MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar leo imetoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba. Katika hukumu hiyo Liyumba anakwenda gerezani miaka mwili baada ya kupatikana na hatia ya utumiaji mbaya wa madaraka alipokuwa kazini, hususan wakati wa ujenzi wa ghorofa pacha za makao makuu ya BoT jijini Dar.
===================
Awali Liyumba alifikishwa mahakamani hapo akiwa pamoja na aliyekuwa meneja miradi wa BoT Deogratius Kweka, ambapo kwa pamoja walikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo, jambo lililopelekea serikali kupata hasala ya sh bilioni 221, kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.
Hata hivyo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka, upande wa mashtaka ulimuachia aliyekuwa mshtakiwa mwenza wa Liyumba {Kweka}, na kumshitaki Liyumba kwa kesi hiyo.Upande huo wa mashtaka uliita mahakamani hapo mashahidi 8, wakiwamo waliokuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa BoT, pamoja na kutoa vielelezo mbali mbali vinavyohusiana na kesi hiyo.
Baada ya ushahidi huo kumalika kusikilizwa, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumfutia Liyumba shtaka la kuisababishia serikali hasala ya bilioni 221 baada ya Upande huo wa serikali kupitia ushahidi na vielelezo vyake kushindwa kuithibitishia mahakama hiyo kama Liyumba alihusika na kosa hilo.Kufuatia uamuzi huo, mahakama ilimtaka Liyumba kujitetea juu ya uhusika wake katika shtaka la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.
Katika utetezi wake Liyumba alijitetea mwenyewe kama shahidi wa kwanza kutoka upande wa utetezi, na baadae alimwiita shahidi wa pili ambaye ni Bosco Ndimbo Kimela, aliyekuwa katibu wa BoT.Baada ya kumaliza usikilizwaji wa ushahidi huo, mahakam hiyo ilizitaka pande zote mbili kuwasilisha hoja zao za kisheria, ambapo alipanga kusoma hukumu dhidi ya Liyumba ifikapo May 24, 2010.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 41 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2010

    Mambo ya Tanzania kweli ni kichekesho sana, yaani mtu anafanya madudu ya ujanja na kuiba mihela kibao halafu anapewe adhabu ya miaka miwili tu jela? Baada ya miaka hiyo jamaa atatoka na kuja kutanua mitaani kama kawaida kwani atakuwa mtu huru.

    Mali alizonazo zote zinatakiwa zipigwe mnada, ili akitoka awe na nyumba ya kawaida ya kuishi na apande daladala hapo mjini.

    Nchi kama China hapo ni kitanzi tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2010

    HIZI SHERIA ZINA KASORO. ZIREKEBISHWE. ZIWE KAMA CHINA. MIAKA MIWILI KWA HASARA KAMA ALIYOSABABISHA NI UTANI NA USANII MTUPU. PERIOD. HUU SI UTAWALA WA SHERIA BALI SHEREHE.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2010

    Miaka Miwili? Amekwisha kaa mwaka mmoja mahabusu, hivyo kabakiwa na mmoja? Tulikwisha sema, ukiwa na pesa zako Bongo, wewe ni mfalme!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2010

    Maskini Liyumba!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2010

    POLITICAL DRIVEN VERDICT. SERIKALI IMEBEBWA

    KUTOJIAMINI KWA MAHAKIMU WETU. HE WAS SUPPOSED TO WALK FREE.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 24, 2010

    kweli na kukamua mipesa yote hio miaka miwili..kweli bongo tambarare..

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    Bongo tambarareeeeeeee,kama ulikuwa kiongozi mkubwa na una hela, au ulijua kula na mwenzio vizuri huwezi kufungwa hata siku moja,hapa changa ya macho tu ,coz jamaa ataambiwa akate rufaa, then anatoka,siku zote wanafungwa wasio kuwa na mtandao mzuri,wapi Zombe? Dito?,
    ankal ,acha kubana,huu ndio ukweli unless na wewe upo kwenye system

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2010

    Tanzania Oyeeh
    Wakati China wangempeleka jela maisha au kumpiga risasi MOJA TU kichwani.........
    Tanzania....Tanzania.....Nchi yenye mifumo ya utawala ya KINAFIKI kwa raia wake.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2010

    wezi wa kuku miaka thelathini wezi wa mabilioni aka vijicent miaka miwili au free poa tuuu hatufiki ng'ooo labda tuongozwe na wayahudi

