Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha Jaji Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Uongozi na wajumbe wa tume hiyo katika sherehe zilizofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wajumbe wa tume hiyo ambao pia waliapishwa ni pamoja na Jaji Hamis Msumi na Ndugu Gaudios Tibakweitira.Pichani Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kupokea miongozo ya kazi
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Tume ya Maadili ya uongozi muda mfupi baada ya kuwaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kutoka kushoto ni Jaji Hamis Amir Msumi,Ndugu Gaudios Tibakweitira na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva.

Tanzania hatuna wasomi wengine zaidi ya hao??? Hawa si wanastahili kupumzika sasa wapishe vijana. Wasomi wetu wanaograduate kila siku watashika nafasi hizo lini???? Toka tukiwa wadogo hadi sasa tunazeeeka majina ni hayohayo, ajira kwa vijana wasomi iko wapiii???!!! Mungu tusaidie TANZANIA yetu iwe na huruma kwa vijana watakuwa machinga hadi lini.
ReplyDeleteTANZANIA HATUHITAJI TUME YA MAADILI KWANI HAIJALETA TOFAUTI YOYOTE YA KIUTENDAJI KWA VIONGOZI, HEBU TUANGALIE NYUMA, WAZIRI MKUU ILIMCHUKUA ZAIDI YA MIAKA KUTANGAZA MALI ZAKE KITENDO AMBACHO KILIKUWA NI UKOSEFU WA MAADILI LICHA YA VYOMBO VYA HABARI KUMSIFU BADALA YA KUHOJI ALIKUWA WAPI MUDA WOTE; SASA HUYO NI KIONGOZI WA JUU SERIKALINI AMBAYE ANGEKUWA NI MFANO KWA WENGINE. TUKIANGALIA MAWAZIRI NA VIONGOZI WENGINE UTENDAJI WAO NI UNAOTIA MASHAKA WENGI WAO HUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KUENDESHA SERIKALI! NA MAMBO MENGINE MENGI TU YANAYOONESHA UDHAIFU KIUTENDAJI KWENYE VYOMBO VYOTE SERIKALINI.
ReplyDeleteRECYCLING!
ReplyDeleteTume ya maadili inachaguliwa mwishoni kabisa mwa awamu ya utawala wa raisi ili ifanye!!!!!!???????
ReplyDeleteWazee tu na majina ni yale yale tu yanachosha, ndio maana tunarudi nyuma. Mfano mzuri ni Bodi za ATC na TANESCO ziliwekwa watu walioharibu siku za nyuma, basi wakaendeleza kuyaua mashirika haya muhimu. Tuwe tunaangalia damu mpya mawazo mapya, mbinu mpya na mikakati mipya.
ReplyDeletemzee Tibakwitira enzi ya mwalimu.wapi Jovin na Edgar ?
ReplyDeleteReclycling!!! Daaah nimelipenda hili neno. The same old politics.Wastaafuu tuuuu. No future for new generation....
ReplyDeleteNCHI HII BWABNA...HEBU WAC=HEKI HAO WAZEE ,HIVI WATAFANYA NINI??
ReplyDeleterecycling ni nzuri ila si kwa akili na kazi za watu.Daaah hii inaitwa "Ulaji"
ReplyDeleteNdugu zangu watanzania, huu ni utamaduni wetu, na tutaendelea kuudumisha! Wawe wazee au picha hayo yapo nje ya katiba.
ReplyDeleteJayK.
jovin yuko Pennslyvania na Edgar Washington DC
ReplyDelete