(mwenye fulanazzz ya kijani) wakifuatilia mpambano
mchezaji wa Yanga Dedi Luba akiruka juu kujaribu
kufunga goli la kichwa,lakini mpira ulitoka
golikipa wa Yanga Feisal Omar(mwana njenje)akiokoa moja ya hatari golini kwake
Kikosi cha Yanga Ughaibuni kabla ya gemu
Kikosi cha Simba Ughaibuni kabla ya pambano
Na Ripota wetu, DC
Ile mechi ya Simba na Yanga za ughaibuni iliyofanyika wikiendi hii Washington DC, Marekani, imeishia kwa Simba kula kipigo cha mabao 5-2 zidi ya mahasimu wao Yanga. Ni Simba ndio iliyokua na nafasi kubwa ya kuibuka mshindi kwenye mpambano huo lakini wenzao wa Yanga ilionekana kuwazidi maarifa hasa kwenye kipindi cha pili. Mpaka mapunziko timu zote zilikua zimefungana 2-2.
Wakati wa kugagua timu kabla ya mchezo, Yanga walitaka mgeni wa heshima afisa balozi Mh.Suleiman Saleh aanze kwao badala ya Simba kwa wasi wasi kwamba bahati inaweza kuwa si yao kwa mpambano huo,na hii ilitokana na ushauri wa kamati ya ufundi ya wana jangwani hao.
Hatimaye, mpira ulianza kwa kasi huku Simba wakilisakama lango la Yanga kama nyuki lakini ulinzi mkali wa mabeki wa Yanga uliokua kiongozwa na Muly na Tif ukishirikiana Jongo na Jack wakisaidiwa na viungo Yahaya, Marley, na Haji uliweza kuzuia mashambulizi ya Simba.
Kunako dakika ya 30 Ebra Nyagaly aliandikia Yanga bao la kuongoza pale alipomchagua Kipa Julius Katanga na kumpelekea mzigo nyavu ndogo.
Kuona hivyo Simba walimtoa beki wao wa kutumainiwa Rashid Beach Boy na kumuingiza Salum aliyeonekana njia ya mkato pale alipomsindikiza Haji hadi akaweza kufunga bao la pili kwa kiki kali iliyomuacha kipa wa Simba akigalagala asijue la kufanya.
Baada ya bao hilo Simba walizinduka usingizini na kuanza kuliandama goli la Yanga kama mnyama aliyejeruhiwa na kuandika bao la kwa kunako dakika ya 40, bao lililogomewa na wachezaji wa Yanga kwa madai kuwa mfungaji Mashaka alimkanyaga kipa kabla ya kufunga baada ya kipa Feisal Omar(mwana Njenje) kuutema mpira uliopigwa kama adhabu ndogo na mchezaji hatari wa Simba Rahim. Kwa mshngao wa wengi Refa Mohamed Said kutoka Misri alilikubali bao hilo.
Bao hilo la Simba ni kama liliongezea timu hiyo ya msimbazi uhai na kuendelea kuwashambulia Yanga kama nyuki na kunako dakika ya 43 Shabani Mwaita aliwafungia Simba bao la kusawazisha kwa shuti kali ndani ya 18 na kumuacha kipa wa Yanga akiusindikiza mpira wavuni kwa macho. Ikawa mapumziko.
kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kulishambulia goli la Simba, mashambulizi yaliyozaa matunda dakika 56 kwa supa sab Mussa kufunga goli kwa shuti nje ya 18, Goli hilo lilionekana kuwakatisha tamaa Simba kitu kilichofanya Yanga waendelee kuliandama goli la Simba kama Nyuki na kunako dakika ya 76 ni Haji aliyepeleka Msiba Msimbazi kwa kufunga goli zuri kwa kutia kimiani majalo toka wingi ya kulia Yahaya Kheri.
kunako dakika ya 86 Yanga walimuingiza Bingo Jr badala ya Dedi Luba ambaye dakika ya 88 alipigilia msumari wa mwisho na kuandika bao la 5 ambalo lililzima matumaini na ndoto za mahasimu hao kwa mwaka huu kua ni wao.
Rashid Mkakile(Bamchawi) alisikika akisema wao kama Simba hawatacheza mechi na Yanga kwenye wanja hilo la Kalmia walisikika viongozi na wapenzi wakisema kiwanja hiki nuksi bora turudi Meadowbrook pk.
kitendo kingine kilichokuwa si cha kawaida ni mchezaji wa kutumainiwa wa Yanga Hussein Ebrahim kuichezea Simba na baade ilibidi wamtoe kwa washabiki wakidai "mtoto Yanga huyo toa nje hawezi kuifunga timu yake".
