Ukarabati wa miundombinu ya Umeme inayoendelea kufanyika katika maeneo kadhaa ya Manispaa ya Morogoro na umeleta athari sehemu mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Mkoa ambayo imekumbwa na giza totoro. Hadi kufikia saa mbili usiku huu hali bado tete na imewalazimu wauguzi na madaktari waliokuwa wakitoa huduma kwa wagonjwa kuwa na wakati mgumu na kutumia taa za kandiri pamoja na mishumaa kama ilivyokutwa wodi namba moja ya majeruhi wa ajali. Haikufahamika mara moja kama Jenereta la Hospitalini hapo ni nzima ama la, ama imekosa wese....Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2010

    haya tena mpaka koroboi ianguke iunguze wagonjwa ndio itazungumziwa bungeni na kutafutiwa jawabu

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2010

    umeme adi yesu hatapo rudi !!zoeni hali !!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2010

    mmh tanzania maendeleo tutayasikia tu...labda wakoloni warudi tena!!hosp ya mkoa umeme tabu?..

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2010

    Ni mambo ya kawaida umeme kukatika. Hata huku Ulaya umeme huwa unakatika. Hiyo inaitwa hitilafu ya kiufundi. Morogoro hospital umeme huwa sio tatizi sana. Ni dharula tu ya kawaida ambayo ni kitu cha kawaida. Kila jambo linarekebishika. Ukizingatia ni nchi za dunia ya tatu, tuvute pumzi!!
    Mdauzzzzzzzzz

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2010

    john mashaka andika atiko kuhusu hili, kweli bongo tambarare

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 24, 2010

    Tarehe Sun May 23, 11:55:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    wewe upo ulaya hipi ama unajishaua !!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    Tarehe Mon May 24, 12:10:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

    na wewe unamtaka huyo john mashaka andike nini sasa !! undikiwe article then what?? umeme ndo utarudi??
    wabongo wamerithika ndomana hatutaendelea kamwe !! kama nyie wananchi manaona kero kutokuwa na umeme do something then!! siyo mnataka kuandikiwa article tu na john mashaka

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2010

    mdau 11:55.kweli unauhakika au ndo kulopoka tuu.hali hii sijaiona ulaya.umeme ukikatika na kwataarifa maalum generator linakick in rightaway.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2010

    MDAU HAPO JUU UMECHEMSHA,ULAYA NCHI GANI?NIPO HUKU MIAKA KADHAA SIJAWAHI KUONA UMEME UMEKATIKA HUKU,ATA NCHI MASKINI KAMA ROMANIA BADO KUNA UMEME.KWELI BONGO TAMBARARE

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2010

    vipi wewe mwenzetu uko Ulaya ya Mbinga? Maana Ulaya (europe) hakuna hizo unazodai wewe? Wewe kwenye shida za wenzetu, tena hospitali ya mkoa, unaleta mzaha!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 24, 2010

    loo huo umeme unaokatika ulaya sijui ni ulaya ipi huyo waziri wa nishati angejiuzulu siku hiyohiyo wazungu wana midomo mirefu kweli hasa likija swala la huduma bora mbona utajuta kuwa waziri ?? utabebewa mabango hadi kwenu sio bongo umeme unakatika bila taarifa na isidingo taarifa ya habari hamuoni ukirudi mshalala huko sirudi kabisaaaa na Mungu anisaidie maisha ni popote na nyumbani ni pale roho yako iliporidhika napo acheni tu majuu kuna raha ati ohooo ankali ana majukumu flani tu yanambana haki ya nani hata yeye angebaki huku

