KAIMU KATIBU MKUU WA TUCTA MH. NICHOLAS ERNEST MGAYA WAKATI WA KUTOA YAMKO LA KUSITISHA MGOMO JANA JIJINI DAR. KWA MUJIBU WA GADNA G. HABASH MH. MGAYA HAKUTOKEA LEO KUPANDA KATIKA KIPINDI CHA JIONI CHA JAHAZI KAMA ALIVYOAHIDI. HIVYO CLOUDS FM INAWATAKA RADHI WADAU KWA HILO KUTOKUWA ILA JUHUDI ZINAENDELEA KUFANYWA VIONGOZI WA TUCTA WAENDE KUPANDA JAHAZI NA HATIMAYE KUBALANSI MAMBO.....


Hongera Mgaya kwa uamuzi mzuri wa kukataa kutokea. Akina Kibonde ndio hao hao. Halafu lengo la wafanyakazi siyo kuonyeshana nani zaidi na JK bali ni kudai maisha mazuri kwa kila mtanzania.
ReplyDeleteHakuna haji ya kushindana na kiongozi wa nchi.
...Mgaya anabusara sana...hakuna haja ya kudebate kwa sasa...
ReplyDeleteNgoja Mbayuwayu uoga umuishe akishakuwa Kong'ota ndo patakuwa hapatoshi.
Kambayuwayu ka Kikwete kalikokataa kuwa tetere
ReplyDeleteM. M. Mwanakijiji
NILISIMULIA kisa cha mbayuwayu ambaye alikuwa anaishi katika shamba la mkulima mmoja huko Ukwereni.
Mbayuwayu huyo aliishi na wenzake katika maisha ya kutegemea nafaka na mbegu mbalimbali zinazopatikana katika shamba la mkulima huyo.
Pamoja naye walikuwepo ndege wengine wengi ambao nao walipata afueni ya maisha yao katika shamba hilo zuri la Mkwere. Miongoni mwa ndege hao walikuwapo tetere ambao walionekana kama ndio ndege wapendwa wa mwenye shamba.
Mkulima huyo alikuwa anahakikisha kuwa tetere wanakula na kunenepa pamoja na ndege wengine kama vile kwale na kukumaji. Na walikuwepo pia dudumizi, vigong'ota, zokoyogo na kurumbiza. Ndege wengine wote hawa walifurahia maisha yao katika shamba la Mkwere isipokuwa mbayuwayu.
Mbayuwayu alikuwa analalamika mara kwa mara kuwa masilahi yake hayaangaliwi na kulindwa kama ya kina tetere.
Mara kwa mara mbayuwayu amejikuta akijitafutia riziki yake hata nje ya shamba, amekuwa akikwepa mitego yeye mwenyewe na hata anapowindwa na paka ilimbidi atafute mbinu endelevu za kujilinda.
Katika maisha hayo mbayuwayu alijikuta anaishi maisha ya ‘kiujanja ujanja’ ilimradi mdomo uende kinywani.
Mbayuwayu walikuwa wanalalamika kuwa tetere walikuwa wameachwa kula kwa uhuru wote na wamefikia kula hata vile vidogo vya mbayuwayu.
Walilalamika kuwa hata wakiona kuna punje zimedondoka ilikuwa ni vigumu, kwani tetere walifika mara moja na kwa kutumia mabavu waliweza hata kuwatimua mbayuwayu hao kwa kuwatishia kuwadonoa.
Kwa vile waliona kuwa masilahi yao na maisha yao yanatishiwa na tetere na mwenye shamba inaonekana hawajali, basi mbayuwayu kwa kutumia Umoja wao wa Mbayuwayu (UMBA), waliamua kuitisha mgomo wakidai masilahi zaidi na nafasi zaidi za kutambuliwa na mwenye shamba na kupewa masilahi ambayo yanakaribiana na yale ya tetere.
Tetere waliachwa kunawiri, na hata kujengewa matundu ya kisasa ili wao na makinda yao waishi maisha ya raha na amani wakati mbayuwayu wakiachwa kujijengea viota vyao kwenye kona za nyumba na majengo mbalimbali humo shambani. Tetere walikuwa wanaruhusiwa kukaa pamoja na kuimba kwa pamoja huku wakitamba kwa mwenye shamba kuwa:
Kuku mfupa mtupu
Mimi nyama tupu!