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2010

    JAMANI HASARA YA 221 BILIONI SHILINGS NA KUTUMIA MADARAKA VIBAYA NI MIAKA MIWILI TU, WAKATI KIBAKA AKIIBA KUKU ANAKULA MVUA TANO, SAWA WATASEMA KUHUSU 221 BILLIONA ALIFUTIWA ALIKUWA ANAKABILIWA NA MOJA TU LA KUTUMIA MADARAKA VIBAYA, SASA TUULIZANE ALIYATUMIAJE VIBAYA NA ADHARI ZAKE ZILIKUWA NINI? HAPA INAONYESHA FIKA KUNA WATU WAKUBWA WANAHUSIKA WANATAKA KUFUKIA HII KESI IISHE TU KUTUPIGA CHANGA LA MACHO AONEKANE AMEFUNGWA NA HAKI IMETENDEKA, HII SI KWELI. NCHI KAMA AMERIKA HIVI HATA KOSA HILO LA KUTUMIA MADARAKA VIBAYA ANGEKULA MVUA SI CHINI YA MIA MOJA (100)KWA KWELI HATUTOFIKA TUNAKOTAKA TUFIKA UTAWALA WA HAKI NA SHERIA NA MAENDELEO YA KASI KWA WOTE. EBU NENDENI JUST NJE KIDOGO TU YA DAR UONE MAISHA YA WATU YALIVYO YA SHIDA WAKATI PESA ZA UMMA HAZITUMIKI VIZURI. 221 BILIONI ZINGEFANYA MAENDELEO MAKUBWA KAMA ZINGETUMIKA SAWA SAWA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 24, 2010

    Duh Haya Ndio Maamuzi ya Mahakama si tii neno lakini miaka miwili midogo sana kwa huyu Liyumba ina nipa moyo kwamba tuendako hata viongozi wawe makini hata maisha watachezea Amka Tanzania,Amka Majaji watu wote ni sawa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2010

    Usanii mtupu mwakani anasubiri msamaha wa Rais. Ingefaa afilisiwe

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 24, 2010

    WHAT A JOKE!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 24, 2010

    Only miaka 2?????? Kazi kweli kweli. Aibe 221 bill, adhabu 2 yrs???

    Kwa hali hii hat na mimi nitaiba nitakapoingia serikalini, wadau kwa sasa niko private sector, huku ninatafuta CPA, nikiipata tu naenda sirikalini,

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 24, 2010

    wezi wa ng'ombe wamehukumiwa Miaka 30 kule Morogoro. mwizi wa mamilioni anakwenda jela miaka miwili...Bongo Mswano kweli

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 24, 2010

    KWA MTAZAMO WANGU FINYU NA UFIKIRI WANGU MDOGO NA UWEZO WANGU MDOGO WA KUCHAMBUA MAMBO NINAONA KUWA TANZANIA HAKUNA HAKI HATA KIDOGO, JAPO SIUNGI MKONO WALA MIGUU UWIZI WA AINA YOYOTE ILE. LAKINI LABDA KWA VILE MIMI SI MTAALAM WA SHERIA, HIVI INAKUAJE MTU ALIYEIBA KUKU AU BAISKELI tena bila kumjeruhi mtu kwanza ANAPATA KICHAPO TOKA KWA WANANCHI kisha AKIFIKISHWA MAHAKAMANI ANAFUNGWA MIAKA MITANO au SITA,NA HAKIMU ANA "NA HII IWE FUNDISHO KWA WENGINE WENYE MAWAZO KAMA YA HUYU" SASA HUYU JAMAA KALITIA TAIFA HASARA YA TSH BILION 221 (MABILION HAYA ETI), ANAFUNGWA MIAKA MIWILI TUU na hii MIAKA MIWILI KWA TZ NI MWAKA MMOJA, HAKUNA KUFIRISIWA WALA NINI, HIVI KWELI KATIKA MABILIONI YOTE HAYO YEYE HAKUPEWA HATA BILIONI KUMI KWELI? HARAFU AKITOKA ANADUNDA MTAANI TU MABILIONI YAMEKWENDA. NA HATA AKIENDA NDANI KWA MAHELA YOTE HAYO WALIYOIBA HATAKULA CHAKULA CHA HUKO MAHABUSU HATA SIKU MOJA. KAMA NDO HIVYO WATU WATAJITOA MHANGA TUU. KWA HELA ZOTE HIZO HATA KAMA AKIPATA KAMISHENI YA BILION TANO KISHA JELA MWAKA MMOJA AAAAAAAAAAAH ILI DILI LINALIPA. ALITAKIWA KUFUNGWA KAMA MHUJUMU UCHUMI HUYU. TUSIFANYE MZAHA ETIII. EBU SOMA TENA HAPA "sh bilioni 221" MY GOD zen JELA MWAKA 1 "ALEKANGI TWIFIKA DEH"

