yapata mwaka na nusu toka mshimo huu uliopo katika mtaa karibu na shopper's plaza jijini dar uanze kukenua na kuachwa kama ulivyo na wahusika. inasemekana magari kibao yameharibika aidha kwa kugongana wakati wa kuukwepa ama kuuvaa mshimo huo. pia watu kadhaa wameripotiwa kuvunjika viungo baada ya kutumbukia mshimoni. wazee wa jiji mpo??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kigagula wa JIJIMay 04, 2010

    Wazee wa Jiji tupo tunaendelea kula posho za vikao kama kawaida na vijana mkitaka nafasi zetu tutawashusha mishipa!! Kaeni kimya kama mnaonyolewa, mbona Richmond mlinyamaza

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2010

    Oh Well! They are busy rubbing shoulders with WAZUNGU on MILO and making a BIG PLAN for our city, and next they will be invited to World Forum and start talking again, and next there will be another meeting sometime next year, and more meeting, meeting and more meeting until they drop, this is not their priority for the next few more years. They have PLAN FOR YOU, get busy dying while they are busy making plans.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2010

    Mmh LaKiNi. NASisi. Watanzania wazembe kweli yaani majirani na hilo eneo mnashindwa kuweka karaii kama 4 za zege kufukia hilo shimo. Halafu juu mnalaza bao kubwa kuziba. Aumnafukia na cementi? Shauri yenu mtangoja milele hiyo serekali .by the time mmekumbukwa mmepoteza maisha ya watu au hata magari yenu yatakua yameshakongoroka.looool embu wajibikeni wanaume wa maeneo jirani na hapo

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2010

    Nipo tayari kukosa kura zenu-JK
    (hata msiponipigia, waajiri wenu watanipigia!!!!!!)

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2010

    mmhh, this country of ours bwana; kaaazi kweli kweli!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2010

    Kaeni mkao wa kula, tena kimya kabisa, sasa hivi keep left zote zitatengenezwa, pesa sasa inaelekezwa kwenye miundo mbinu mafano: mabarabara, umeme, mashule, mbolea, nk nk...... Hakuna haja ya kuwanufaisha hawa wachache 350,000 tu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2010

    Unajua itagharimu shilingi bilioni ngapi kwa kufunika na kufukia mashimo yote yaliyoko barabarani?

    Tunazihitaji fedha kwa shughuli za maendeleo!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2010

    Jamaa wa chuma chakavu wameshakula manhole cover. Ila uzembe huu ni wa serikali. Weka sheria kuwa chuma chakavu kisinunulie kienyeji na atakayefanya hivyo tunamshitaki kwa vandalism. Then sajili wanunuzi wote na kuhakikisha kuwa ukaguzi ufanyika kabla ya kununua, vitu kama mifuniko ya manhole vikikamatwa kwenye mzigo wako unalipa gharama ya mifuniko 500.

    Halafu kwa wajenzi wahakikishe wanatumia mifuniko ya zege uzito kilo 300, kama mtu ataiba labla aje na winchi

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2010

    Ndiyo tupo! si mlituona jana pale Karimjee Hall tukimwimbia Mhe Rais "sema usiogope sema" na guess what, kila mmoja wetu aliondoka na bahasha. Tupo, wee itisha kikao na bahasha utatuona.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 05, 2010

    Majirani na hilo shomo hawana expertise ya mambo hayo, ni madaktari, wahasibu etc, sio wafanyakazi wa ktk karakana...na wewe unayesema wajaze cement una akili kweli? Hiyo ni either septic tank au some other type ya pit shit, ikijazwa zege itafanya kazi yake? Hii ni kazi ya jiji so jiji liiangalie, ndo mana Ankal kaiweka ili jiji waone

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...