Hujambo kaka Misupu. Niko Vekesheni Dodoma na nimejionea mambo mengi ambayo nitafurahia wadau wakiyaona pia.
Mdau wa kweli
Godfrey George Kyoko
Huyo hapo mwanafunzi ambaye nilimkuta shule moja ya msingi Dodoma. Ni mlemavu wa mikono na miguu ila anatumia mguu wa kulia kufanya shughuli zake zote. Anaetaka kumsaidia tuwasiliane – +255 787 771 414 au +255 715 771 414
Nyumbani kwa bibi yangu kijiji cha Mpwayungu, wilaya ya chamwino. Hili ni Tembe ambalo nililala usingizi mzuri sana usiku huo ndani yake. Yaani we acha tu!


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2010

    Yaani we mdau unatia aibu....sasa kuishi kwako Ulaya/America tunatusaidia nini kama unarudi na bado unalala kwenye nyumba za mbavu..badilika kijana..mkomboe bibi..mweke katika mazingira mazuri ya kuishi....oohhh

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2010

    Sasa cha ajabu ni kipi.. sisi tunalala kila siku na hatupigi kelele papasi, kupe ,chawa nk..hii sio habari

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2010

    natumaini wanabidii wenzangu mtaiona hii posti, naomba tujadiliane jinsi ya kumuwezesha na kufanya maisha yake yawe marahisi mwanafunzi huyu, ambaye kwetu sisi ni mtoto,mdogo wetu. nimeguswa na hili jamani

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2010

    Mjengee kajumba bibi yako, acha longolongo! Usingizi mtamu kitu gani bwana?? Usikute humo analala pia mother halafu wewe unaenda kuenjoy usingizi wa siku moja tena wa uchovu wa safari.

    Mkumbuke kwenu wajameni

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2010

    ama kweli pale nilipofikiri nina matatizo nakutana na mwingine yaliyomzidi manake sijui kama nimeona vizuri. navyohisi mdogo wangu huyu:

    hatembei, anatambaa
    miguu naona ina ulemavu
    mikono ina ulemavu

    naona anahitaji vitu vingi kushinda sie wote, ila sijaelewa katika bro aliyetoa hii picha ni kwamba mdogo wangu huyu anahitaji tu vitu vya kawaida mfano, wheelchair, madftari,peni, nk pa kuishi pako au ni msaada mpaka pa kuishi. najua wadau watanirukia ila ningependa kujua. Kaka heri ungeweka na email yako kusudi tukuandikie sio tu simu sababu habari kwa kamichu hazikai huwa zinaletwa nyingine. Mimi nitatuma msaada wangu nategemea na wadau wenzangu wote tutajiunga kumsaidia mdogo wetu huyu.
    shukrani kamichu na kaka uliyetoa picha.

    NB: kwa kweli mi kwabibi sijawahi kwenda kijijini wakati nimekuwa na akili zangu alikuwa tayari marehemu ila kwa picha hii nimejiuliza hoteli ya nini wakati nyumba nzuri kabisa hiyo? ama kweli tembea uone. mpe bibi hongera kwa kuweka nyumba yake vizuri. mwambie na mie naomba kuja.

    mdau, north america

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2010

    nadhani hapo ndo utaona umuhimu wa kumjengea nyumba bora bibi na next time utalala pahala bora zaidi.huko ujenzi sio garama sana ndugu yangu we utaweza tu.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana mdau, maana watu hapa wamezoea kutuonyesha mapicha ya kifahari kila siku, wakati asili yetu ndo hii, ukubali - ukatae lakini ndo maisha yetu. Na pia hata ukae Ulaya - America, hata uwe na uwezo mkubwa wa kifedha, huwezi kubadilisha nyumba zote za ndugu. Kama tunavyofahamu wanandugu ni wengi sana kwahiyo asili yetu ndo hiyo ya nyumba za tembe, mbavu za mbwa n.k. Pia wabibi, wababu huwezi kuwabadilisha kabisa eti umjengee nyumba ya bati?? Hata lala hata siku moja wao wamezoea hivyo hivyo na nyumba zao hizo. Mimi nilijitahidi ili kumbadilisha babu yangu, kumnunulia kitanda kizuri,sijui nini na nini...lakini nilivyo ondoka tu! Akagawa kwa wajukuu tena yeye mwenyewe bila kulazimishwa wala nini. Mimi binafsi nakusifu sana kutuletea hii picha nzuri ya asili yetu, maana hapa tumezoea kuona mpicha ya kifahari tu, hamna za kiasili maana watu wanaona aibu na asili zao.
    CHIBI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2010

