habari za kazi bwana michuzi. siku chache zilizopita uliweka tangazo la itv kuwa ipo katika mtandao kupitia
baadhi yetu huku ughaibuni tulijaribu na kuipata live. sasa leo nimejaribu naonma tayari imeshawekwa kufuli. kunahitajika username na password. naomba uwawekee wadau habari hii ili kama kuna mtu anajua jinsi ya kufanya ili tuendelee kupata news za nyumbani atusaidie.
mdau ughaibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2010

    unachosema ni kweli,hata mimi nimefanikiwa kutizama kwa siku moja tu halafu ikawa locked,nadhani wanatoa ofa ya siku moja kama majaribio,nimejaribu kutafuta code bila mafanikio.
    mwenye kuifahamu code tafadhali tujulishane.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2010

    Kwa ufupi majaribio yameisha,kwasasa unatakiwa kulipa ili uendelee kuona na kusikia habari za nyumbani.Ingia kwenye PAYPAL na lipia kwa muda utakaouchagua hapo tena utapatiwa password yako. BURE INAUWA..!

    ReplyDelete
  3. Ni kweli imewekwa kufuli ila mie nilichofanya nililipia Euro 5 ili kuweza kupata zile channel zote na kweli ITV inaonekana vizuri sana kwa sasa na haina tofuti na ukiwa nyumbani, haikati kati. Ipo clear sana. Hiyo Euro tano itakuwezesha kuona zile channel kwa muda wa mwezi mmoja. Nadhani kabla ya hapo ilikua imewekwa kwa majaribio na ilikua haionekani vizuri, ila kuanzia leo ilipowekewa kufuli inaonekana vizuri sana. Naona wameamua kutubania ila ndo gharama tena za uwendeshaji ambazo ni lazima kama sie walaji lazima tuzilipie.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2010

    SASA MUDA WA KULIPIA UMEFIKA. MDAU LIPIA UENDELEE KULA RAHA, BURE IMESHAPITA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 16, 2010

    Mwanangu sasa hivi imekuwa lipia uone..lipia kwa credit card euro 5.58 kwa mwezi uone kitu live. Mimi nimeshalipa na naendelea kuona kitu live kama nipo Bongo Vile.. Pole sana ndio biashara hizo. Mtu uonjeshwa then laters unalipia!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 16, 2010

    kuhusu kufuli siwezi kukusaidia, lakini kwa siku 4 nilizoweza kuingia mtandaoni hapo wala sikufaidi, chenga kibao, kata nyingi kama vile antena imejaa kunguru.

    isitoshe muda mwingi nilikuwa naona habari za ulaya nadhani usiku kwa bongo bado wanarusha channel za nchi za watu.
    Lugalo ATL

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 16, 2010

    Lipia EUro 60 kwa miezi 12, au kwa mwezi Euro 5, utapata username and password

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 16, 2010

    naona kuna ku donate sio wezi hawa lakin???

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 16, 2010

    Ndugu muulizaji, acha kupenda dezo! huyo jamaa naye anatumia gharama kama kulipia bandwidth, Computer, Satellite, Umeme, Programs, Muda, Wafanyakazi, Domain,nk. Ameweka iwe ya kulipia kujipatia riziki yake.Vilevile hudama hii ina manufaa sana kwa wanaohitaji. Gharama yake ni dola 7 kwa mwezi. Tena ameweka bayana kabisa unamlipa kwa paypal. Tuache mambo ya wizi na kupenda dezo hayatatuletea tija.

    Mzozaji

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 16, 2010

    Pole mdau nami yalinikuta hayo jana. Mimi pia nipo ughaibuni.Jana jioni nataka niangalie taarifa ya habari nikakuta kufuri,usrname na password.
    Mdau yeyete mwenye kujua tafadhari tunaomba uturushie hapa. Inawezekana jamaa walisoma wakaona bora watufungie.

    Mdau Belgium

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 16, 2010

    Pole sana mdau hata mimi imenitokea hiyo hali.Unatakiwa ku donate kama Euro 5 ambayoni sawa na dolar 7 kwa mwezi 1 ili upewe Name na password. Tumia paypal ku-donate, ni safe and secured.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 16, 2010

