Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa William Mganga Ngeleja, leo ametoa hotuba iliyojikita kwenye masuala ya Biofueli na uendelevu wake kwa mtazamo wa Tanzania, hapa Sevilla nchini Hispania akimwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Kongamano la Kimataifa la Biofueli, 2010.

Kongamano hilo litakalodumu kwa siku mbili, limewaleta pamoja viongozi wa sekta za viwanda, wawakilishi wa serikali na asasi zisizokuwa za kiserikali, wakichambua na kujadili masuala ya Biofueli ulimwenguni ili kurejesha matumaini kuhusu umuhimu wa biofueli na kubainisha mikakati mahususi itakayofanikisha biashara yake na uendelevu wa muda mrefu wa sekta hii.

Kongamano la Kimataifa la Biofueli 2010, ni la tisa katika mfululizo wa makongamano ya aina hii yanayoandaliwa kila mwaka na taasisi za F.O. Licht na Focus Abengoa Foundation.
Pichani juu ni Mhe. Waziri wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja, akitoa hotuba maalunu katika kongamano hilo asubuhi ya leo.
Rais wa Taasisi ya Focus Abengoa, Prof Jose B. Terceiro, akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Biofueli, 2010 leo asubuhi hapa Sevilla Spain.

Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala (mbele kushoto) Mhandisisi Ngosi Mwihava na Msaidizi wa Waziri, Sosthenes Masola wakishiriki kwenye mkutano.
Mhe Waziri wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja (katikati), Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala, Mhandisi Ngosi Mwihava (wa kwanza kushoto), Msaidizi wa Waziri, Sosthenes Masola (mwisho-kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Waandaaji wa Kongamano la Kimataifa la Biofueli, 2010, nje ya ukumbi wa mkutano, Sevilla, Hispania leo asubuhi.
Picha na Habari na Veronica Simba wa Nishati na Madini)




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2010

    Safi mnajitahidi, lakini mbona suruali zenu zina mikunjo kibao mapajani tofauti na za hao wenyeji, vilevile mbona wenzenu wamefungua kifungo kimoja nyie mmevifunga viwili au vitatu, mnatakiwa mchangamke, unaibia kwa wenzio chap chap halaf mnakua droo!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    Tanzania tunajua kuhudhuria sana makingamano, tamasha, semina nk nk...Ni nini tunachojifunza huko? manake havionekani nchini kabisa...

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2010

    Mheshimiwa Ngeleja, basi jitahidi nasi tupunguziwe gharama za umeme wa solar tuweze kuweka majumbani kwetu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2010

    mkimaliza mkutano wenu mkafanye shopping za suruali manake hao mafundi wa kariakoo bwana ebu oneni mambo mmmh!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2010

    Mi nakukubali Ngeleja, sema wizara uliyopo ngumu. Sasa usibweteke, chapa mzigo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...