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2010

    jamanieee naomba mtambue kwamba hospitali ni sehemu ambayo kwakweli haitakiwi kukosa umeme aidha wa tanesco au ikibidi hata wa jenereta,hospitali kuna watu wanatakiwa kufanyiwa upasuaji inakuwaje umeme ukiwa umekatika gafla labda mzazi akatakiwa kufanyiwa operation ya gafla?hospitali ya mkoa inashindwa kumiliki generator msitete hilo ni uzembe wa hali ya juu.niwaeleze kwamba hospitali ya morogoro sio tu umeme mimi binafsi nilikuwa na mgonjwa hapo hospitali drip unaambiwa ukanunue ukienda dirishani unaambiwa hamna inabidi utoke ukatafute,hata siringe pia hawana,iliniuma sana lakini namwachia mwenyezi mungu,nilikuwa na mzazi wangu alilazwa hospitali hiyo alikuwa hajitambui yupo mahututi lakini walimlaza wodi ya kawaida,mgonjwa alikuwa anaishiwa pumzi mpaka daktari anakuja anamkandamiza kifua ila aweze kupata pumzi,why mgonjwa asipelekwe icu akawekwa oxygen?ukiwafwata manesi wanajibu kwa dharau,wanaendelea kukuagiza dawa na madrip na masiringe wakati wao wameshajua kabisa kwamba mgonjwa atafariki,naomba niulize hospitali kubwa kama hiyo haina oxygen?????waziri wa afya analijua hilo?na mgonjwa wangu kuna wakati alikuwa anaishiwa pumzi unaona kama anafariki mimi nachanganyikiwa nakimbia wagonjwa wenye nafuu wanakuja kumpepea badae anaamka tena,cha ajabu mpendwa wangu alivokosa pumzi gafla hata dakika hawakuchukua wakawa wamesha mfunga shuka im not sure kama alikuwa ameshakata roho but namwachia mwenyezi mungu,mh.waziri wa afya David Mwakyusa naomba uliangalie swala la OXYGEN,na vitu vingine muhimu kama gloves,syringe,drip n.k.pia wagonjwa ambao wapo mahututi naomba wawekwe kwenye chumba maalumu chenye utulivu wa hali ya juu.ni hayo tu naomba uniwakilishie hayo kwa wadau akiwapo mheshimiwa Mwakyusa!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 24, 2010

    Michuzi nahofia wakubwa wanaweza kukusakama kuwa umetumwa kwa kuweka picha zinaoonyesha uozo uliotanda Bongo katika blog hii. Nahofia unaweza kuambiwa si mzalendo. Wakubwa wangependa taswira kama hizi zisivuke mipaka pamoja na kuwa dunia sasa ni 'global village'. Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hii ndio Tanzania ya karne ya 21. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 24, 2010

    ULAYA YA WAPI UMEME UNAKATIKA? HATA NCHI MASIKINI KAMA POLAND HAUKATIKI, HATA HIVYO UMESHASEMA KAMA UNAKATIKA BASI NI KWA SABABU ZA KI-UFUNDI SI KWELI LITAKUWA LA KI-ITALAFU KWANI KAMA NI LA KI-UFUNDI MAFUNDI WOTE WA UMEME UNAOWAJUWA WEWE WAKO HUKU ULAYA, MIMI NIKO HUKO ULAYA SASA NI MIAKA 15 HATA SIKU MOJA SIJAPATA KUONA SI UMEME AU MAJI KUKATIKA HATA KAMA ULIPI BILL. SWALA LA KUKATIKA MAJI LA BONGO SINA UHAKIKA NI KAMA LA KI-UFUNDI AU ITILAFU!!!! SANA SANA NI TATIZO LA PRIORITY NA UMASIKINI WA SERIKALI

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 24, 2010

    ...cha moto lazima tukione na akili zetu mgando; Liyumba kafuja mali ambayo ingeweza kuongeza uwezo wa kutatua tatizo la umeme kafungwa miaka miwili ambayo kimsingi ni kama kaachiwa huru. Kisha tunaanza kulia hakuna umeme... sh*^%&t

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 25, 2010

    Shida yangu si huyo aliyetaja Ulaya
    Hata ninyi mnaojifanya mko Ulaya inawezakana mko Kilosa Mazinyungu huko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...