Fainali ya mashindano ya Kili Taifa Cup 2010 itapigwa kesho katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Lindi itamenyana na Singida.
Fainali ya mwaka huu imezua msisimuko mkubwa kwani timu zote mbili ni za mkoani tofauti na miaka ya nyuma.
Ilala, ambao walikuwa mabingwa wa mwaka jana, ndio timu pekee kutoka Dar es Salaam iliofanikiwa kutinga Nusu Fainali.
Mechi ya kesho inatarajiwa kuanza saa tisa alasiri na kabla ya hapo kutakuwa na burudani kutoka kwa vikundi mbalimbali ikiwemo Bendi ya African Stars, Twanga Pepeta, vikundi vya sarakasi na ngoma za kitamaduni.
“Mashindano ya mwaka huu ni ya kipekee kwani timu zote mbili zilizotinga fanali ni za mikoani. Hii inadhihirisha kuwa mpira unakuwa na kuna vipaji mikoani ambavyo vinatakiwa kunaswa na kutumika ipasavyo. Ni matumaini yetu kuwa makocha mbalimbali wamekuwa wakifuatilia mashindano haya na watawasajili vijana walioonyesha soka ya hai ya juu,” anasema George Kavishe, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager.
Mwaka huu bingwa wa Kili Taifa Cup atapokea kitita cha Tsh milioni 35,
mshindi wa pili - 20m, mshindi wa tatu - 10m, mshindi wa nne - 5m, kipa bora - 2m, kocha bora - 2m, refa bora - 2m, mchezaji bora - 2m, timu yenye nidhamu ya hali ya juu - 2m na mfungaji bora - 2m zote kwa hisani ya Kilimanjaro Premium Lager.
TFF imekuwa ikitangaza mchezaji bora katika kila mechi na mshindi kupokea Tsh 50,000.baada ya mechi.
Kilimanjaro Premium Lage inaendesha promosheni katika mikoa ya Lindi na Singida ili kuhakikisha wakazi wa maeneo hayo wanajotokeza kwa wingi kushangilia au kuangalia timu zao zikicheza kesho.
Hii ni mara ya pili kwa Kilimanjaro Premium Lager kufadhili Kombe la Taifa, ila ni mara ya nne mfululizo kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kufanya hivyo. Miaka miwili ya mwanzo ikiwa chini ya bia yake nyingine ya Safari Larger, ambayo ni mojawapo ya bia maarufu za TBL.
Nawatakia Lindi ushindi....Ilulu Oyee
ReplyDelete