Mkataba huo ukisainiwa leo saa kumi na moja kamili jioni na Kamishna wa Fedha za nje Bw. Ngosha Magonya kwa niaba ya Waziri wa fedha na Uchumi Mhe. Mustafa Haidi Mkulo na Mkurugenzi Mkuu wa Badea Bw. Abdelaziz Khelef mjini Abidjan- Ivory cost.
Vifijo na vigelegele vilitawala pale Benki ya maendeleo ya uchumi ya Afrika ilivyo badilishana rasmi mkataba wa makubaliano wa kupatiwa Mkopo wa dola za kimarekani milioni 8.

Katika kusaini makubaliano hayo Bw. Abdelaziz Khelef ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Badea alisema kuwa ,mradi una lengo la kuchangia maendeleo ya mtandao wa barabara katika kisiwa cha Zanzibar ili kukidhi mahitaji ya usafiri wa barabara, kusaidia kufufua sekta ya kilimo huko Unguja ambako kuna ardhi nzuri ya kilimo,kusaidia katika mambo ya usafirishaji wa abiria na mazao yao ya kilimo kwa njia ya barabara katika masoko na bandari kwa ajili ya kuuza nje ya nchi. Vilevile kusaidia kufufua sekta ya utalii kwa kuimarisha usafiri wa watalii kwenye sehemu za utalii huko Unguja. Na kupigana na umaskini katika maeneo yenye mradi.

mkopo huo uliosainiwa leo hii mjini hapa utalipwa katika kipindi cha miaka 30 ukichanganya na kipindi cha huruma ambacho ni miaka 10 kwa riba ya asilimia 1 kwa mwaka.

Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu-
Wizari ya Fedha na Uchumi
Abidjan
Bw. Ngosha Magonya baada ya kusaini makubaliano hayo na Bw. Abdelaziz Khelef ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Badea


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2010

    Hivi inakuaje nchi hii kila siku inakopeshwa tu, watoto wetu watapata tabu sana huko mbeleni, itakua ni kulipa madeni tu na interst (riba) kwa kwenda mbele.
    Kwa nini viongozi wetu wasitafute njia ya kuliingizia taifa pesa bila kutegemea mikopo jamani.
    Kuna mambo mengi yanaweza fanyika kubana matumizi na kuelekeza pesa kwenye mambo ya muhimu jamani:
    1. Punguza wabunge
    2. Viongozi wa serikali watumie public/private transport.
    3 mengine nisaidieni maana ni mengi.

    Ni hayo tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2010

    Land Cruiser moja ni takribani mil 100 hivi mara wabunge zaidi ya 200 haraka haraka 100x200 unapata Bil 20 sasa huo mkopo wa US$ mil8 aaaaah! Si tupunguze hizi Land Cruier jamani? Anyway they said "Africa is the best place in this world for making money while you give aids".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...