    Mi nimeguswa sana na hii habari ila nilikuwa naomba kutoa ushauri upatikane mshanganuo wa mahitaji ya huyo mdogo wetu ndugu yetu mtoto wetu ili hata yule ambaye alikuwa hajui atamsaidia nini anaweza kupata wazo kutokana na michanganuo hiyo
    Kitu cha pili niliomba iwekwe labda acount nomber ili sisi tuliombali tuweze kuchangia kuchangia kwa namna hiyo au full address ili hata kwa westen union tuweze kutuma. Lakini kabla ya hapo iwepo email ya anayeshughulikia maswala hayo ili mipango hiyo iweze kufanyika vinzuri na kwa usahihi zaidi
    Otherwise hiyo nyumba imenivutia sana mi sioni sababu ya kumjengea nyumba nyingine kwani hiyo nyumba ni ya ukweli mbaya na ndo ya kihistoria hiyo kwani kulala kwenye nyumba nzuri unapata nini? Tuendelee kudumisha mila zetu wajameni aaaaaaaa!!!!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2010

    ebu acha hizo fanya mjengee bibi nyumba ya maana yani hata dirisha haina unapiga picha na kuleta humu jamani muwe mnakumbuka makwenu siku ya siku ni mambo ya aibu hata kama nyumbani ni nyumbani kwa kweli hapo mh hata hakuna miti vumbii tunaomba sana wadau wote sio kula bata tuu na kusahau kwenu mjengee bibi nyumba ya maana hata kama ni ya udongo basi iwe na hadhi nzuri.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2010

    Post ya kwanza mbona sioni popote mdau amesema aliishi America au Ulaya? Kama una ugomvi nae personaly then tafuta sehemu nyingine ya kumkamatia.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 29, 2010

    jamani nyie ina wahusu nini hata bibi yake akilala chini kama wako happy nyie kina waumia nini,hapo ametuwekea picha ya mtot mlemavu ambaye anastahili msaada mkubwa sana sio kelele zenu za kumsema jamaa ni bibi yake,... wenye uwezo wakumsaidia jamani fanyeni mpango hii dunia nia ya kupita ... na tusilalamike na kustress na vijishida vdogo vivyotukumba ktk maisha ye2 .... angalieni watu wenye shida zaidi yako ndo utaweza hatakumshukuru mungu kwa ulichonacho. mungu amsaidie mtoto wa watu amin. PEACE!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2010

    Ee bwana ee...acheni kumdanganya mwenzenu...kaka mjengee nyumba bibi hata kama ya udongo lakini weka sakafu chini na bati....tusidanganyane bwana mambo ya kulala kwenye tembe yashapitwa siku hizi. Tembe zibakie makumbusho...Hakuna hata mmoja aliyemshauri asimjengee bibi yake ambaye analala kwenye tembe hapa...Kaka usisikilize uchimvi...wote hao kama wewe hawajawajengea bibi zao ndo maana wanakuwa na defensive mechanism...to justify their selfish behaviours. Please muweke bibi pazuri mwongezee maisha kidogo kwani ukimjengea atafurahi...na unajua furaha huongeza maisha. Mtu asikudanganye eti atakataa...Nani hataki kizuri bwana? Acheni hizo...Charity starts at home Bw...AKU !

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 29, 2010

    ukisoma comments za watu wengi humu utagundua yafuatayo:-
    1.jamii yetu bado ipo katika hali ya ujima,na inakumbatia ujinga ikidhani ndiyo asili. huwezi kusifia nyumba hiyo kuwa ni bora na ndiyo asili yako,unapaswa kuwa na mtizamo chanya kubadilika ili kuepuka vitu visivyo stahili,hii nyumba haikidhi viwango vya afya na anayeishi humo nikwakuwa hana jinsi tu. tusidanganyane hapa hata wamasai kuvaa matairi ya gari na shuka siyo asili,kwakuwa hawakuwahi kuwa na kiwanda cha kuvitengeneza! sasa asili iko wapi?labda wangevaa magome.
    2.watu wengi hawana exposure ya historia,hata ulaya,asia,america,walipitia hatua flani lakini hivi sasa hawaviendekezi hivyo vitu sanasana utavikuta makumbusho,maana havina tija kwa maisha ya sasa na wangevikumbatia wangekuwa ombaomba kama sisi,swali ni kuwa wangeomba kwa nani?hahaha
    3.nimeona wengi wanazungumzia habari za ooh ndugu wengi,huu ujinga wa kuendekeza extended family ndiyo unaosababisha baadhi ya watu kutokuwa responsible wakitegemea kuwa ndugu yao mmoja anaye hangaikia life ndiye aende akawaokoe. lazima watu wajifunze kubadilika ndipo tutaendelea,ulaya,amaerica hawaendekezi ujingaujinga huu wa kutegemea ndugu na kutwishana mizigo isiyostahili,kama wewe huwezi kuwa na mipango ya kukuwezesha kuwa na familia unayo imudu kuitunza ukitegemea kuzalisha ombaomba ili wakasaidiwe na wasamaria wema wakiwemo ndugu zako wanaochakarika,wewe pia unastahili bakora ili uzinduke uanze kujipanga vizuri na kujenga muelekeo mpya wa kimaisha.ukizaa unatunza mwenyewe,na uzingatie pia kuwa unaweza kufa gafla wakati ungali bado unategemewa hivyo usiwajengee wengine mzigo wa kukutunzia wanao 10.afadhali uache 1 au 2 hapo kidogo inaeleweka.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 29, 2010

