Barabara ya Old Bagamoyo road itayotumika na wadau wa mbezi, mikocheni, kawe, Msasani wakati wa mfungo. Wanaombwa wajihadhari wanapokaribia kituo cha Kwa Warioba kwani kuna maji ya chooni yamezagaa barabara yote kutokana na mtaro kuziba. hivyo kuna rojo rojo la uding'aa kibao barabarani.....hapo harufu hatujaitaja.
barabara ya ali hassan mwinyi road ambayo itafungwa kesho kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tatu. na jioni kuanzia saa tisa hadi saa moja.

Barabara ya Morogoro road ndiyo itatumika wakati ya Ali Hassan Mwinyi road

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. William Lukuvi, amesema kwamba barabara zitazofungwa kupisha viongozi na wajumbe wa mkutano wa Uchumi unaoanza kesho ukumbi wa Mlimani City jijini Dar hazitafungwa moja kwa moja isipokuwa katika muda maalumu.

Amesema pia hata wakati wa msafara, magari ya dharura yakiwamo ya zimamoto na ya wagonjwa yataruhusiwa kupita, pamoja na magari ya wanafunzi na wafanyakazi yataruhusiwa kupita wakati utakapopatikana upenyo.

Amesema barabara hizo zitaanza kufungwa kuanzia leo hadi Jumamosi; mkutano utakapofungwa na kwamba zitakuwa zinafungwa na kufunguliwa mpaka mkutano umalizike.

Barabara zitakazofungwa ni ya Nyerere kutoka Uwanja wa Ndege hadi katikati ya Jiji ambayo itatumiwa na wageni wanaokuja kuhudhuria mkutano huo unaofunguliwa rasmi kesho.

Kesho hadi Ijumaa, kuanzia saa moja mpaka saa tatu asubuhi, barabara ya Ali Hassan Mwinyi itatumika kusafirisha wageni kwenda kwenye kumbi za mikutano zilizopo kando ya barabara ya Sam Nujoma. Mh. Lukuvi kasema barabara hizo zitafungwa kutokana na wageni wengi kulala katika hoteli zilizo katikati ya Jiji na kwamba baadaye zitafunguliwa kwa matumizi ya kawaida.

Itakapofika saa 9 alasiri, barabra hizo zitafungwa tena hadi saa moja usiku kwa ajili ya washiriki wa mkutano kurudi katika hoteli walizofikia.

Ndio kusema wakaazi wa Sinza, Kijitonyama, Mwenge na wote wanaotumia barabara ya Ali Hassan Mwinyi, itabidi watumie barabara ya Morogoro huku wakazi wa Mbezi, Mikocheni, Kawe, Msasani watakuwa wakipita barabara ya Old Bagamoyo ili kuepuka usumbufu.

Aidha, wananchi wanaopata huduma katika maduka ya Mlimani City wameshauriwa kutumia barabara ya Chuo Kikuu cha Ardhi, kwani barabara ya Sam Nujoma, itakuwa ikitumika kwa shughuli za mkutano huo.

Maduka hayo, pamoja na 'Samaki Samaki', hayatofungwa katika kipindi cha mkutano huo, hivyo wadau wa maeoeno hayo msikonde wala nini....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2010

    Ingekuwa ni muda muafaka wa kuchukua likizo au kufanya safari za kikazi nje ya dar ili kukwepa foleni....NINGELIJUA...NINGE....
    duh balaa hili sijui itakuaje hadi jumamosi!!! visingizio kibao hapo, kila mtu ata-take advantage ya foleni kuleta uongo na excuse zake...mfano: DUH NIMESHINDWA KWENDA BENKI, FOLENI KIBAO!! au NIKO KWENYE FOLENI HAPA FIRE , LAKINI NAKUJA NITACHELEWA KIDOGO!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2010

    This WEF will just cost taxpayers' money and for the duration the same taxpayers will be seriously restricted in their daily activieties! I do not see any benefit for DAR or even TZ! The people should demanostrate against that WEF!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2010

    Ankal naomba kuuliza,hii barabara ya sam nujoma inafungwa siku nzima option imetolewa kwa wanaoenda mlimani city je kwa tunaofanya kazi jengo la mawasiliano tutafanyaje! naomba tuulizie hilo tafadhali!

