Ankali habari za kazi.
Mi naomna msaada kidogo, kuna kitabu kimoja nilikisoma zamani miaka ya 80, Kinaitwa “JE KISASI?” kimetungwa na mtunzi mahiri sana, bwana Hemed Kimwaga, Alikuwa mwandishi katika gazeti la “Mfanyakazi” enzi hizo! Hiki kitabu nahitaji kukisoma tena, hivo kama kuna mtu yeyote anacho tuwasiliane, au kama naweza kupata kontakti za mwandishi mwenyewe huenda akawa nacho, itakuwa poa!
Hud,
0719553621.
Mi naomna msaada kidogo, kuna kitabu kimoja nilikisoma zamani miaka ya 80, Kinaitwa “JE KISASI?” kimetungwa na mtunzi mahiri sana, bwana Hemed Kimwaga, Alikuwa mwandishi katika gazeti la “Mfanyakazi” enzi hizo! Hiki kitabu nahitaji kukisoma tena, hivo kama kuna mtu yeyote anacho tuwasiliane, au kama naweza kupata kontakti za mwandishi mwenyewe huenda akawa nacho, itakuwa poa!
Hud,
0719553621.
wewe hebu soma vitabu vya kizungu uboreshe rugha achana na hayo ma vitabu ya kizamani ya juma na roza!
ReplyDeletewe mdau hapo juu wa 10:11am ovyo!
ReplyDeleteANKAL,HUYU BWANA KANIKUMBUSHA ZAMANI SANA. PENGINE KUNA HAJA YA KUPATA ORODHA YA VITABU VYA ZAMANI VYA KISWAHILI ILI KUKUZA LUGHA YETU NA HATA LAFUDHI.
ReplyDeleteKANIKUMBUSHA VITABU VUFUATAVYO
1. KIKOSI CHA KISASI- ELVISI MUSIBA
2. KAMLETE AKIBISHA MLIPUE- HAMMIE RAJAB
3. TUANZE LINI- KAJUBI MUKAJANGA
4. KABWE MAKANIKA- ZAHIR ALLY
5. KULI- SHAFII ADAM SHAFII
6. LAWALAWA- FARAJ KATALLAMBULLAH
7. SANDA YA JAMBAZI- HAMMIE RAJAB
8. PAMBO- PENINA MLAMA
9. MSAKO WA HAYAWANI- EDDIE GANZEL
10.BAADA YA KISA MKASA- EMANUEL MAKAIDI
11. TUTARUDI NA ROHO ZETU?- BEN MTOBWA
12. ROSA MISTIKA- EUPHASE KAZILAHABI
13. USIKU WA BALAA- SAID BAWJI
14. IKIBIDI KUFA NIFE- NICO YE MBAJO
15. NATAKA IWE SIRI- PETER S. KIRUMBI
16. MWISHO WA MAPENZI- JOHN SIMBAMWENE
17.GUBERI MFAWIDHI- JOHN RUTAYISNGWA
18. DIWANI YA MUYAKA- MUYAKA BIN ABEID
19. MABEPARI WA VENISI-(TAFSIRI)- MWL NYERERE
20.USHINDI WA MAJERUHI- NDYANAO BALISIDYA (DADAKE PATRICK WA AFRO 70-WOTE MAREHEMU)
BALOZI TUNAKAZI KWELI KWELI. KWA SABABU VITABU VYA KINA SHAKE SPEAR VYA 1600 VIPO VYETU HAKUNA
MDAU
we mdau wa kwanza unaoneka limbukeni sana ............ Binamu watu kama nyie ndo anawaimbia mrudi kwenu mjini hakuwafai... unataka kuiga kila kitu.. Umbayuwayu tu UMEKUJAA.