Mpaka dakika 90 YANGA 5, SIMBA 2 na kuna habari kwamba Simba wameitisha kikao kumjadili mwanachama wao aliyelamba pesa kibao kumleta fundi toka Mombasa kurekebisha mambo.

Hongera Yanga and my honey Hadji Helper.
ReplyDeleteHeeeee! simba walileta fundi kutoka Mombasa!!!! kweli wamaliwa waombe refund tartiibu!!
ReplyDeleteHadji baby i love your style,Yanga team looks bling!
ReplyDeleteJamani Hadji honey sorry nilimisi game,you look lovely baby so as the rest of Yanga team.Keep up good work Yanga.
ReplyDeleteSAFI SANA...! BADO KAKA ZAO SASA.
ReplyDeleteupuuzi mtupu.usipotoa mkono ndiyo iweje?
ReplyDeleteHadji helper nakuona unafanya vitu vyako.
ReplyDeleteHongereni Yanga japo kuwa mimi Simba kwani asiyekubali kushindwa si mshindani.
Hivi ninyi mnajifanya kucheza mpira huko, mnazo health insurance? Mkiuumia hapo, ukapoteza kazi kwa sababu huwezi kufanya kazi kutokana na majeraha na kuipoteza hiyo insurance ya kazini? Tatizo wa Tanzania wanataka kuishi hapa U.S. kama walivyokuwa wanaishi TZ. Mambo mengine hayako practical. Acheni mambo yenu ya simba na yanga. Mlikuja US kucheza soccer?
ReplyDeleteWee mdau wa hapo juu una lako jambo.Kuwananga watoto wa watu waache kucheza mpira,insurance zao wewe zinakuhusu nini? maana umeshikwa kijiba cha roho bila sababu.Wadau walio ulaya shuhuli zao wewe zakuhusu nini? shikaadabu yako,huwalishi wewe,huwalishi wewe.Inaelekea wewe EX wa mtu accent imekutoka,wakaka hawa wa simba na yanga wamekukosea nini?Usituharibie blog ya kaka Michu hapa,umechoka huna bei.Umdomo uliponza kichwa.Uchunge mdomo wako bibi.
ReplyDeleteInaelekea wee mdau wa insurance huna akili timamu.Unadhani kila mtu marekani kalost kama wewe?Lazima wewe ni EX wa mtu,haaaaaaaaaaa! hawakutaki vijembe vya nini?Wakaka wa watu watanashati hawana maneno na mtu unataka kuwavunjia heshima bure.Umelikoroga utalinywa hilo haaaaaaaaaaaaaa! huna bei.Waumie mpaka wapoteze insurance? mwanga wewe mdau maisha yanakuchanganya huko marekani rudi kwenu kigilagila.
ReplyDeleteWe jamaa hapo juu hebu tuepushie! Usije ukachafua hali ya hewa humu! Vijana wanajifurahisha na kujenga mili yao ili iwe imara. We kalia na kitambi chako na ndio maana life span ya Mtanzania miaka 45. Hivi ulishawahi kujiuuliza kwanini?? Hamna desturi ya kushiriki kwenye michezo unachojua wewe ni bia na ngono!! Halafu kuhusu insurace sijui nikujibu nini maana inaonekana hata TV huangalii!! Baba Healthy care bill imeshakuwa sheria kwahiyo sasa huku ruksa tu!! We kalia kukunja tu watu tunadibwela! mwe!!
ReplyDeleteSIMBA MAKOPO SIMBA MAKOPO! YANGA IMARA YANGA IMARA!!!
ReplyDeleteJamani chants hizi mnazikumbuka??
Kweli huyo mdau hapo juu lazima anabebea kitambi cha visheti hana sport anaijua maisha yanamchabanga ya marekani anaonea donge wengine.Kucheza mpira wa miguu ni kazi lazima mtu uwe na cardio exercise,hawa wako fiti na mapafu imara.Asituchokozee kaka zetu,hana adabu wala upendo na watu,alone and left out.Anachanganya visheti,kachumbari na Mc..D basi vinguo vimembana kwa jinsi alivyonona.
ReplyDeleteLack of activities ndio kabisa itakupa magonjwa ya moyo. Ukienda kwa daktari la kwanza analotaka kujua ni kama unafnya mazoezi na atakashauri ushriki katika michezo kama hii. Otherwise Ulaya ukiwa ni mtu wa gari na kazini tu mwili wako utaharibika vibaya. Vyakula vyenyewe ndio hivyo, Ushauri wa bure toka fanya mazoezi, tembea kwa miguu sehemu za karibu, shiriki katika michezo kama una nafasi.
ReplyDelete