    ReplyDelete
  4. TEH TEH TEH TEH! Kunya anye kuku akinya Bata kaarisha. Haya bwana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2010

    MKUTANO WA UCHUMI NI MUHIMU SAANA

    Mdau 09.38 AM
    mtazamo wako hautosaidia katika kuleta maendeleo ya uchumi ambayo nchi zote ulimwenguni zinajaribu kufanya jitihada zote kupitia katika vikao kama kinachotarajiwa kufanyika Tanzania.
    Kufungwa kwa baadhi ya barabara wakati wa mikutano mikubwa kama huu ni kawaida ya nchi zote hata zile zilizoendelea kama USA,EC na Scandnivien kwa usalama wa viongozi wawakilishi wa nchi mbali mbali katika mikutano.
    walipa kodi wa Tanzania wana uhuru wakati wowote kufanya maandamano kama kuna swala linalokwenda kinyume na matumizi ya pesa za kodi hata kama haitowafurahisha wachache wa ngazi za juu,hakuna kiongozi yeyote amabye anaweza kupinga swala hilo la uhuru wa walipa kodi kupitia vyama vya wafanya kazi au hata vyama vya siasa tofauti nchini lakini kuwepo na sababu muhimu za kufanyika maanadamano kuepukana na kuutumia uhuru vibaya.
    Mikutano ya uchumi ni muhimu hata kama haitoleta matokeo ya haraka, inatupa mwanzo wa kufikia mwisho wa matatizo ya uchumi Tanzania na bara zima la afrika.

    Mickey Jones
    Denmark

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2010

    Barabara ya OLD BAGAMOYO ROAD solution yake ni ndogo sana na wala haitahitaji ujenzi wa FLYOVERS.

    Foleni yote ya barabara hii inatokana na sehemu ndogo ya kutoka pale Carnivore Pub mpaka njia panda ya kuenda JWTZ Golf Club. Dawa yake ni;

    1. Manispaa irekebishe drainage inayopokea maji kutoka Coca Cola Road na kuyamuaga mto Lugalo.

    2. Manispaa irekebishe lami ilipoharibika KWA KIWANGO CHA LAMI.

    3. JKT (wenye madaraja) waondoe Matuta mbele ya madaraja yale mawili. Hakuna atayeyagonga.

    4. Pale makutano ya barabara ya JWTZ Golf Club pana manhole ya DAWASCO ambayo inazaa Pothole kubwa lisilopona kamwe. DAWASCO warekebishe.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2010

    kweli kuongoza nchi iliyojaa mafara ni raha kamili.......WAMENYAMAZA KIMYAAA.....wao kila kitu mkwao mswano.......DSM ina barabara MBILI na zote zimefungwa....BADO MMESHANGAA TUU......INGETANGAZWA HOLIDAY basi.....

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2010

    HIYO BARABARA YA OLD BAGAMOYO ROAD SEHEMU YANAPOTOKEA MAJI MACHAFU KUNA KAHARUFU KA RUSHWA!!!!!