Hivyo mbayuwayu wakaamua kutangaza mgomo ili kumshinikiza mwenye shamba kuangalia masIlahi yao. Zikiwa zimebakia siku chache za mgomo kufika, mbayuwayu walijikuta wameweza kuwashawishi mbayuwayu wa jamii tofauti kuweza kushiriki mgomo huo na kwa pamoja wakaanza kutangaza juu ya ujio wa mgomo wa mbayuwayu wote shambani.
Na hata siku ya sherehe ya ndege wote wafanyao kazi zilipofika mbayuwayu waliandamana wakiwa na mabango yaliyosomeka:
Mwenye shamba tukumbuke
Mbayuwayu na sisi tuna haki
Kwanini tetere peke yao?
Walipita siku hiyo kwa umoja mkubwa japo mwenye shamba na yeye aliamua kufanya sherehe ya ndege wengine, ambapo tetere, dudumizi, kurumbiza na wenzake walihudhuria kwa furaha wakiburudishwa na miziki mbalimbali.
Katika sherehe ya mbayuwayu msimamo uliendelea kutolewa kuwa ni lazima wagome, kwani japo wao ni vindege vidogo na ambavyo vinaonekana havina maana ukilinganisha na mbayuwayu, lakini vina sehemu katika maisha ya shamba, kwani ndivyo vinatafuna vijidudu vidogovidogo vya hatari, huchangamsha ndege wengine na husaidia sana katika kuhakikisha usalama wa shamba, kwani vina uwezo wa kwenda sehemu mbalimbali hata zilizo ndogo na vina mwendo kasi sana kuweza kuwakwepa adui.
Hata hivyo, mwenye shamba alikasirika alipoona kuwa mbayuwayu kweli wamedhamiria kuitisha mgomo. Zikiwa zimebakia saa chache kabla ya mgomo huo mkubwa kuanza, mwenye shamba akaitisha mkutano wa ndege wazee na kuanza kuwahutubia kwa ukali, akielezea ni kwanini mbayuwayu hawastahili maisha ya tetere!
Akizungumza kwa ukali na akifoka hadi mapovu yakimtoka mdomoni, mwenye shamba aliwaambia mbayuwayu kuwa yeyote atakayegoma atakiona cha moto kwani wawindaji wote wameruhusiwa kutumia bunduki, manati na hata mizinga ili kuhakikisha kuwa mbayuwayu hawaleti madhara katika shamba kwa kugoma kwao.
!
Afadhali hakutokea kwani kuhojiwa na hao itasaidia nini kwa sasa. Wasubiri tuu mpaka baada ya tarehe 8 baada ya kile kikao.
ReplyDeleteSafi sana..
Tunaelewa ndugu yetu Mgaya..Rais sera hana anaamua kuwa mtemi na anavunja sheria. Anaingilia uhuru wa Mahakama, anasema uongo(Barua imeonyesha) na ameamua kuwa mbabe sababu hoja hana.
ReplyDeleteMzawa
DUH, HIVI HAWA NI WANAHABARI JANA HAWAJUI JANA KULIKUWA NA NINI? MR.MGAYA ALIKUWA KWENYE SHUGHULI YA KUMUAGA NGULI MWINGINE KATIKA MAMBO YA WAFANYAKAZI MAREHEMU BRONO MPANGALA, NA CHA KUSHANGAZA HAKUNA CHOMBO CHOCHOTE CHA HABARI KILICHO TO TAARIFA JUU YA KIFO CHAKE, KWA WENYE KUMBUKUMBU MZEE HUYU NDIOE ALIENDESHA MGOMO WA MWAKA 1994, MUNGO ALIZA ROHO YAKE MAHARA PEMA......., EBU MR. MGAYA RUDISHENI GAZETI LETU LA MFANYAKAZIIIIIIIIIIII
ReplyDeleteMDAU
VIJEMBE VILIVYOKUWA VIKITOLEWA NA KINA KIBONDE VILIKUWA TOSHA KUENDESHA KIPINDI KWANI WAO WALICHUKULIA KUWA NI MGOGORO KATI YA CCM NA TUCTA NA CCM KIBUKA MSHINDI, HAO NDIYO AKINA KIBONDE MAKADA WA CCM NDANI YA CLOUDS FM KWA MUJIBU WAO WENYEWE NA TAYARI WALIKUWA WAMEKWISHA MHUKUMU.
