Bwana Issa Michuzi habari yako,
Naomba uianike hii kero hapa katika Globu ya Jamii ili wadau waweze kuleta maoni yao.
Inakera sana kusikia walemavu wanavyolalama kuhusu majengo na miundo mbinu iliyopo nchini ambayo haizingatii hali zao.
Inabidi wadau tuungane kushinikiza serikali kupitisha michoro ile tu inayowajali walemavu. Hata Airpoti utaona hawaweki vifaa/vigari vya kuwarahisishia walemavu. Makanisa na Misikiti nayo. Juzi tu nimehudhuria misa kanisa la KKKT pale Kotela, Mamba.
Lina ngazi mlima zaidi ya thelathini. Huko NMB tumeambiwa nako ni tatizo. Ingia majengo ya DSM ni tatizo tupu. Hata majengo ya karibuni hayajasanifiwa kujali walemavu. Imekuwaje yamepitishwa??.
Wizara husika mpo hapo??Nashauri NGOs pamoja na serikali zifanye jitihada kuwafunza architects/ building designers kuhusu michoro inayokubalika kwa walemavu wote.
Nashangaa Manisipaa na serikali zinapitidha michoro hiyo bado. Nilifurahishwa sana na majengo na miundo mbinu ya Mzumbe University jinsi inavuojali walemavu. Au ni kwa kuwa misaada ilitoka Norway/NORAD?.
Watanzania tubadilike, miaka 50+ ya uhuru sasa. Nawashauri wanaosanifu majengo ya umma waende Mzumbe wakajifunzi kwa kuona.
mdau
Richard Mazingira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2010

    yani mt wg umeongea kitu cha maana sana kwani sidhani hata km hao wachoraji wa ramani za majengo km wamesoma!!i hope vyombo husika vitafuatilia swala hili!! inabidi tuwakumbuke na walemavu sio tunajijengea tu magorofa bila mpango!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2010

    Kanisa la Yesu Kristo La watakatifu wa Siku za Mwisho Pale Kinondoni Morroco ni mfano mzuri wa jinsi jengo linavyojali walemavu kwa kuweka mifumo inayowajali(Support). Kuna ngazi za walemavu, vyoo vya walemavu na access nzuri za walemavu.
    Nendeni mpige picha

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2010

    Naomba nitoe mfano katika jengo la JM Mall (Habour Vew)
    Mwanzoni kulikuwa na ngazi za walemavu katia korido ya mbele ya jengo. baada ya ukarabati wao na kuweka maru maru ikaondolewa na kuweka ngazi. Kweli michoro lazima ihusishe njia za walemavu. wahusika wazingatie.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2010

    me ata sielewi izi wizara na mawaziri wake wanafanya nini

    unajua ngoja mtu limpate asa viongozi ndo watakulupuka kuweka iyo miundo-mbinu

    dhambi hii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...