MAREHEMU SALIM ISSA ISIHAKA

UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA KWA NIABA YA WATANZANIA INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA NDUGU SALIM ISSA ISIHAKA KILICHOTOKEA LEO TAREHE 5/5/2010 MCHANA MJINI NAPOLI ITALY. MAREHEMU AMEUMWA GHAFLA.

MIPANGO YA MAZISHI INAFANYWA NA KWA TAARIFA ZA HARAKA NI KUWA MAREHEMU ATAZIKWA KATIKA MAKABURI YA KIISLAM MJINI ROMA. TAARIFA KAMILI YA SIKU YA MAZISHI ITATANGAZWA. JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA INAUNGANA NA WAZAZI ,NDUGU JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA HUU. MWENYEZIMUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMIN!!!
TAFADHALI KWA MAELEZO ZAIDI NA MICHANGO WASILIANA NA
VIONGOZI WA MATAWI:
NAPOLI: TEL: +39 3488307269
MODENA/RAVENA: TEL:+ 39 3403475405
ROMA: TEL: +39 348 4617229
GENOVA: TEL: +39 333 952 8659
PADOVA/VENEZIA: TEL: +39 338 716 8944

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2010

    ina lilah wainailah rajuunn
    tulikupenda salim sana ni mcheshi mtu
    wakujitolea kwakila jambo upo mbele kwa raha na shida lakini allah
    anamapenzi makubwa kutushinda sie wanadamu.mungu akupe makao mema akusamehe makosa yako amin.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2010

    m/mungu ampe kauli thabit marehemu safari yenye wepesi na amuondoshee adhabu za kaburi.

    Slim kaka yangu tutakukumbuka daima milele kwa uchesi na ukarimu wako. Haikuwa rahisi nilipopokea habari hizi mungu alikupenda zaidi.

    Inalillahi waina Illahi Rajioun.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2010

    R.I.P INASIKITISHA SANA SUCH A HANDSOME MAN!

    ReplyDelete
  4. Inna Lilahi wa Inna Iayhi Rajjun

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2010

    bwana michuzi hizi picha za marehemu sasa tunaomba uwe unaomba ruhusa kwa wafiwa kuzitundika. Kuna watu wana roho mbaya na wamepigika kiasi kwamba mpaka wanakuja humu kuwatukana waliotangulia mbele ya haki. Utawasikia "oooh majin yenu ya kibaharia..., oooh ndiyo madhara ya kudandia meli,...oooh ugiriki kumechoka mnaendelea kufa tuu rudini nyumbani" Ili mradi tuu mambo juu ya mambo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2010

    Upumzike kwa amani Salim. Poleni wafiwa. Naomba msaada jamani. Natafuta habari za mtoto wa dada yangu aliekuwa baharia mwaka 1986 na kupotea hadi sasa. Tumelia hadi tumechoka. alikuwa anaitwa MHANDO MGAYA mwenyeji wa Tanga. Mwenye habari zake za uzima au umauti taf anijulishe kupitia hii blog. asanteni.
    Ma mdogo

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2010

    Nami namtufuta BIYE (MHaya)! Aliondoka Dar mwaka 1986 kwa kudandia meli. Wazazi wake wamefariki bila kujua mwanao yuko wapi!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 06, 2010

    tunashukuru sana kwa kumuombea ndugu yetu SALIM ISSA ABDALLAH mazishi yatakua jumatatu inshaallah huko italy roma na sisi tunategemea kwenda kesho na huku london ndio wapo dada zake watatu kama kuna mtu anataka kuwapa pole wafiwa mnaweza kuwapata kwenye namba hii +447529935745. SHUKRAN. INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUUN.

    ReplyDelete
  9. I.W.R lakini ni vipi kwa sanduku?
    waislamu wa Italia mnao wajibu wa kutuelimisha imekuwaje.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...