Raisi wa Nigeria Umaru Yar'Adua (pichani) amefariki dunia siku ya Jumatano mwezi wa tano akiwa na miaka 58. Marehemu Yar'Adua alikuwa na matatizo ya moyo pamoja na figo.

Marehemu Yar'Adua atazikwa leo siku ya Alhamisi mchana katika kijiji cha Katsina nchini Nigeria.

Yar'Adua hakujushughulisha na mambo ya siasa tangu mwezi wa kumi na moja alipokuwa ameenda kutibiwa nchini Saudia Arabia. Alirudi chini Nigeria mwezi wa pili lakini alishindwa kuendesha shughuli za kiserikali kutokana na kuumwa.

Msaidizi wa Raisi Mh. Goodluck Jonathan atashikilia madaraka mpaka mwezi wa utakapofanyika uchaguzi mwingine mwezi wa nne 2011.

Marehemu Yar'Adua alikuwa ni msomi wa kwanza kutoka cho kikuu kuchukua madaraka, alishinda uchaguzi mwezi wa nne mwaka 2007.

Yar'Adua alipewa jina la "Baba Go-Slow", kutokana na utendaji wake wa kazi.

Historia yake.

Yar'Adua, alizaliwa katika mji wa Katsina mwezi wa nane tarehe 16 mwaka 1951, alikuwa muislamu.

Ametokea katika familia yenye kufuata mchakato wa kisiasa. Baba yake alikuwa waziri na kaka yake alikuwa mtu wa pili katika serikali ya Raisi Obasanjo's toka mwaka 1976 mpaka 1979.

Alisoma katika chuo kikuu cha Ahmadu Bello University Zaria kutoka mwaka 1972 mpaka 1975 masomo ya Chemist. Amesomea masomo ya MSc toka 1978-1980.

Alianza kusomesha Chemistry kabla ya kuingia katika biashara mwaka 1980s alikuwa mkurugenzi katika kampuni ya Sambo Farms Ltd katika mji wa Katsina.

Alichaguliwa kuungoza mji wa Katsina 1999 na kuchaguliwa tena kuongoza mji huo mwaka 2003. Maremu Yar'Adua alioa mwaka 1975 alijaaliwa kupata watoto saba.

Ally Muhdin
wa TZ-ONE.Blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 06, 2010

    wow! nimeshtuka sana poleni wanaija woote oyo yooo

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 06, 2010

    R.I.P Mr President.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 06, 2010

    RIP Yar'Adua!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2010

    Inalilahi wainailahi rajiuun....hakika kwake ndio marejeo!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2010

    Habari ya msiba, na 'woow', wapi na wapi? Ingebidi useme labda, OMG, etc

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2010

    To Allah we belong and to Him we Return, May Allah rest his soul in peace

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 06, 2010

    kwani wow! ni tusi?? kuna mishtuko ya aina nyingi omg ni yako mie siijui ebo!! hapa tunaomboleza usianze zileee za kong'ota mie mbayuwayu siishi unavyotaka wewe
    rip mr president

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...