ReplyDeletesafi sana bwana Mgaya. kwa sasa unahitaji kutulia. na kama ni mahojiano nakubaliana na mdau aliyepta mtafute Jeneral Ulimwengu , au vijana wa mlimani tv. au hata melin hassan wa tbc wanajua kazi ya habari na ndiyo shughuri yao.namkumbuka Kibonde alianza kutangaza clouds fm ,katika kipingi cha michezo alikuwa na rick abdara. rick alikuwa anafanya uchambuzi wa club bingwa ulaya. rick alipoacha kibonde akachua nafasi.
ReplyDeletegadna na kibonde ni wanajua uzaifu wa jk, wanajua kwamba wakipiga debe anaweza wapa nafasi .siwezi kushangaa kuja sikia kibonde kachanguliwa afisa habari wa ikulu
KWA WALE WASIOMJUA KIBONDE, NI KADA WA CCM NA HAYO AMEKUWA AKIYASEMA YEYE MWENYEWE KWA KUJIAMINI NA KUWA ALIKUWA WA MWANZO KUICHANGIA CCM PESA NA HAYO ALIYASEMA MWENYEWE PIA ALIJISIFU KUPOKEA SHUKURANI KUTOKA KWA MWENYEKITI WA CCM, HUYU HANA SIFA ZA UANDISHI WA HABARI WA KUAMINIKA BALI NI MWANASIASA MPELELEZI HIVYO VYAMA VYA SIASA VISIJARIBU KUMKARIBISHA KWENYE MIKUTANO YAO. KAULI ZAKE KILA MARA NI ZA KUJA KILA JAMBO HATA KAMA HANA UHAKIKA NALO, MSIKILIZENI KWENYE KIPINDI CHA JAHAZI KIRUSHWACHO BAADA YA SAA KUMI NA NUSU ALASIRI MTAMJUA NI MTU WA AINA GANI. HATA HIVYO MIMI HUWA NASHINDWA KUIELEWE CLOUDS NI VIPI INARUHUSU MTANGAZAJI AITUMIE KUKISIFU CHAMA CHAKE KWENYE KIPINDI AMBACHO SI CHA KISIASA! NA MARA NYINGI HUVIPONDA VYAMA VINGINE KITENDO KINACHO MUONDOLEA SIFA YA UANDISHI KWANI ANAFANYA HIVYO AKIWA KAZINI NA SI NJE YA KAZI.
ReplyDeleteCLOUDS FM MARA NYINGI IMEKUWA IKITUMIWA NA WATANGAZAJI WAKE KUINADI CCM KWENYE VIPINDI AMBAVYO HAVIHUSIKI NA SIASA, KAMA HUO NDIYO MSIMAMO WA KITUO HICHO BASI SI MSIMAMO SAHIHI KWANI UTAKIONDOLEA SIFA KITUO HICHO LABDA TU KAMA NACHO KINAUNGANA NA KINA KIBONDE KWENYE USEMI WA SHAURI YAO HATA WAKIACHA KUISIKILIZA CLOUDS FM ITAENDELEA KURUSHA MATANGAZO YAKE.
ReplyDeletesafi Mgaya walikuwa wanataka kukupaka mafuta kwa mgongo wa chupa !!!!! afadhali uliwashutikia wanafki. juzi muongee pumba jana mumtake Mgaya aje . hamna haja ya samahani wenye uelewa tulielewa toka jana . hii itakuwa ni fundisho zuri kwenu.