    AWALI,YALE MAJI MACHAFU YALIKUWA YANATOKEA KWENYE MTARO UNAOELEKEA BAHARINI SEHEMU HIYOHIYO.
    HALMASHAURI WAMEZIBA MTARO HUO UNAOENDA BAHARINI INAELEKEA KWA "KITU KIDOGO" HALAFU WAMEELEKEZA MAJI MACHAFU KWENDA KILOMETA NZIMA KWENDA MTO MLALAKUWA KATIKA KAMTARO AMBAKO HAKA KINA WALA MTEREMKO(SLOPE).
    HIVYO, UCHAFU HAUENDI KWA SABABU YA "KITU KIDOGO" YA WATU WA HALMASHAURI(SIJUI KAMA MEYA YUMO AU VIPI)

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2010

    Naamini kungelikuwepo na solution bora zaidi kama vile kufunga saa moja barabara hizo saa moja kabla ya wajumbe kuanza kuhudhuria na kuzingunga tena saa moja kabla ya wajumbe kuondoka mkutanoni.

    ReplyDelete
  10. Mikausho MikaliMay 04, 2010

    Ankal,hawa watu wangekuwa wabunifu tu.huu mkutano ungefanyika ijumaa mpaka jumapili kwa hiyo mikogo yao ya kufunga barabara.tena ijumaa wangefanya tu public holiday basi kama wenzetu uganda walivyofanya.kwani haya mambo ya kutumia sijui old bagamoyo manake unapita old bagamoyo,ubalozi wa marekani,unazunguka mitaa ya oysterbay ukifika salender unakwama.wakazi wa sinza wataitafuta old bagamoyo kivipi ?inamaana watakuwa wanaruhusiwa ku cross njia ya RG ,Coca cola,na victoria ili kwenda kuitafuta hiyo old bagamoyo.mbona itakuwa balaa hizo siku 3!wakubwa wajifunze kuwa wabunifu au watafute ushauri.kuna watu wengi tu wazuri wa logistics hapa mjini

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 04, 2010

    MIKUMBI YA MIKUTANO JENGENI NJE YA MIJI UBISHI TU, SASANDIO MATOKEO YAKE

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 05, 2010

    BONGO SIRUDI NG'O NA VILE VIJIMAWAZO NILIVYO KUWA NAVYO NAVIFUTILIA MBALI KUDADADEKI!!!!!!!!!

    KHA!, CHEKI FOLENI, CHEKI MAZINGIRA MABOVU, CHEKI SERIKALI INAGOMA KUONGEZA MISHAHARA!!!!!!! KHA! MI SIWEZI HIZI ISSUES NGOJA NIWAACHIE MAFISADI. UTADHANI TUKO KARNE YA 2 HII KITU NOMA!

    KWA MAHESABU YA FASTA FASTA KAMA MPANGILIO NDIO HUU, NITAKUFA, WATOTO WANGU WATAKUFA, VIZAZI VYA WAJUKUU NA VITUKUU VYANGU VITAKUFA NA KIPINDO HICHO NDIO TUTAKUWA TUMEFIKIA KIDOOOOOOOGO MAENDELEO YA SOUTH AFRICA!!!!!!!!!

    KENT, ENGLAND

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 05, 2010

    We mjamaa wa Kent(05:26:00) una matatizo ya kimsingi.Beba maboksi yako na nina uhakika huko uliko uko ghetto na maisha ya kijungujiko.
    Sasa kama hurudi bongo nani anajali? we kula kuku wako na bata sie libeneke kwa kwenda mbele,matatizo nayo yanachangamoto zake.
    Tatizo mtu akiishi kidogo tu huko majuu anafikiri yuko peponi.Mtu kama wewe usipoona opportunities za bongo mtaishia kula chakula cha makopo cha makemikali kibao, mapresha ma ,makansa ndo kwao.
    Pamoja na shida za bongo utamu wake twaujua sisi.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 05, 2010

    Mnajua waTZ ni watu wapole sana si mafala kama msemaji alivyotaja hapo juu. Na bughudha hii watz walio nayo imeletwa na sisi tunaotaka "ISLAMIC BANKING" vinginevyo hapa ni tambarare. Hawa wa IS vurugu ni jadi yao, kuua ni kikolezo cha u IS. kwa hiyo hii ndio hali. hawa watu waombewe ili imani yao ifundishe kumjua Mungu NA kuacha naovu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...