Mchezaji Kaka akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg sasa hivi akiwa na timu yake ya Brazil
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Brazil wakiwasili Sauzi sasa hivi. Wanatarajiwa kuanza tizi. Baod haijajulikana kama watakuja Dar kwa mechi yao na Taifa Stars Jumatano kama livyotangazwa jana, kwani hakuna taarifa hiyo katika kambi yao huko Sauzi.
Picha na richard maspero wa Globu ya Jamii
Habari Kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2010

    biashara na ianze!!

    duh shughul ipo afrika sasa

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2010

    sasa kaka michuzi ina maana Brazil hawaji bongo tena,sasa zile habari za kina TEnga na wenzake ni uzushi mtupu au vipi,AU ndo mambo yaleyale ya Danganya toto Kula kande mbichi.Si wangesema mapema tu kwamba mambo sio mambo na hayajawa mambo....VIPI KUHUSU YALE MABILIONI YA MAANDALIZI YALIYO CHINI YA WAZIRI FULANI KWA AJILI YA WORLD CUP ATTRACTION YA NEW STADIUM YATAENDA WAPI,MAANA BADO HAKUNA MATUMIZI KWA KUWA HAKUNA TIMU ILIYOKUJA KUCHEZA BONGO,AU NDO CHANGA LA MACHO LA WIZI WA MABILIONI KWA KISINGIZIO CHA NEW STADIUM ATTRACTION...HAYO MABILIONI AMBAYO NAFIKIRI MPAKA SASA HAYAJATUMIKA NI AFADHALI WAKAJENGEE HOSPITALI/ZAHANATI ZA KISASA HUKO VIJIJINI AU SHULE......ASANTE KAKA MICHUZI

    ReplyDelete
  3. hii ni timu ya pili kuwasili hapa jana jioni Australia ndo walikuwa wa kwanza kuwasili hapa world cup is here ni time sasa ya timu za africa kushine hii bafana mdebwedo sijui watafika wapi manake hapa kila gari full mabendera mie nimetundika zangu za tanganyika hahah

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2010

    Kumekucha jamani....Nagira A Town

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2010

    sijawahi kuona timu ikisharipoti kwenye nchi ya mashindano then ikaondoka tena kwenda kwenye friendlies...TFF watadanganya watu tena kwamba they are just on transit to DSM as it is easier to connect from Rio thorugh ORTambo...lakini kama hata kambi ya timu haina taarifa na match dhidi ya Tanzania...hizi ni hekaya za alfu lela ulela tu...no brazi no nothing...!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 27, 2010

    TFF bado wanaota nadhani.Sidhani kama watatoa mguu wao tena kuja Tz maana tayari wameshafika uwanja wa mapambano, SA. Hiyo budget ya US$ 6mil, kama kawaida wai-EPA tu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2010

    jana kwenye taarifa ya habari ITV saa mbili usiku habari za michezo, balozi wao alisikika akisema kwa ufasaha kuwa watakuja hata tz kukipiga na....... imekuwaje tena? au ndege imepotea njia nini?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 27, 2010

    Tukifika Sauzi..!!!Hey Bra - utiini Weena.....!!! @ Nagira.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2010

    MNATEGEMEA BRAZIL WASICHEZE MECHI ZA KIRAFIKI HADI WORLD CUP IANZE...? KAMA NI UONGO BASI BALOZI WAO PIA NI MUONGO.. NA KAMA KAMBI HAWANA TAARIFA SIO JUKUMU LA WACHEZAJI KUJUA WATEZA MECHI IPI YA KIRAFIKI NI SUALA LA UONGOZI, WAO WACHEZAJI WANASUBIRI KUAMBIWA TU... MBONA HAMJIAMINI...

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 27, 2010

    jamani watanzania muwe na subira sio mnakurupuka tu na kuanza kulaumu na kutoa maneno ya kejeli, mechi ipo na ni tar 7 june,,

    ata ivyo bw. Tenga alisema ishu bado haijawa comfirmed, acheni hizo bwana

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 27, 2010

    NI KWELI WATACHEZA NA TANZANIA TAREHE SABA JUNE 2010 HATA HAPA UK BBC WAMESEMA HIVYO SASA HIVI KWENYE TAARIFA YA HABARI YA SAA KUMI NA MOJA JIONI ZA HUKU, WAPI SIJUWI INAWEZA KUWA HUKO HUKO SOUTH AU WATAKUJA TANZANIA KWA MUDA KAMA HOLIDAY NA KUCHEZA NA TANZANIA

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 27, 2010

    we mbaruku ndo full mdebwdo kweli kama hiyo timu ya zenji ni bab kubwa ikawaje hawajatuwakilisha huko south africa?? mambo yenu ni ndani tuu nje mnalambishwa alamba alamba dizain khalua khalua mkirudi mmelegeaaaa

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 27, 2010

    kuna wachangiaji mnaboa sana uwezo wenu wa kufikiri mdogo sana sasa south na dar kuna umbali gani ni just masaa mawili na nusu hadi 3 kwa ndege wao wanajua wamekuja africa na match yao ya ufunguzi ni tarehe 15,haiwezekani source zote ziwe za uongo someni wesite nyingi sio kutegemea michuzi na ITV pekee brazil wanacheza na stars jumatatu tarehe saba saa moja usiku FYI

    ReplyDelete
  14. MECHI IPO KAMA ILIVYOPANGWA

    Mheshimiwa Balozi wa Brazil na wadau wahusika wa Tanzania wameshakamilisha maandalizi ya mechi

    Ukifungua link hii ya FIFA utaona habari ya mechi hiyo imeshapangwa 7th June, 2010

    http://www.fifa.com/associations/association=bra/index.html

    MAKULILO, Jr.
    www.makulilo.blogspot.com
    www.scholarshipnetwork.ning.com
    San Diego, CA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...