na
Innocent Mungy - Shanghai,China
Tarehe 17 ya Mwezi mei kila Mwaka, Dunia huadhimisha siku ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Jamii (TEKNOHAMA). Nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano Duniani, International Telecommunications Union (ITU), huadhimisha siku hii muhimu kwa nia ya kukumbushana umuhimu wa teknologia ya habari na Mawasiiano kwa maendeleo ya dunia na jinsi inavyoweza kuboresha maisha ya wanadamu kwa ujumla.
Maadhimisho ya mwaka huu yanaadhimishwa kimataifa katika jiji la Shanghai nchini China ambako maonesho makubwa ya teknolojia yanafanyika kwa kipindi cha miezi sita. Maonesho hayo maarufu kama Expo Shanghai 2010, yanayoendana na kauli mbiu ya mwaka huu, "Miji Mizuri, Maisha Bora" yalianza rasmi mei mosi mwaka huu na yataendelea hadi mwezi October 2010. Bofya hapa kwa habari zaidi: http://www.itu.int/wtisd/2010/theme.html
Mamilioni ya watu wamefurika kwenye jiji hili la Shanghai linalokadiriwa kuwa na wakazi milioni 22 na ushee katika kusheherekea maadhimisho haya yatakayofikia kilele jumatatu tarehe 17 Mei 2010 kwa hotuba na makongamano mbalimbali yanayolenga katika kuelezea mafanikio ya sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano na mchango wake katika kuboresha majiji na miji ili kuwa mahali pazuri zaidi pa kuishi.
Watanzania kadhaa wako mjini hapa kushiriki katika maadhimisho haya yaliyopata baraka za ufunguzi na Mama Anna Tibaijuka, wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (HABITAT).
Jana katika Banda la Umoja wa Mataifa, ITU ilifanya washa kuhusu umuhimu wa TEKNOHAMA katika kuboresha mazingira duniani na hasa katika kujenga "miji kijani" ( ICT's: Building the Green Cities of the Future).
Wataalamu mbalimbali walitoa mada zilizoibua hisia mbalimbali kutoka kwa washiriki hususan mapendekezo ya ITU ya kuwa na charger moja kwa simu zote (Universal Charger). Mada ingine iliyosisimua ni ile ya uchafuzi wa mazingira kwa magari yanayotoa hewa chafu ambapo imependekezwa nchi duniani na hasa majiji yajizatiti kuyaondoa magari yanayoharibu mazingira zaidi.
Bofya hapa kupata mawasilisho ya mada hizo kwa undani.
Teknohama ni kitu gani in English?
ReplyDeletekanzuri binamu tunategemea mengi toka huko hasa mambo mapya ya teknohama ambayo kizungu chake sisi huku pangani ni taabani
ReplyDeleteteknohama= teknolojia ya habari na mawasiliano.
ReplyDeleteMdau
Kariakoo Shimoni.
FANYA KAUTAFITI KIDOGO TU, UNA-COMPUTER TUMIA PROFESSOR GOOGLE.COM ATAKUHABARISHA TEKNOHAMA NI NINI. SI KI-ENGLISH NI KISWAHILI, NI KIFUPI CHA MANENO YA FUATAYO: TEKNOLEGIA YA HABARI NA MAWASILIANO SO THEY HAVE JUST TAKEN SOME OF LETTERS IN EACH WORD AND FORM THAT SO CALLED TEKNOHAMA; AS AS FOLLOWING TEKNO-legia ya HA-bari NA MA-wasiliano
ReplyDeleteNadhani ni technology
ReplyDeleteLakini nauliza siye tunaenda kuonyesha nini au tunaenda kung'aa macho tu?
Nilitegemea hizo chance wangeenda vijana wa college wanaosoma vyuo vinavyohusika. Hao watu wakuu wazee wakienda watajifunza nini na tungeomba elimu yao tujue haya majambo wanayajua vipi?
kwako anony wa Tarehe Sun May 16, 07:24:00 PM,
ReplyDeletetembelea, http://www.teknohama.com/ utajua ni nini.
TEKNOHAMA ni Teknologia ya Habari na Mawasiliano- Information and Communication Technology-ICT.
ReplyDeleteJAMANI WAVAAJI SUTI, ILE LEBO PALE CHINI YA MKONO WA SUTI INAPASWA KUTOLEWA BAADA YA KUNUNUA SUTI, MSIFIKIRI NI UREMBO. NI USHAMBA KUVAA SUTI NA LEBO. ANGALIA SUTI YA HUYO TALL MWENYE SHATI JEUPE...
ReplyDeleteTeknohama = Information Communications Technology.
ReplyDeletewanashangaa tu majengo hao....akimaliza hapo wanunue suti na maredio/tv warudi navyo..with no any implementation ya kilichowapeleka huko
ReplyDeleteanony wa tarehe Mon May 17, 12:14:00 AM, hivi vijana maana yake nini? Vijana wa shule wanajua technohama? anyway ya wataalamu tuwaachie wataalamu
ReplyDeleteAsanteni wadau kwa kunieleza maana ya teknohama. Ila nimeangalia tovuti yao (www.teknohama.com) kwa maelekezo ya mdau mmoja na niemona wanatumia neno "wavuti", imenichanganya tena, kwani haipaswi kuitwa "tovuti"? "Wavuti" ni nini?
ReplyDeleteBy the way, "blog" pia ni nini kwa Kiswahili?
TEKNOHAMA KWA KINGEREZA NI "INFORMATION AND COMMUNICATIONS TECHNOLOGY".NENO TEKNOHAMA NI UFUPISHO WA ISTILAHI TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO AMBAYO ILITOHOLEWA MOJA KWA MOJA KUTOKA KWA ISTILAHI YA KIMOMBO KWENYE NUKUU PALE JUU.
ReplyDeleteNYONGESA MARTIN WAFULA
MASINDE MULIRO UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY.KENYA