    KCC-UKEREWE

    ReplyDelete
  17. where is justice liyumba anyongwe

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 24, 2010

    HIVI HIYO MIAKA MIWILI INALINGANA NA UBADHIRIFU ULIOFANYIKA? COZ BAADA YA MIAKA HIYO MIWILI MTU ATATOKA NA KUENDELEA KUPONDA MALI ZILIZOCHUMWA KWA UOZO HUO. INGEKUWA BORA KAMA ANGEFILISIWA MALI ZAKE KWA MANUFAA YA UMMA PAMOJA NA KIFUNGO, HELA ZINGEPATIKANA KUENDELEZA MIRADI MBALIMBALI YA UMMA KM BARABARA NA ZAHANATI!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 24, 2010

    yaaani miaka miwili tu, kwa criminal kama huyu? wakati kuna wengine wapo jela zaidi ya miaka 7 kwa makosa ambayo hata hayana maana. T.I.D alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kumpiga mtu. huyu anakwenda jela miaka 2 kwa kuiletea serikali hasara ya bilioni, bilioni , bilioni 221, kwa nchi masikini kama Tanzania, nchi ambayo ilikuwa ikiomba kufutiwa madeni, kweli inaingia akilini? Two years!!? Raia wanapata tabu vijijini huko maji hakuna, huduma za afya vijijini huko tabu, hakuna chochote maskini, huyu jamaa katia hasara, bilioni 221, then kahukumiwa miaka 2. YANI MI NAONA HII HUKUMU KAMA INAZIDI KUCHOCHEA ULETAJI WA HASARA SERIKALINI.
    MMHHH!! NI MTAZAMO TU LAKINI.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 24, 2010

    huu ni ungese mtupu jizi kama hili serikali gani hii,upuuzi

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 24, 2010

    Even with the landmarks? Hiana hiana

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 24, 2010

    bora wangemuachia tu!hii geresha kesho utasikia wafungwa wenye makosa fulani wametolewa kwa msamaha wa kiongozi fulani na yeye out!vibaka wanafungwa miaka 30 kwa kuiba pochi yenye sh 5000 yeye billions miaka 2!!!!!!!!!!

    Na wapi kesi ya zombe!!! sheria TZ zipo kwa ajili ya maskini tu.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 24, 2010

    wangemuachia tu tujue moja!na zombe ndo imetoka!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 24, 2010

    Wengine serikalini, manispaa, halmashauri name it...kama kweli mnasafisha basi fagio lisiwe na chelewa MOJA tu......

    ReplyDelete
  25. hivi nyie mnallamika nini pigeni dili hii ndio style pekee ya kutokea. watanzania vipi mnaonyeshwa how to get rich unalalamika.Uwanja ni wenu. na mhasibu yoyote wa serikalini kama huna hata ka Vogue katika utawala huu jinyonge

    Mdau

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 24, 2010

    POAAAAA,TIJIFUNZE WABONGO KUCHAGUA VIONGOZI BORA,KAMA VIP TUPOTEZEE TUU MANAKE IMESHATOKEA KWANI HAIBADILIKI MKUBWA MKUBWA TU,MDOGO HANA CHAKE,MWENYE KISU KIKALI NDIE ANAEKULA NYAMA

    ReplyDelete
  27. Mume Wangu, Mikanjuni TangaMay 24, 2010

    JAMANI WATOA MAONI WENZANGU, HIYO MIAKA MIWILI NI KWA KOSA LA KUTUMIA OFISI VIBAYA TU NA HANA KOSA JENGINE HUYO MZEE WA VIGARI VYEKUNDU.
    KOSA LA KUTIA HASARA YA MABILIONI LILIFUTWA NA MAHAKIMU HAO HAO.
    TAFADHALI MSICHANGANYE VIFUNGU VYA SHERIA VYA MAHAKAMA NA VILE VYA PORINI.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 24, 2010

    Upuuzi mtupu.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 24, 2010

    Akili za kuambiwa! changanya na zako halafu saaaaaafi.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 24, 2010

    Nyie watu mbona hamjui kufuatilia kesi. Shtaka la kuisababishia Serikali hasara ya Mabilioni liitupiliwa mbali na majaji wote watatu baada ya mawakili wa serikali kushindwa kuthibitisha. Akabakiwa na kosa moja tuu la kutumia madaraka vibaya,ambapo mahakimu wawili wamemuona ana hiyo hatia na mwingine mmoja amemuona hana hata hiyo hatia.
    UKWELI NAUNGANA NA HUYO HAKIMU MMOJA KWANI HIYO HATIA IMESHINIKIZWA TUU KISIASA ILI KUWARIDHISHA WATU KINYUME NA SHERIA. Kosa la kutumia madaraka vibaya ni kufukuzwa kazi na siyo KUFUNGWA. LIPUMBA KATA RUFAA MAHAKAMA KUU NA NAKUHAKIKISHIA YOU WILL WALK FREE.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 24, 2010

    Stupid..plain stupid..they can lock me up for 5 years if they want to if give me half of the money...infact make the a quarter of the money for 10years...Most Tanzanians will live their lives without getting even 5% of the money lost...WIZI MTUPU NDANI YA WIZI MTUPU!

