Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akionyweshwa moja ya Vitanda bora na vya kisasa na Daktari mkuu Professor Yaman Tekant katika hospitali ya ACIBADEM Nchini Uturuki mara baada ya kutembelea hospitali hiyo jana. Hospitali hiyo inamilikiwa na makampuni binafsi ya ACIBADEM Health Group ambayo yameonyesha nia ya kuja kufanya utafiti nchini Tanzania kwa ajiri ya kuwekeza katika sekta ya afya. Katikati ni Mhe. Suzani Lyimo Mbunge wa Viti Maalum
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akitembela hospitali ya ACIBADEM Nchini Uturuki katika ziara aliyoifanya kujionea Teknolojia mbalimbali katika sekta ya Afya nchini humo. Kushoto ni Daktari mkuu wa Hospitali hiyo Professor Yaman Tekant na kulia ni daktari bingwa wa Kansa prof. Dr. ENIS OZYAR ambaye pia alishawahi kufanya kazi katika hospitali ya Ocean Road nchini Tanzania . Hospitali hiyo inamilikiwa na makampuni binafsi ya ACIBADEM Health Group ambayo yameonyesha nia ya kuja kufanya utafiti nchini Tanzania kwa ajiri ya kuwekeza katika sekta ya afya
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta akionyweshwa moja ya mitambo ya kisasa ya kutibu kansa kwa njia ya mionzi na Daktari mkuu Professor Yaman Tekant katika hospitali ya ACIBADEM Nchini Uturuki mara baada ya kutembelea hospitali hiyo jana. Hospitali hiyo inamilikiwa na makampuni binafsi ya ACIBADEM Health Group ambayo yameonyesha nia ya kuja kufanya utafiti nchini Tanzania kwa ajiri ya kuwekeza katika sekta ya afya.
Picha na mdau Owen Mwandumbya wa Bunge




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 16, 2010

    DEAL MPYA SASA YA KUWEKEZA KATIKA AFYA ZENU NA MZEE ANAONEKANA KUNA KIASIFULANI ANATEGEMEA KUTOKA HAPO SIO MAENDELEO YA NCHI KWA UJUMLA.BADALA MAMBO HAYO WAFANYE WATU TOKA SECTOR YA UWEKEZAJI ANAFANYA SPEAKER WA BUNGE.NDIO KUSEMA IMESHAPITISHWA NA MAMBO NI YALE YALE,MTANZANIA NI OMBA OMBA WA KUDUMU WAKATI WACHACHE WANANEEMEKA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 16, 2010

    Mdau hapo juu usisahau Spika Sita alikua Director wa TIC so anauzoefu na madili ya uwekezaji.Ni bora amalizane nao huko huko ili kupunguza Gharama za kutuma timu nyingine iende for the same issue. Iyo hospital tunaiitaji sana Bongo.Bado tuna upungufu mkuwa wa health center bongo.

    ReplyDelete
  3. BoomshakaMay 16, 2010

    Wewe pimbi wa hapo juu.. spika wa bunge ana majukumu mengi tu, sio tu kukaa kwenye kiti bungeni kama unavyofikiria.. Yaani, kuna watanzania wengine mimi siwaelewi kabisa.. Nyie ndio mnafanya hata nchi ndogo ndogo kama Rwanda zinaendelea kwa kasi zaidi kuliko TZ.. Yaani, serikali inajitahidi kadri ya uwezo wake kuleta maendeleo nchini, nyinyi bado hamkosi la kusema.. Sasa kuna ubaya gani hapo, hospitali nzuri na ya kisasa kabisa.. Kwani lazima mwekezezai apitie hiyo sekta ya uwekezaji?? Viongozi wakisafiri nje, moja ya kazi yao ni kutembea sehemu kama hizi ili wakirudi nyumbani wanahakikisha wamerudi na mawazo mbalimbali ya kuendeleza taifa.. WATU KAMA NYINYI NDIO MNAZOROTESHA MAENDELEO HAPA!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 16, 2010

    Mbona comments zenu haziendani na habari yenyewe??? Jamaa wanasema wanakusudia kuja kufanya utafiti ili kama vipi wawekeze katika sekta ya afya, nyinyi mnaona Spika amefanya maamuzi gani hapo???

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2010

    Tusije tukafanywa guniea pigs...Utafiti mhhhhhh....Wa magonjwa gani? Mhhhhhh......hamna cha bure siku hizi na uchumi unavyoporomoka? Wanatafutia wakao kazi. Huko kwao madoctor hawana kazi hivyo wakileta hayo mavitu watapeleka na watu wao ...kill tow birds with one stone...kufanya utafiti wa madawa yao waliyoyavumbua na kuweza kuwapatia kazi vijana wao..

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2010

    Msimuue bure mdau wa hapo juu kwani ametoa maoni yake na anahaki ya kufanya hivyo. Ni kweli viongozi wetu ndiyo wanaoturudisha nyuma kimaendeleo na wala siyo mtu mwingine.

    You can't have the same people doing the same thing the same way over and over again and expecting different results. Kama si wenda wazimu ni nini?

    Usirukeruke hapa jadili mada.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 17, 2010

    Tunahitaji sana hospitali Tanzania. Ziwe za watu binafsi, Madhehebu, Serikali, wawekezaji wakubwa, wamachinga au hata watu wasiokuwa na akili kama anony wa kwanza.

    Ninaomba sana kama ikiwezekana hii hospitali ijengwe Tegeta, kwani hatuna hospitali ya maana kuanzia Bunju mpaka Mbezi.

    ReplyDelete
  8. MBUYI MWELA NA HOLLYWOODMay 17, 2010

    NYIE WATU ACHENI HIZO SPIKA SITTA WENGI HAMUMJUI,SI MTU WA VIJISENTI,HANA MAKUU NDIO HANA AKAUNTI NJE YA NCHI NA KWA TAARIFA YENU AMBAO PENGINE BADO WADOGO HAMKUWEPO HUKO NYUMA ENZI ZA MWALIMU HUYU MTU AKIWA WAZIRI WA MIUNDO MBINU ALIKWENDA HUKO UGHAIBUNI KUFUATILIA UNUNUZI WA KITU FULANI CHA UMMA KILICHOKUWA NDANI YA WIZARA YAKE BASI WALE JAMAA WAUZAJI BAADA YA MAKUBALIANO YA UNUNUZI WAKAMPA KITU KWA SASA MNAITA TAKRIMA YA DOLA 30,000 US,JAMAA ALICHOFANYA NI KUPIGA SIMU BONGO KWA MWALIMU NA KUMWAMBIA HABARI HIYO,NDIPO MWALIMU ALIPOMRUHUSU ACHUKUE ZIJE KUSAIDIA WATU WOTE BONGO,NANI ANAWEZA KUWA NA UJASIRI HUO,ZAIDI YA SOKOINE NA MWALIMU HAKUNA,SITTA ALIWEZA,KWANI ANGECHUKUA NANI ANGEJUA?JARIBUNI KUFUATILIA SIO KUWA WARAHISISHAJI NA WAPOTOSHAJI WA MAMBO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...