Aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu Commercial Bank of Africa (CBA), Nehemia Mchechu (wa pili kushoto) na mkewe Mercy, wakiwashukuru wafanyakazi wa benki hiyo mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya mbuzi, wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa Sweet Eazy, Masaki, Dar usiku wa kuamkia leo. Mchechu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu Commercial Bank of Africa (CBA), Nehemia Mchechu (katikati), akifurahia zawadi ya picha iliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa Sweet Eazy, Masaki, Dar. Wa kwanza kushoto ni mkewe Mercy na kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji mkuu wa CBA, Julius Mcharo. Mchechu ameteuliwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mwanamuziki, Mafumu Bilal 'Mbombenga', akiimba wakati wa hafla ya kumuaga Ofisa Mtendaji Mkuu wa Commercial Bank of Africa (CBA), Nehemia Mchechu (hayupo pichani), iliyofanyika katika ukumbi wa Sweet Eazy, Masaki, Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2010

    Poor Goat

    ReplyDelete
  2. Hongera Mhishimiwa! Wafanyakazi wa CBA nao wana visa! wana-mechishia bosi wao mpaka na Mbuzi, mbuzi, kivazi vyote sare sare maua....hhahahaa. Safiii. Mpare anaondoka anamwachia Mpare.

    Naondoka.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2010

    Ikulu wamefanikwa kumweka mtu wanayemtaka..kweli mbongo tambarare!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2010

    Nehemia mimi ni mtanzania ninaishi hapa Dar es Salaam na mfanyakazi katika kampuni moja, sasa mimi naomba nipate nafasi ya kuonana na wewe kwani nina habari za nyumba moja ya NHC ambayo ipo Upanga awali walikuwa wanakaa watanzania wenye asili ya kihindi lakini sasa wamehama na kuhamia kwenye nyumba kubwa ambayo wemewenza kununua funguo, sasa tatizo langu ni kwamba nyumba ile wameweka madareva wao wa magari wanapaki na kulala, mimi ni sina pesa nikiripoti hii nyumba kwa njia za halali nitaikosa lakini nina imani na wewe nikianzia kwako sitaikosa kwani mh. raisi anajua utendaji wako wa kazi ndio maana akakuteua

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2010

    Ooh! waosha vinywa .... mnapenda kuhisi mambo... poor nyie loh! eti mpare hhahah .. .. majungu loh! ukabila bongo loh! Ee.. Mwenyezi Mungu tuhurumie...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...