Ankal, tunakushukuru sana kwa jitihada zako za kutuhabarisha kupitia
blogu yako maarufu. Hakika blogu yako imekuwa msaada mkubwa sana kwetu
Watanzania wa kada zote. Kaka ninalo tatizo kidogo naomba msaada wako
unifikishie kwa wadau wanipe ushauri.
Tatizo langu ni uso / ngozi ya uso kuwasha. Nimekuwa nikitumia
vipodozi tofauti tofauti kwa muda wa zaidi ya miaka tisa. Tatizo
lilianza taratibu tu kwa kubadilisha aina moja ya vipodozi na kuanza
kutumia aina nyingine kila baada ya aina ile ya awali kunisababishia
ngozi kuwasha. Niliendelea na utaratibu huo mpaka hatimaye nikaanza
kuona viupele vidogo vidogo vyenye maji. Hivi viupele vimeendelea
kuwapo kwa muda kama mwaka hivi. Nilijaribu kutumia sabuni ya kuzuia
kuwasha hali haikuweza kubadilika. Pia nimewahi kutumia aina tofauti
za scrub lakini bado hali haikuweza kubadilika.
Hatimaye nilichukua uamuzi wa kuacha kabisa kutumia vitu vyote yaani
vipodozi, sabuni na scrub. Kwa kipindi ambacho nimeacha kutumia bado
viupele vidogo vidogo vimeendelea kuwepo na saa zingine uso pia hupata
muwasho. Wadau naomba ushauri wenu ni vipi naweza kurekebisha hali
hii.
Mdau Jamila
blogu yako maarufu. Hakika blogu yako imekuwa msaada mkubwa sana kwetu
Watanzania wa kada zote. Kaka ninalo tatizo kidogo naomba msaada wako
unifikishie kwa wadau wanipe ushauri.
Tatizo langu ni uso / ngozi ya uso kuwasha. Nimekuwa nikitumia
vipodozi tofauti tofauti kwa muda wa zaidi ya miaka tisa. Tatizo
lilianza taratibu tu kwa kubadilisha aina moja ya vipodozi na kuanza
kutumia aina nyingine kila baada ya aina ile ya awali kunisababishia
ngozi kuwasha. Niliendelea na utaratibu huo mpaka hatimaye nikaanza
kuona viupele vidogo vidogo vyenye maji. Hivi viupele vimeendelea
kuwapo kwa muda kama mwaka hivi. Nilijaribu kutumia sabuni ya kuzuia
kuwasha hali haikuweza kubadilika. Pia nimewahi kutumia aina tofauti
za scrub lakini bado hali haikuweza kubadilika.
Hatimaye nilichukua uamuzi wa kuacha kabisa kutumia vitu vyote yaani
vipodozi, sabuni na scrub. Kwa kipindi ambacho nimeacha kutumia bado
viupele vidogo vidogo vimeendelea kuwepo na saa zingine uso pia hupata
muwasho. Wadau naomba ushauri wenu ni vipi naweza kurekebisha hali
hii.
Mdau Jamila
Ebo unatuuliza sisi si uende kwa Dr.Mtaalamu wa magonjwa ya ngozi akufanyie uchunguzi.
ReplyDeleteNenda kwa daktari wa ngozi, utapata ushauri wa kitaalam zaidi.
ReplyDeleteJARIBU KWENDA KWA DAKTARI BINGWA WA NGOZI KUPATA USHAURI
ReplyDeletematatizo ya ngozi hasa ya uso ni hatari sana nakushauri pata ushauri wa daktari si kila dawa au kipodozi atumiacho mtu kiwe na matokeo sawa kwa kila ngozi. please see physician
ReplyDeleteMdau Jamila.
ReplyDeleteNdugu jaribu kutumia white Petr jelly, mafuta ya nazi na vidonge vya vitamin C lakini kwa muda wa mwezi.
Tembelea ofisi za Angaza, magomeni mapipa,waelezee watakusikiliza
ReplyDeletekamuoane Dr manake hizo dalili za vipele mhh kapime na damu pia usitumie tena hizo cream
ReplyDeleteWewe ni mgonjwa.. kamuone daktari wa magonjwa ya ngozi vipodozi haviwezi kukusaidia kitu.