    MIMI NAENDELEA BADO KUIPATA.
    ILI UWEZE KUENDELEA KUIONA, KAMA ULIVYOSEMA, INABIDI UWE NA USER NAME NA PASSWORD.
    HIVYO UTAVIPATA KWA KULIPIA.
    PALE PANAPOSEMA -DONATE TO WATCH-NDIPO UINGIE. GHARAMA ZAKE NI EURO 5 KWA MWEZI.
    UKIKUBALI KULIPIA, AMA KWA PAYPAL AU CREDIT CARD, NDPO WATAKUTUMIA HIZO USER NAME NA PASSWORD. ILA MIMI NILIPOLIPIA TU NIKAWATUMIA E MAIL KUWAJULISHA, NA JIONI YAKE WAKANITUMIA.
    HIVI SASA NAFAIDI CHANNELS ZOTE KARIBU 15.
    AHSANTE
    Mndengereko, ukerewe

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 16, 2010

    acheni kupenda dezo.nilipoiona siku yakwanza nikajuwa hapa kuna namna wala sijajishukisha..wewe kuna kitu gani bure dunia yaleooo...tufanye kazi na tuache starehe

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 16, 2010

    Tena sasa hivi wameongeza na East Africa Television (Channel 5) , Midundo motomoto. Sasa hivi imebaki TBC tuu akiweka hiyo tumemaliza.
    Lipia ufaidi achana na dezo inaua.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 16, 2010

    Ahsante Mdengereko wa Ukerewe, maana wabongo wengine hawasemi wapo nchi gani baada ya kuilipia wanaiona hiyo ITV kupitia www.TV4Africa.com!?!?

    Maana unaweza kuwa nchi zingine ikawa taabu kuiona kama Iran na China.

    Mdau
    Muscat.Oman

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 16, 2010

    nami nilipata dezo kwa siku 5 , nikalipia euro5.88, kwa sasa naangalia bila matatizo na ni clear

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 16, 2010

    Kama unataka lipia uendelee kuona,inabidi kwanza card yako ya benki uwe umeiandikisha www.paypal.com (hii ni site ya kuaminika kwa malipo ya card kwani inakuhakikishia usalama wako kuwa hutahitaji kutoa information za kadi yako mara kwa mara). Ukishamaliza kujiandikisha Paypal ukibonyeza pale donate itakuunga na Paypal account yako then uta-transfer hizo pesa kwenda kwa hao jamaa. Hapohapo wanakuletea username na password kwenye page na pia kwenye mail yako. Usiogope si matapeli wala nini. Tuliolipia tunaendelea kufaidi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 16, 2010

    Hata hapa Inyonga imepigwa kufuli! Itabidi niende Mpanda kulipia!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 16, 2010

    jamani mliolipia tupeni nasisi user name na password moja akilipa inatosha!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 16, 2010

    Mimi niko USA naipata bila chenga wala nini baada ya kulipa dola 7.
    Kama niko nyumbani vilee..

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 16, 2010

    "paypal bonyeza then utaweza lipia nakupata username+password"please clik here to donate you will receive your login data immediatly after the donation.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 17, 2010

    Hii kitu isingetangazwa hapa tungeona kwa bure kwa muda mrefu sana. Mmetupotezea uhondo. Mara ilipotangazwa hapa kwa ankal michuzi basi watu wakaenda kama jeshi la siafu kuangalia. Naona wenyewe wakashangaa hawa watu wote wametokea wapi kuangalia hii ITV. Wakajua kuna ulaji hapo...ndio maana wakablock..Mpaka sasa zile nchi zingine ambazo nazo zilikua free bado zipo free.....


    Ankal inabidi watu wakitangaza hapa wakulipe....Matangazo yako yanafika masafa ya mbali na wenye kutangaza wananufaika sana

    ReplyDelete
  23. Sijaiona hiyo East Africa TV bado, ila wangetuwekea hapo TBC kazi ingekua imekwisha, tungejihisi tupo nyumbani kabisa. Kwa wale ambao wanadaiwa username na password, mwendo hapo donate hiyo Euro 5 unatumia hizo details muda huo huo.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 17, 2010

    Mdau tunaelewa wewe ndiye unaye post hizo comments everytime urging people to pay 5 euro n or 7 dollar but ur style of doing is annoying...u read a comment n then u go back n oooh pay 5 euro hata mimi nilikuwa napata bure yari yari yari...its disgusting is like u begging just sit back realx ume -introduce hiyo kitu wache watu waone ubora wako watanunua..AAAAAGHHH!!!

    ReplyDelete
  25. Kwa mdau unaesema huoni EATv nadhani ulitakiwa tuu ku refresh hiyo player ungeiona. Nimejaribu kuwaandikia hao jamaa kuhusu TBC wakasema wanaiweka, hata hivyo wana USB dongle ambayo nayo wanauza euro 20. Ila kwa sie tuliolipia kwa kweli utadhani tupo bongo vile..!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...