ReplyDeleteCLOUDS FM NI REDIO KITUO CHA BURUDANI NA BIASHARA ZAIDI.WATANGAZAJI WAKE SIYO WANAZUONI MAHIRI NA MAKINI KATIKA TASNIA YA HABARI NA MAWASILIANO KWA UMMA.KITUO KIENDELEE KULINDA HESHIMA YAKE KWA JAMII KUPITIA BURUDANI NA SI VINGINEVYO.NI LAZIMA WAWE MAKINI KATIKA SHUGHULI ZAO NA WASIKUCHULIE KILA JAMBO NI BURUDANI KWA WANANCHI.KAMA WAO WAMEZOEA KUSHEREHESHA WENZAO WAMEZOEA KUTANGAZA.KAMA CLOUDS WANATAKA KUACHANA NA BURUDANI NA KUINGIA KWENYE ULINGO WA HABARI NA MATUKIO NI VEMA WATAFUTE WANAZUONI MAHIRI NA MAKINI KATIKA TASNIA HIYO NA SIYO WASHEREHESHAJI WA HABARI NA MATUKIO AMBAO KWAO BUSARA SIYO MTAJI MUHIMU.
ReplyDeleteKasoma nyakati,na ukizingatia mlishalikoroga wenyewe na kuhukumu jana yake tu,watu watakuwa wamemshauri akaamua kuwatosa na nyie kihuni vilevile.
ReplyDeleteHana haja ya kufafanua tena kwa sasa,labda mpaka baada ya mazungumzo ya tarehe 8
ReplyDeleteHuu ni wakati mzuri kwa tume ya mawasiliano na Idara ya habari-maelezo kufuatilia kwa karibuni zaidi utendaji wa vituo vya redio na televisheni nchini Tanzania ili kujiridhisha.Sina hakika sana iwapo vituo vyote vinazingatia maadili ya tasnia ya habari na utangazaji na iwapo watangazaji wake ni wanahabari wenye sifa na vyeti vilivyothibitishwa na mamlaka husika.
ReplyDeleteKwa mtu aliye serious kama Mgaya hawezi kuthubutu kuhojiwa na chombo cha kisanii kama Clouds, hapo wanafaa wasanii kwenda lakini si watu wa sifa maana ukienda pale hata kama utatoa point ya maana itaonekana ni entertainment tu badala ya kuwa serious issue, narudia kwa mtu serious kama Mgaya hawezi kwenda katika entertaiment media ataenda kwenye srious media.
ReplyDeleteHabash na Kibonde ni vibaraka wa Chama fulani na kwa hali hii wameishusha hadhi ya Clouds kwa Umbea wao. Namuunga mkono Mgaya kwa kutoenda kwa vikaragosi hawa. Kubwa ni kuwa tunakomaa zaidi kwa serikali kutotaka kujibu hoja zetu kwa wakati.
ReplyDeleteJamani huyo kibonde alishatangaza kuongezewa mshahara asilimia 100 na mwajiri wake, usitegemee akasupport jitihada za TUCTA kukomboa wafanyakazi wake. Yeye anapiga domo kwa kuwa analipwa vizuri ndio maana ana nguvu ya kupiga hilo domo lake kama la Respected Mkwere na makong'ota yake! Ama kweli alieshiba hamjui mwenye njaa. Kwa viongozi wetu wa TUCTA bado tuko nanyi, we support you guys, Mungu awatie nguvu na Inshallah tutashinda mapambano haya.
ReplyDeleteVizuri sana Mgaya. Kibonde na Garger hawana sifa za kutosha kujadili suala kama hili. Waachie wajadili habari zisizoaminika za magazeti ya udaku. We toka lini ukasikia mlinza by proffesional aanze kujadili suala linalohitaji ukomavu wa busara? Kumbuka tu lile suala ya msanii fulani katika zinduka. Jinsi kibonde alivyokuwa akishabikia kuwa msanii huyo ni mpumbavu hatukujua kabisa kuwa kumbe na yeye alishiriki kama MC katika tamasha hilo. Sasa naanza elewa kwa nini watu wengine wenye busara za kutoka wamekuwa wakikashifu Clouds FM na kuonyesha dhahiri kuwa inaweza kuwa na upungufu wa maadili. Haya bwana, sijui lini tunafika na hawa wanafiki!!
