Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA Mhandisi Profesa Jamidu Katima Akitoa neno la Utangulizi wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kamati za watumiaji za Kimikoa kanda ya Pwani yalifanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20/05/2010 maeneo ya Kundunchi Beach Hotel & Resort.
Mwakilishi wa Banki ya Dunia bi. Rosemary Rop, akitoa ufafanuzi wa Mafunzo hayoKatibu Mtendaji wa EWURA CCC akitoa somo wakati wa mafunzoMmoja wa wanakamati akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo hayoPicha ya pamoja ikwajumuisha mgeni rasmi, wawezeshaji na washiriki wote wa mafunzo kanda ya Pwani.


Nishati na Maji ni vitu ambavyo vinagusa maisha ya kila mtanzania. Kwa kuzingatia unyeti wa sekta ya nishati na maji, Serikali iliamua kuwepo na udhibiti ili kulinda kuimarisha ubora wa huduma hizo kama zilivyo huduma zingine.

EWURA ni mdhibiti katika sekta ya Nishati na Maji. Kwa upande mwingine, lipo Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA lijulikanalo kama EWURA Consumer Consultative Council (EWURA CCC).

Pamoja na majukumu mengine, Baraza hili lina jukumu la kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA, jukumu ambalo hutekelezwa kwa kutumia njia mbalimbali kama vile kutoa ushauri kwa madhibiti na watendaji wengine, Kupokea na kusambaza taarifa kuhusu maslahi ya watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA, Kushauriana na wenye viwanda, Serikali na vikundi vingine vya watumiaji juu ya masuala yanayowahusu watumiaji.

Katika kukamilisha malengo yake, Baraza limeunda Kamati za Watumiaji za Kimkoa zitakazofanya kazi bega kwa bega na EWURA CCC. Kamati za watumiaji za Kimkoa zimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji ya Mwaka 2001 Ibara ya 414 kifungu cha 30.

Kamati hizi ambazo ziko kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara tayari zimeshafanyiwa mafunzo yaliyofanyika katika Kanda nne ikiwa ni Kanda ya Kaskazini mikoa ya Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Manyara; Kanda ya Ziwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, na Kagera; Kanda ya Kati mikoa ya Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa, Kigoma na Rukwa; Kanda ya Pwani, mikoa ya Pwani, Lindi, Ruvuma, Mtwara na Morogoro.

Kuanzishwa kwa kamati hizi kutarahisisha na kuimarisha upatikanaji huduma za nishati na maji kwa kuwa nguvu zaidi katika kutetea maslahi ya mtumiaji itakuwa imesogezwa karibu watumiaji katika mikoa yote ya Tanzania Bara.Kamati hizi tayari zimeanza kutekeleza majukumu yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...