Warembo wa Miss Dar Inter College wakifanya mazoezi club billicanas
Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari waliofika leo katika Hoteli ya Movenpic wakati wa akitangaza udhamini wake wa Mil. 12 kwa ajili ya shindano la Miss Dar Inter College.kushoto ni Mratibu wa shindano hilo,Silas Michael.
Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos akikabidhi Hundi yenye Thamani ya shilingi Mil. 12 kwa Mratibu wa Shindano la Miss Dar Inter College,Silas Michael huku warembo washiriki wakishuhudiaa.
Mdhamini akiwa na Warembo katika picha ya pamoja.
warembo wakijisevia msosi
warembo wakijichana.

KAMPUNI ya RBP & INDUSTRIAL TECHNOLOGY TANZANIA LIMITED ya jijini Dar es Salaam leo imetangaza kudhamini shindano la Miss Dar Inter College na imeweza kutoa kiasi cha shilingi milioni 12 kwa ajili ya zawadi za warembo wanaowania taji hilo litakalofanyika May 27 kwenye klabu ya kimataifa ya Bilicanas jijini Dar es Salaam.

Warembo watakaoshiriki shindano hilo ni kutoka vyuo vya mbali mbali vya elimu ya juu vya jijini Dar vikiwemo CBE, IFM, DSJ, TSJ, ISW.

Akiongea na Waandishi wa habari waliofika katika mkutano uliofanyika leo katika Hoteli ya Movenpic,Rais wa Kampuni hiyo ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY TANZANIA LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos alisema.”

Kampuni yangu ya RBP ni ya kizalendo na imeona vyema kuwasaidia warembo hawa ambao ni wasomi na pia ni taifa la kesho na ambao wataweza kuleta maendeleo katika nchi yetu kupitia fani hiyo ya urembo”.

Aliendelea kusema “Ninawapa msaada huu Warembo hawa kama wanangu na hivyo kama Mama ninaejali familia na watoto kwa ujumla nimeona leo niweze kuwasaidia katika kufanikisha kupatikana kwa zawadi zitakazoweza kuwanufahisha maishani mwao.”

Msaada huo ni mwendelezo tu wa kusaidia na kuinua vipaji vya wasichana hapa nchini ambapo juzi tu Mdhamini huyo aliweza kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa timu ya taifa ya wanawake ‘TWIGA STARS’ ambayo inajiandaa na kucheza michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake.

Twiga itacheza na timu ya taifa ya Elitrea May 23 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo unaotazamiwa kuwa na upinzani mkali.

Kwakumalizia Mama Al Kharoos aliwahusia warembo hao kwa kuwataka waepukane na vishawishi na mambo yasiyofaa katika Jamii pia wawe na tabia njema waapo majumbani mwao. Kwani kujiheshimu kwao ndiko kutakapo wapatia heshima katika sehemu yoyote ile watakayokuwepo.

RAHMA AL KHAROOS
Rais – RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2010

    Ankal picha za jana diamond jubilee vipi?au jana kwa sababu ilikuwa kiingilio 15,000/= hukuweza kwenda? Nakutania tu ankal najua mambo yako safi huwezi kosa 15000.

    Turushie nasi tuliopo ughaibuni tuweze kujua kilichojiri.

    Mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2010

    Ankal, tunasubiri na wewe uanzishe Miss Globu ya Jamii, maana umebakia wewe tu, wadau wako hatuelewi unasubiri nini bado kuanzisha mashindano hayo. Tupo tayari kujitolea kwa hali na mali. Tutachangisha harambee. Anzisha basi hilo shindano.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 16, 2010

    Ankal, Mimi natoka kidogo nje ya mada, ninakuja na haka ka-mada kadogo ambacho nimekaona kule mtaa wa pili kwa watani zako wa jadi (Jamii Forum).

    Labda L'alliance Franc,aise watatusaidia zaidi, lakini wana JF wao badala ya kusema P. D. G ama kama inavyotamkwa na wenyewe wenye lugha yao, Peh Deh Geeh, wao wanasema Preshedee ama kitu kama hicho.

    Ninavyoelewa mimi, P. D. G (Peh Deh Geeh) maana yake ni Directeur Presidant General, yaani President Directer General, ama kitu kama hicho, ikimaanisha Top Boss, in sor far as uendehsaji wa Makampuni unahusika. P.D.G ni watu kama akina Ma-C. E.O, Ma-Managing Director na Ma-Executive Director.

    Pia, P.D.G kwa maana isiyo rasmi, hutumika pia kumaanisha mtu mwenye pesa pesa, ama mtu anayejulikana, au kitu kama hicho.

    Nimeona niongelee, japo sina uhakika kama hapa ndipo mahala pake. Ila nadhani itasaidia wanajamii.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2010

    Hii mambo ya kutupa hela huku ni wanafunzi wangapi wangesomeshwa au ni nyumba bora ngapi zingejegwa na watu kupangishwa kwa kulipa kodi ndogo?

    Let try to be creative and think out of the box.Kidogo kidogo tungebadili mazingira ya nchi yetu. na the more unawasaidia watu the more wangetajirika na kujinyanyua na kukunua magari au kusafiri sana na kufanya mafuta yenu yanunuliwe kwa wingi...

    Mambo ya mamiss bongo sasa hivi imekua hata haina maana tena....

    Kaka michuzi usitupe maoni yangu kwenye kapu kwa vile tunataka kuwasaidia wenye hela zao kujua kuwa kuna vitu vingi tu vya kufanya Tanzania zaidi ya mamiss na kwend achina kununua nguo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2010

    .... safari bado ni ndefu ya kuwafunda hawa mabinti zetu .. mashindano ya urembo siyo kupita mbele with sexiest appearance tu bali hata table manners wakati wa kula ... hapa tayari walioweka mabegi yao juu ya meza ni knock out /disqualify ... huwezi kula na begi lipo juu ya meza.. huwezi kula na mkono mmoja umeegemea kwenye meza mfano huyo dada wa kwanza kulia ..ndio maana mabinti zetu wanakuwa wasindikizaji siku zoote ...
    Mdau
    Japan

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2010

    we mdau wa Japan usifananishe Tanzania na huko kwenu,sisi tumezoea kuweka mabegi mezani wakati wa kula kwa sababu ya wizi,acha begi chini ukione chamoto,kuanzia simu mpaka poda watu wanaiba,
    Kula na mkono mmoja tumejizoelea Ugali wetu wa kila siku,wali usiku,maanjumati ambayo mpaka siku ya harusi ndo nakula,yatanizoesha vipi kula na mikono miwili?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 17, 2010

    P. D. G [Peh Deh Geeh (Djee)] maana yake ni Président Directeur Général, na sio Directeur Président Général, kama nilivyoelezea hapo mwanzo (mpangilio wa tafsiri), ila maana yake ni ile ile, President Director General ama Top Boss. L'alliance Française watanisaidia zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...