma Africa Band imeamua kuachia hewani nyimbo hizo mbili za JK 2010.

Bendi hiyo maarfu kwa majina kama "The Golden Voice of East Africa" aka FFU ambayo ni mashuhuri kwa kuwatia kiwewe washabiki na mdundo wao kila kona duniani redioni au katika matamasha.

CD na nyimbo hiyo ya "Jakaya Kikwete 2010" sio biashara ya kuuzwa madukani, bali ni kwa kusikiliza kwa mujibu wa Kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka ras Makunja aka kamanda wa FFU!

JK anakuwa Rais wa kwanza afrika mashariki kubeba CD yenye jina lake "Jakaya Kikwete 2010" CD yenye ujumbe muhimu kwa watanzania wote, wakati Bendi ya The Ngoma Africa Band imekuwa bendi ya kwanza kuwachia hewani CD hiyo yenye mziki wa moto wa kuotea mbali. Mdundo unaosindikiza ujumbe wa nyimbo hizo umelenga wasikilizaji na
wadau wa umri wa vizazi vyote.

Kwa nini? bendi ya Ngoma Africa imemwashia taa kijani "Jakaya Kikwete 2010" majibu yanapatikana CD hiyo "Jakaya Kikwete 2010". Mnakaribishwa wote! kuburudika na CD ambayo ni fahari ya watanzania!

CD "Jakaya Kikwete 2010" ni CD ambayo kila mtanzania na wafrika wote lazima tujivunie. habari za kupatikana kwake mtaletewa karibuni na Globu yenu ya jamii. Na kwa maelezo zaidi lete ujumbe
ngoma4u@googlemail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. naona vichaa wa ffu aka ze ngoma afrika wamekuja na suluisho JK 2010,hongereni kazi yenu inakubalika na wote

    ReplyDelete
  2. hi!te!te! wazee wa kukaanga mbuyu! Ngoma Africa band hii kazi yenu tumeikubali kuwa nyinyi hamtaki msalie katika kazi,big up

    ReplyDelete
  3. Siasa Siasa Siasa, watanzania hata kwenye kumbi za burudani tumekumbatia Wanasiasa. Siasa na Wanasiasa wametufanya tuwaabudu wao..sijui tumlaumu Nyerere,au tulaumu mfumo wa Chama kimoja tuliokuwa nao au tulaumu Ubovu wa Elimu yetu!!

    ReplyDelete
  4. Kazi nzuri but it is not fair kuirusha hewani sasa kwani hii ni kampeni ya waziwazi na muda wa kampeni bado. Itafaa sana wakati wa kampeni utapofika.

    ReplyDelete
  5. vijana wa kufanya fujo uone,ngoma africa band hii kazi yenu babu kubwa,kwa cd yenu hii naweza kuwataja kuwa nyini mko juu.
    endelezeni imaya yenu ya mziki

    ReplyDelete
  6. safi sana,kazi nzuri sana

    ReplyDelete
  7. safi sana,lakini jaribuni kudeal na copy right,maana hii ngoma inaweza kupigwa kila pande ya nchi na ccm,au kama mmeitoa zawadi kwa muheshimia ni vizuri,na kama ni biashara meneja wenu aongee vizuri na amos makala ili upewe dili la kupiga na TOT kwenye kampeni.

    ReplyDelete
  8. The power of money. Sounds like "pay me and I can do what you want!Kweli nchi ni ya wachache.

    ReplyDelete
  9. mwe!mwe!mwe!kibwana kichwa ngumu ketu ras makunja na nduguzo ffu,hii ni funga kazitupu,mie sisemi nawachia wasukutuaji

    ReplyDelete
  10. hii njaa ya kufanya vitu kwa sababu ya kunufaisha matumbo yenu hina umiza taifa. Unapo nunuliwa leo na kumchagua kiongozi asiye bora jua kwamba umeuza kizazi chako pia!!!!
    watanzania tuta change lini!!
    mungu hibariki tanzania

    ReplyDelete
  11. Ninyi "Ngoma ya Afrika" mmelipwa ngapi?

    ReplyDelete
  12. Ras Makunja na Ngoma Africa band do!salaleeeeee!!!!hii si kuwatafutia kazi mbichi!!
    kazi safi lakini mbona linaonekana kombora la mchana mchana,kwa mradi huu hamna pinzani

    ReplyDelete
  13. Ras Makunja na mzimu wa dansi ngoma afrika band,ili si baraha la kuwatafutia watu kazi

    ReplyDelete
  14. sasa hii shughuli kubwa mnawapa watu shughuli mbichi!kwa huu mziki mkubwa na ujumbe wake ni hatari tupu

    ReplyDelete
  15. Michuzi umetuletea machizi wa mziki??kwa ili kaka unatatufutia janga,vichaa si wanajulikana kwa tabia zao hizi?harafu wewe unawaweka ukumbuni?

    ReplyDelete
  16. Comments za WV utazijua tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...