Kongamano hilo litakalodumu kwa siku mbili, limewaleta pamoja viongozi wa sekta za viwanda, wawakilishi wa serikali na asasi zisizokuwa za kiserikali, wakichambua na kujadili masuala ya Biofueli ulimwenguni ili kurejesha matumaini kuhusu umuhimu wa biofueli na kubainisha mikakati mahususi itakayofanikisha biashara yake na uendelevu wa muda mrefu wa sekta hii.
Kongamano la Kimataifa la Biofueli 2010, ni la tisa katika mfululizo wa makongamano ya aina hii yanayoandaliwa kila mwaka na taasisi za F.O. Licht na Focus Abengoa Foundation.
Pichani juu ni Mhe. Waziri wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja, akitoa hotuba maalunu katika kongamano hilo asubuhi ya leo.
Rais wa Taasisi ya Focus Abengoa, Prof Jose B. Terceiro, akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Biofueli, 2010 leo asubuhi hapa Sevilla Spain.
Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala (mbele kushoto) Mhandisisi Ngosi Mwihava na Msaidizi wa Waziri, Sosthenes Masola wakishiriki kwenye mkutano.
Mhe Waziri wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja (katikati), Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala, Mhandisi Ngosi Mwihava (wa kwanza kushoto), Msaidizi wa Waziri, Sosthenes Masola (mwisho-kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Waandaaji wa Kongamano la Kimataifa la Biofueli, 2010, nje ya ukumbi wa mkutano, Sevilla, Hispania leo asubuhi.
Picha na Habari na Veronica Simba wa Nishati na Madini)
Picha na Habari na Veronica Simba wa Nishati na Madini)
Safi mnajitahidi, lakini mbona suruali zenu zina mikunjo kibao mapajani tofauti na za hao wenyeji, vilevile mbona wenzenu wamefungua kifungo kimoja nyie mmevifunga viwili au vitatu, mnatakiwa mchangamke, unaibia kwa wenzio chap chap halaf mnakua droo!
ReplyDeleteTanzania tunajua kuhudhuria sana makingamano, tamasha, semina nk nk...Ni nini tunachojifunza huko? manake havionekani nchini kabisa...
ReplyDeleteMheshimiwa Ngeleja, basi jitahidi nasi tupunguziwe gharama za umeme wa solar tuweze kuweka majumbani kwetu.
ReplyDeletemkimaliza mkutano wenu mkafanye shopping za suruali manake hao mafundi wa kariakoo bwana ebu oneni mambo mmmh!
ReplyDeleteMi nakukubali Ngeleja, sema wizara uliyopo ngumu. Sasa usibweteke, chapa mzigo.
ReplyDelete