ReplyDeleteKwa kweli hata mimi huyu bwana mkubwa amenikumbusha mbali sana, huyo mtoa maoni hapo juu anaonekana ni mshamba sana na limbukeni wa kupindukia 'Heshimu Lugha yako' huwezi kwenda Ulaya or Asia ukakuta wanasoma vitabu vya kiswahili hata siku moja, bali utakuta watumia lugha zao.
ReplyDeleteNaomba nimsaidie ndugu yangu Mtanzania na Mzalendo hii ndo numbre ya Bwana Hemed Kimwaga-0718885870
thanx
Pia kulikuwa na vitabu vifuatavyo:
ReplyDelete1. Kufa na kupona, na Njama -vya Elvis Aristabrus Musiba.
2. Pete- Kezirahabi
3. Ama Zao Ama Zangu- Hammie Rajabu
4. Kizazi Hiki- Mkufya?
5. Shida- Ndyanao Balisidya (masikini alipata PhD yake akiwa hoi kitandani Hospitali na siku chache baada ya kupata hiyo PhD kama sikosei mwaka 1986, aliaga dunia)
Mdau umenikumbusha mbali usisaha kitabu cha
ReplyDelete1. Mashimo ya mfalme suleimani
2.Hadithi za Bwana Alan Quarteman
Kiswahili tukikuze vitabu tunavyo, huyo anoni anayepigia debe kiingereza bila shaka anabeba boksi kwa hiyo hiyo ni lugha yake ya kutumwa.
Mswahili halisi
Mdau huyo mwandishi wa hiyo riwaya anaitwa HEMEDI KIMWANGA ni Kimwaga
ReplyDelete"wewe hebu soma vitabu vya kizungu uboreshe rugha achana na hayo ma vitabu ya kizamani ya juma na roza!"
ReplyDeletekiswahili kilichotukuka
hongera sana kaka, mie pia naomba mdau mwenye kujua viyabu vyenye simulizi za mtu aliyekuwa kiitwa Willy Gamba, anisaidie namna ya kuvipata kama bado vinapatikana.
ReplyDeletethanks sana kwa kutukumbusha huko
Kweli nimekumbuka mbali
ReplyDeleteKufa na kupona
Jizuuu
njama
juzi nilikuwa na watu wa asia wanasema wamekaa london 15yrs lakini lafudhi yao haikubadilika katokea mbongo mmoja akaongea nae kidogo akamuliza umewahi kukaa nje jamaa akajibu ndio,mda gani jamaa akasema 3yrs, wapi londoni mbona lafudhi yako imechange ghafla kiasi hiki sasa naona ndio hawa watu ambao wanajidharau wenyewe wambongo kukaa nje kidogo anajifanya black america kumbe wamachinga pure shwain
ReplyDeleteHii pia imenikumbusha hadithi na simulizi kutoka GUBI LA WIFI, UA JEKUNDU, ALFA LELA HULELA
ReplyDeletemmenikumbusha mbali wadau. vipi kile kinachoitwa MIKONONI MWA NUNDA sikumbuki mtunzi wake
ReplyDeleteMdau wa 01:46, Umeniletea kumbukumbu ya huzuni. Ndyanao May Balisidya, aka Mrs. Materu, alikuwa mtu mmoja mwema sana. Alinifundisha mlimani. Alikuwa mdogo wake marehemu Patrick Balisidya. Mrs. Materu alifariki 1987 kwa saratani ya ziwa. Tunamwomba Muumba awalaze wote mahali pema. Amin.
ReplyDeleteHuyu jamaa anaye dharau vitabu vya kiswahili anafikiri kwa moyo badala ya kufikiri kwa kutumia akili.Anaishi kwa mazoea, hajui tofauti kati ya UKWELI na MTAZAMO watu wa aina hii kundi lao ni kubwa sana.
ReplyDeletemie pia mmenikumbusha mengi hasa kitabu cha Pesa Zako ZInanuka na Nyota ya Rehema. Pia kitabu ambacho wahusika walikuwa Josina na Kalenga, jina limenitoka.
ReplyDelete