ReplyDeleteDada yangu,ukitaka tatizo hilo liondoke ningependekeza utumie kitunguu saumu. Twangwa kitunguu saumu mpaka kilainike. Osha uso wako kwa maji ya moto alafu subiri kama dakika tatu maji yakauke yenyewe. Hakikisha uso usiwe mkavu sana. Pakaza kitunguu saumu katika uso wako na uwache uji majimaji hayo ya kitunguu saumu yakauke. Utaona kwamba uso wako umekuwa na mask kama gundi. Baada ya nusu saa unaweza kwenda kuoga na safisha vizuri uso wako. Tafadhali usitumie sabuni za manukato. Ningekushauri tumia sabuni za kuogea watoto za baby Johnson. Sabuni hizi hazina kemikali. Fanya hivi kila jioni. Baada ya kuosha usifute na taulo, bali acha maji yakauke yenyewe. Ningekushauri utumie lotion nyepesi na iliyotengenezwa kwa ngozi sensitive. Hapa pia tafuta zile lotion za watoto
ReplyDeleteAthari za kitunguu saumu ni kwamba unaweza kunuka harufu ya kitunguu saumu. Hivyo nakushauri mavazi yako pulizia manukato mazuri ili kupunguza makali ya hiyo harufu (lakini si wakati wote unaweza kunuka kitunguu saumu kama ukiosha uso vyema).
Nakutakia mafanikio mema kwa maana kitunguu saumu ni dawa bora kwa magonjwa mengi, ikiwa pamoja na kansa, vidonda vya koo, vidonda vya tumbo nk.
Mdau J
Jamila pole sana mdau. ila kabla ya kukupa maoni yangu naomba unieleze uko nchi gani kwanza? Ili nijua nitakurushia vipii msaada wa aina yoyote. Asante sana
ReplyDeleteAcha kutumia vipodozi vya aina yoyote kwa sasa tafuta LIWA (ya kipande/kigongo) siyo ile iliyosagwa kabisa.
ReplyDeletetumia maji kidogo saga kipande cha liwa kwenye sakafu rafu rafu ya saruji siyo tiles utapata urojo wa liwa pakaa usoni (WAKATI UKO NYUMBANI) waweza kuscrub kidogo kidogo kama hutaki vile ,kaa nayo mpaka ikauke kisha osha uso wako na maji na sabuni ukipenda, pakaa mara kwa mara unapokuwa uko nyumbani vipele vitaondoka ila kwa wakati huo usitumie makrimu yoyote usoni, LIWA haina madhara yoyote na ni dawa ya ngozi.
kama ukikosa liwa ya kipande tumia hiyo hiyo ya unga lakini best ni ya kipande usage mwenyewe sakafuni.
Hii inawafaa hata wale wenye chunusi za madonda usoni muhimu uache kupaka makorokoro wakati huu.
Uso wako utasafika mwenyewe utatamani kujiramba! ila uwe na subira kidogo ROME haikujengwa siku moja!
Ungekuwa karibu ningekupatia kipande lakini bahati mbaya niko mbali. tafuta maduka ya dawa za asili kama pale kariakoo posta.
Nenda kamuone daktari wa ngozi haraka kabla hujapata canser ya ngozi. Unasema vipozi au ulikuwa unjaribisha mikorogo mbalimbali na yote imedunda. Kimbia hospitali haraka kabla hujaharibikiwa.
ReplyDeletePole ndugu, nenda umuone Dr wa ngozi mission mikocheni hospital. kuna dactari mzuri sana atakushauri cha kufanya.
ReplyDeletePole sana, kwanza achana na matumizi ya vipodozi kwa kuwa vipodozi vingi vinatengenezwa kwa kemikali tofauti nawe natumai ni mwafrika mungu aliyekupenda akakupa ngozi nzuri, pili muone daktari wa ngozi. acha ushamba wa kutumia vipodozi wakati huo umepita acha ngozi yako asili watu wataikubali tu
ReplyDeleteJAMILA, SI VIZURI KUJIFANYIA UTAFITI MWENYEWE, JAMBO ULILOTAKIWA KULIFANYA NI KUONANA NA MTAALAM WA NGOZI AMBAYE NI DAKITARI. MUDA WOTE ULIOPOTEZA UNAWEZA KUKUSABABISHIA MATATIZO YA KUDUMU. NENDA KAMUONE DAKITARI WA NGOZI NA USIZIDI KUPOTEZA MUDA ZAIDI KWA KUTAKA USHAURI KUTOKA WATU ZAIDI YA ELFU MOJA KWANI TUTAZIDI KUKUCHANGANYA KWA UKWELI NA UTANI, KUMBUKA KWENYE MSAFARA WA MAMBA NA KENGE WAMO.
