Ankali habari za kazi.
Mi naomna msaada kidogo, kuna kitabu kimoja nilikisoma zamani miaka ya 80, Kinaitwa “JE KISASI?” kimetungwa na mtunzi mahiri sana, bwana Hemed Kimwaga, Alikuwa mwandishi katika gazeti la “Mfanyakazi” enzi hizo! Hiki kitabu nahitaji kukisoma tena, hivo kama kuna mtu yeyote anacho tuwasiliane, au kama naweza kupata kontakti za mwandishi mwenyewe huenda akawa nacho, itakuwa poa!
Hud,
0719553621.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    wewe hebu soma vitabu vya kizungu uboreshe rugha achana na hayo ma vitabu ya kizamani ya juma na roza!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    we mdau hapo juu wa 10:11am ovyo!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2010

    ANKAL,HUYU BWANA KANIKUMBUSHA ZAMANI SANA. PENGINE KUNA HAJA YA KUPATA ORODHA YA VITABU VYA ZAMANI VYA KISWAHILI ILI KUKUZA LUGHA YETU NA HATA LAFUDHI.
    KANIKUMBUSHA VITABU VUFUATAVYO
    1. KIKOSI CHA KISASI- ELVISI MUSIBA
    2. KAMLETE AKIBISHA MLIPUE- HAMMIE RAJAB
    3. TUANZE LINI- KAJUBI MUKAJANGA
    4. KABWE MAKANIKA- ZAHIR ALLY
    5. KULI- SHAFII ADAM SHAFII
    6. LAWALAWA- FARAJ KATALLAMBULLAH
    7. SANDA YA JAMBAZI- HAMMIE RAJAB
    8. PAMBO- PENINA MLAMA
    9. MSAKO WA HAYAWANI- EDDIE GANZEL
    10.BAADA YA KISA MKASA- EMANUEL MAKAIDI
    11. TUTARUDI NA ROHO ZETU?- BEN MTOBWA
    12. ROSA MISTIKA- EUPHASE KAZILAHABI
    13. USIKU WA BALAA- SAID BAWJI
    14. IKIBIDI KUFA NIFE- NICO YE MBAJO
    15. NATAKA IWE SIRI- PETER S. KIRUMBI
    16. MWISHO WA MAPENZI- JOHN SIMBAMWENE
    17.GUBERI MFAWIDHI- JOHN RUTAYISNGWA
    18. DIWANI YA MUYAKA- MUYAKA BIN ABEID
    19. MABEPARI WA VENISI-(TAFSIRI)- MWL NYERERE
    20.USHINDI WA MAJERUHI- NDYANAO BALISIDYA (DADAKE PATRICK WA AFRO 70-WOTE MAREHEMU)
    BALOZI TUNAKAZI KWELI KWELI. KWA SABABU VITABU VYA KINA SHAKE SPEAR VYA 1600 VIPO VYETU HAKUNA

    MDAU

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2010

    we mdau wa kwanza unaoneka limbukeni sana ............ Binamu watu kama nyie ndo anawaimbia mrudi kwenu mjini hakuwafai... unataka kuiga kila kitu.. Umbayuwayu tu UMEKUJAA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2010

    Kwa kweli hata mimi huyu bwana mkubwa amenikumbusha mbali sana, huyo mtoa maoni hapo juu anaonekana ni mshamba sana na limbukeni wa kupindukia 'Heshimu Lugha yako' huwezi kwenda Ulaya or Asia ukakuta wanasoma vitabu vya kiswahili hata siku moja, bali utakuta watumia lugha zao.

    Naomba nimsaidie ndugu yangu Mtanzania na Mzalendo hii ndo numbre ya Bwana Hemed Kimwaga-0718885870
    thanx

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2010

    Pia kulikuwa na vitabu vifuatavyo:

    1. Kufa na kupona, na Njama -vya Elvis Aristabrus Musiba.

    2. Pete- Kezirahabi
    3. Ama Zao Ama Zangu- Hammie Rajabu
    4. Kizazi Hiki- Mkufya?
    5. Shida- Ndyanao Balisidya (masikini alipata PhD yake akiwa hoi kitandani Hospitali na siku chache baada ya kupata hiyo PhD kama sikosei mwaka 1986, aliaga dunia)

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2010

    Mdau umenikumbusha mbali usisaha kitabu cha
    1. Mashimo ya mfalme suleimani
    2.Hadithi za Bwana Alan Quarteman
    Kiswahili tukikuze vitabu tunavyo, huyo anoni anayepigia debe kiingereza bila shaka anabeba boksi kwa hiyo hiyo ni lugha yake ya kutumwa.
    Mswahili halisi

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2010

    Mdau huyo mwandishi wa hiyo riwaya anaitwa HEMEDI KIMWANGA ni Kimwaga

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2010

    "wewe hebu soma vitabu vya kizungu uboreshe rugha achana na hayo ma vitabu ya kizamani ya juma na roza!"

    kiswahili kilichotukuka

    ReplyDelete
  10. hongera sana kaka, mie pia naomba mdau mwenye kujua viyabu vyenye simulizi za mtu aliyekuwa kiitwa Willy Gamba, anisaidie namna ya kuvipata kama bado vinapatikana.
    thanks sana kwa kutukumbusha huko

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 20, 2010

    Kweli nimekumbuka mbali

    Kufa na kupona
    Jizuuu
    njama

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 20, 2010

    juzi nilikuwa na watu wa asia wanasema wamekaa london 15yrs lakini lafudhi yao haikubadilika katokea mbongo mmoja akaongea nae kidogo akamuliza umewahi kukaa nje jamaa akajibu ndio,mda gani jamaa akasema 3yrs, wapi londoni mbona lafudhi yako imechange ghafla kiasi hiki sasa naona ndio hawa watu ambao wanajidharau wenyewe wambongo kukaa nje kidogo anajifanya black america kumbe wamachinga pure shwain

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 20, 2010

    Hii pia imenikumbusha hadithi na simulizi kutoka GUBI LA WIFI, UA JEKUNDU, ALFA LELA HULELA

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 21, 2010

    mmenikumbusha mbali wadau. vipi kile kinachoitwa MIKONONI MWA NUNDA sikumbuki mtunzi wake

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 21, 2010

    Mdau wa 01:46, Umeniletea kumbukumbu ya huzuni. Ndyanao May Balisidya, aka Mrs. Materu, alikuwa mtu mmoja mwema sana. Alinifundisha mlimani. Alikuwa mdogo wake marehemu Patrick Balisidya. Mrs. Materu alifariki 1987 kwa saratani ya ziwa. Tunamwomba Muumba awalaze wote mahali pema. Amin.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 24, 2010

    Huyu jamaa anaye dharau vitabu vya kiswahili anafikiri kwa moyo badala ya kufikiri kwa kutumia akili.Anaishi kwa mazoea, hajui tofauti kati ya UKWELI na MTAZAMO watu wa aina hii kundi lao ni kubwa sana.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 06, 2016

    mie pia mmenikumbusha mengi hasa kitabu cha Pesa Zako ZInanuka na Nyota ya Rehema. Pia kitabu ambacho wahusika walikuwa Josina na Kalenga, jina limenitoka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...