ReplyDeletewadau clouds FM, wanapoteza mwelekeo kabisa now. hizi mambo huwa zinagusa mambo ambayo ndo yanawafanya watu waendeshe familia zao katika kila sector ya maisha.
ReplyDeletesasa kwa watu kama wakina kibonde hasa wanaoendesha vipindi vya kutokutumia busara upeo mkubwa hawawezi wakachambua mada kama hizi.
Najua kibonde unapitia sana blog hii and unasoma comments zote upate chakupigia domo ili mkono uende kinywani. Tambua kuwa wewe upo hapo clouds not by professional ni kwa kipaji cha kuzaliwa na mazingira uliokulia TU!.
Kuna watu wanafanya kazi walizozisomea na walizo invest muda wao mwingi sana kuzisomea ndo hao wanaodai mishahara.
Sasa Sithani kama Hicho kipindi chako ni sehemu muafaka ya kujadili mambo kama haya.
Wewe tafuta mambo mengine yakuchekesha na kutoa salaam zako watu wacheke jioni giza liingie haya mambo hayafai kwa kipindi chako.
USITAKE KUCHEKESHA WALIONUNA.
Regards,
Mwalimu.
Hongera Mgaya kwa kutotokea kwenye kipindi cha porojo kwani sote tunajua Kuanzia kwa Ruge ambae ni Kada na Rafiki wa JK hadi kwa Makada wawili wa Jahazi
ReplyDeleteMgaya wewe ni kiongozi wa chama cha wafanyakazi sio mtoa porojo kama hawa Jahazi na wapenda Mteremko
Kwa sisi tunaifahamu familia ya mzee Samson Kibonde babake Ephraim tunasema Ephraim siyo mwanachama wala kada wa CCM ila kadanganyika na watoto wa mjini na kujiingiza kwenye tasnia ya siasa bila busara.
ReplyDeleteKIBONDE NA GADNER NI KAMA TUNAWAONEA TU,WAO WANABURUZWA TU NA RUGE HAWAJUI HATA KINACHOENDELEA,SASA MGAYA KUKAA MEZANI ETI AHOJIWE NA GADNA NI MATUSI,WAO WAMUALIKE "MWAJIRI MKUU" KWA KUWA NDIO MSIKILIZAJI WA HICHO KIPINDI CHAO,KWA KUWA "MWAJIRI MKUU' YEYE HUWA NI MPENZI HATA WA MAMBO YA HOVYO HOVYO KAMA ANAVYOPENDA KUJISEMEA MH.ZITTO KABWE,MUNGU AMJALIE APONE HARAKA HUKO ALIKO.HUYO KIBONDE KWANZA SIJUI HATA KAMA BABAKE KAPATA HELA ZAKE ZA EAST AFRICA COMMUNITY KAMA MFANYAKAZI WA BANDARI,
ReplyDeleteACHANENI NI KINA KIBONDE NA HUYO MWENZAKE HAO WAKO KATIKA KUNDI LILE AMBALO YEYE MWENYEWE "MWAJIRI MKUU" ALIWAHI KULISEMA LA WAFUATA MKUMBO,WATU DIZAINI HII NDIO WANAIFANYA NCHI HII ICHUKUE MUDA MREFU SANA KUPIGA HATUA,SITASHANGAA NIKISIKIA WANATANGAZA KUANDAA MAANDAMANO MAKUBWA YA WATU WA KUPANDIKIZA KUUNGA MKONO "HOTUBA YA KIHISTORIA" YA "MWAJIRI MKUU'.
ReplyDeleteKIBONDEEEE POLE KAKA, LAKINI SIKUPENDA NAMNA ULIVYOKUWA UKIMWONGELEA NAIBU KATIBU MKUU WA TUCTA. ULIKUWA UKIONGEA KISHABIKI MNO. DIZAINI KMA UDAKU HIVI. MKUBWA WA KAZI UWE NA KIPIMO NA PIA TAKE CARE USIJE UKAHARIBU SIFA ULIZOJIJENGEA KWA JAMIII.
ReplyDelete