ReplyDeleteMungu wangu, Wewe jamila yaani unakaa na tatizo zaidi ya miaka alafu unasema umejaribu jaribu vitu vya kupaka! Hivi wewe upo kweli kwenye hii dunia ya utandawazi? Kwa nini usiende hospital hiyo ni hospital case my dear nenda haraka hospital usijekuta uko kwenye matatizo mengine makubwa. Tafadhali PATA USHAURI WA KODAKTARI hakuna msaada mwingine zaidi ya huo!
ReplyDeleteMama Mo'
This is consultation u need to pay money... knowledge is not for free...
ReplyDeleteUmenichanganya kidogo hapo juu kabisa umesema tatizo lako ni uso kuwasha, halafu mwisho umesema saa zingine uso pia hupata muwasho!!!! nini tofauti ya 'uso kuwasha' na 'uso kupata muwasho'
ReplyDeleteUshauri wangu, usipake kitu chocho kwa muda wa miezi miwili halafu uone itakuwaje.
Hey jamila mimi sio Doc lakini nikuulize una uzito kiasi gani? Yaani kama unajua BMA index ungejaribu kufanya hivyo...Sijui kama hii inahusina na wew lakini mimi niliwashwa sana usoni lakini sikuwa na viupele. Kwenda kwa mactary wakaniambia nifanye massage sana na kufnay mazoezi ili damu iwe inatembea vizuri na kunywa maji sana. Na katika kuwa nafanya hivyo sijawahi kusumbuliwa tena na kuwashwa usoni na kwa sasa hivi weight yangu ipo kwenye normal range....
ReplyDeleteNatumaini wajuzi watakujulia
matunda,mboga za majani,ulezi,samaki na maziwa kwa wingi.itachukua muda mrefu sana kuisha kwani umeshaharibu kinga zako za mwili,sasa anza balanced diet kama ya mtoto mdogo.
ReplyDeleteSiku zote nasema stay black stay Beauty, hivi vipodozi(mikorogo) na dawa za nywele mnazo zitumia kwakufikiri kama weupe ni uzuri mtaja kiona cha moto mbeleni.Hata watengenezaji wenyewe(western Contries)hawavitumii. michuzi naomba utubandikie kile kibao tafadhali´´madhala yake ni makubwa ohh-madhara yake ni makubwa...wengine ....madhara yake nimakubwa´´
Pole sana mdau,Natumaini utakuwa ukitumia kwa nia ya kuondoa kuwashwa sio kuwa mrembo kama vijana wenzetu.
ReplyDeleteSasa nakushauri kwamba kuna magonjwa mengine huwa yako mwilini kwa maana ya damuni kupaa nje kemikali ni kuusambaza.
Unatakiwa kwenda hospita na kuwaona wataalamu wa ngozi bila kukata tamaa.
Pole, naungana na wadau hapo juu kuwa bora usijaribu kujitibu mwenyewe, na uende ukamuene mtaalamu wa mgonjwa ya ngozi.
ReplyDeleteUsitwange kitunguu swaumu na wala usinywe sumu, HAKIKISHA UNAENDA HOSPITALI UKAFANYIWE UCHUNGUZI NA KUPEWA TIBA SAHIHI, usijitibu wala mtu asiye daktari asikutibu, vinginevyo unaweza ukaingia katika steji nyingine ambayo ni ngumu kutoka.
ReplyDeletepole nakushauri ukaonane na mtaalamu wa ngozi aangalie kama umepata infection yeyote kwenye ngozi yako ya uso, na kama hauna basi tumia product za clean and clear 'made in europe' (usiniulize kwanini) na usiache kwa muda wa miezi miwili utanipa majibu yako, BLACKHEAD CLEARING DAILY SCRUB AND DEEP CLEANSING COOLING LOTION.
ReplyDelete