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 24, 2010

    KUKU MWIKA 15, MIHELA KA HIYO MIAKA 2 DADAHHHHH!!
    TUNAKUFA BILA KELELE MASKINI SIE.... MMMMHH. POOOAAA

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 24, 2010

    WEWE MSOMAJI UNAYESEMA KOSA HAPO NI LA KUTUMIA OFISI VIBAYA TU NA SIO KUSABABISHA HASARA, HEBU TUAMBIE AMETUMIAJE OFISI/MADARAKA VIBAYA? SIO NDIO KWA KUFANYA MAAMUZI YA AJABU YALISABABISHA HASARA AU KUNA JINGINE? HAPO NI KUTUZUNGUKA TU ILI AONEKANE HAJATENDA KOSA KUBWA, UKWELI UTABAKI PALE PALE, OTHERWISE ALITUMIA OFISI VIBAYA KWA KUIGEUZA BAA AU HOTELI AU LODGE? ALIKUWA ANAFUGA KUKU NA MBUZI OFISINI! UPUUZI MTUPU

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 24, 2010

    Yes Nakubali Tz tuna wasomi wa Ukweli Katika kila fani ,na hata wasiosoma wanaona faida ya wasomi wetu bongo (hatari kweli kweli Vyeti mitaani)

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 24, 2010

    ndugu yangu michuzi kwa kweli mpka yaan mwili usikia baridi! yaan madudu yote yale bwana mkubwa huyo! then miak 2 tu! bora wasingetupotezea muda! wa kufatilia mie nadhan wangemuachia huru tu! kama bwana zombe,people are mature!? lakin hapo nyumban ni pagumu sana na laana ipo mie nadhan, iwezekan leo maisha ya mtz halis hakuna asiyeyajua leo inakua ubabaishaji tu! na kutokupendana, mie nadhan sheria zetu zingeangaliwa tena kutokana na maisha yetu halisi!! mfano kaka michu hebu agalia china, hata pia japan wako makin sana kwenye ubathilifu na ndio nchi tajir angalia pia usa,then tunalia tunataka maendeleo maendeleo gani yasiyo a uzalendo!! mwalimu nyerere nadhan wangemdondosha kwa presha mzee wa watu!! jaman kweli mtu anatafuna fedha zote hizo wakati hapo mwananyamal hosp. dawa mtihan!?,amana hosp.wamama wajawazito vitanda haba!? barabara kiwango cha lami ziro folen sasa nasikia ndio usiseme!! inakua kama hawaoni wakitoka nje!! hata flyover kuanzia posta hadi mbezi! jaman!!?? kwa kweli nchi haitufundishi bali inazid kupotosha,hiyo ni laana!!
    mdau japan.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 24, 2010

    Daudi, upo Juu!

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 24, 2010

    Vidagaa tu hivi, mapapa bado yanaogelea.

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 24, 2010

    bill 222.kwa miaka 2? huo wizi unalipa sana.kwa walio na nafasi za kuiba wataiba sana.Hata kama ni 1b. kwa miaka 10 wengi watajitolea,biashara gani utaweza kupata faida hiyo kwa muda huo.

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 24, 2010

    UNYESEMA UKAFUNGE MIAKA 10 ILI MRADI UPATE KASEHEMEU KA $$$ ZA MTUHUMIWA UMENICHEKESHA SANA.



    (US BLOGGER)

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 25, 2010

    Msamaha wa wafungwa kila mwaka December 9th ndo Liyumba atakuwa huru. Na hapa hakuna kesi tena. Hongera mafisadi wa Tanzania. Endelea kuchangua Viongozi wabovu. Mmtalionja jiwe. Mafisadi wa Tanzania hawanaga kesi. Tanzania hakuna sheria endapo kama wewe ni fisadi. Sheria huwa inawakumba walala hoi.

    SIKU YA UHURU DECEMBER 9TH /2010 LIYUMBA JUU ZAIDI, JK atakutoa kwa sababu ndo mlezi wako.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 25, 2010

    mimi ninafikiri hastahili hata kufungwa nimpongeze hakimu aliyemwona kuwa hana hatia. Haya matumizi mabaya ya ofisi yanafanywa sana na wakubwa wa nchi yetu. Labda wanefungwa wao kwanza. hapa nchini ufisadi umekuwa sana na wanaofungwa ni watu wadogo tu wasio na kitu. Lakina wakubwa wote ni mafisadi wakubwa wanaostahili kwanza kwenda jela. Pole sana ndg yangu lyumba. baada ya kukuta rufaa utatoka tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...