    sorry mimi hapa sihelewi !! sasa hapa mdau unataka sisi tumsaidie huyo mwanafunzi ama BiBi yako???

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 29, 2010

    mimi sioni ubaya wa kuishi/kulala kwenye tembe, dirisha la nini, ukitaka mandhari si utoke nje tu, look how big the yard is, wanasema waafrika tumepigwa na jua lakini hatuoni mwanga, we got all this sunshine but we dont see anything!!!. jamaa wamekazania kuomba tu . mdau USA

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 30, 2010

    INAUMA LAKINI NDO UKWELI.KAMAU MAHALA FULANI KASEMA TULIVYO WATZ.MANENO MENGI KWENYE MAMBO YASIYO NA MAANA YEYOTE.AJABU MICHANGIO MINGI NI KUHUSU NYUMBA ZA TULIKOTOKA.MAJAMAA WENGI HAWAJAONA PICHA YA HUYO MTOTO,WANAONA NYUMBA TU.LABDA MDAU AWEKE HIYO PICHA YA MTOTO PEKEE NDO TUTAONA.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 30, 2010

    NANI KASEMA UJENZI WA NYUMBA NI GHARAMA KUBWA TANZANIA TATIZO NI KUTAKA KUJENGA MAKASRI YA ENZI ZA KING HENDRY,HAPA DUNIANI TUNAPITA TU KWA MUDA UJENZI WA KUDUMU KWANI HAPA KWENU MILELE MIMI NIMEVUTIWA SANA NA UJENZI HUU NA NI MFANO WA KUIGWA NA WABEBA MABOKSI HUKO UGHAIBUNI SIO LAZIMA KUJITIA VILEMA KWA KUTAFUTA MAKUBWA WAKATI MADOGO YAPO SEMENI NA ROHO ZENU VEMA KABLA HAMJAZEEKA BILA KUPATA PA KULALA.
    KAKA KUONA SAN DIEGO.
    MWENGE GENGENI.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 30, 2010

    Email ya shirika linalo muangalia huyu mtoto ni hii: info@parenttz.org

    Ahsanteni wadau kwa kutoa maoni mengi na mazuri.

    Kwanza mimi sibebi box marekani wala ulaya, nipo hapa hapa bongo tu. bibi yangu anapenda kuishi kwenye tembe hilo na hata mimi huwa namtembelea sana na tunalala humo humo. Hio kwetu ni nyumba ya kifahari.

    Kuhusu huyo mtoto anahitaji mambo mengi, kama sare, baeskeli ila mjue lazima mtu amsukume hawezi kujiendesha, pia nafanya bidii kupata shule ambayo anaweza kupelekwa ili asome na kutunzwa vizuri kuliko hapo anakula vumbi tu.

    Mdau wa North America email yangu hio hapo juu.

    Mdau Chibi hongera....

    Email: info@parenttz.org

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 30, 2010

    Watu wanashangaza!!!!!!!????????? Mkataa asili mtumwa, hata kama itajengwa nyumba nyingine hiyo isivunjwe asilani, kwangu mimi ni musium ya nguvu maana ni maridadi sana. Watalii wakija wanafurahia sana kulala kwenye nyumba hizo tena kwenye mahoteli ya kitalii. Ushamba tu.

    Mwaya nawaunga mkono wadau waliotangulia juu ya kumsaidia mtoto huyo, kwa kweli amekuwa mfano wa kuigwa kwa wote walioumbwa kama yeye.

    GJK

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 31, 2010

    ningeongea vizuri zaidi kama angetuwekea na picha ya nyumba ya baba yake au ya kwake mwenyewe kama anyo.kama zote ziko kama hiyo ya bibi basi kijana ana matatizo.mtu anaizidi nyumba urefu akiingia ndani inakuwaje.jamani kumbukeni nyunbani kwenu.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 31, 2010

    Big up wadau GJK,Mdau USA na Mdau Mwenge Gengeni.
    Ahsanteni wadau wote kwa kuendelea kuchangia. Shida yangu sio kumjengea bibi wala kupata msaada wowote. Cha msingi hapa nilitaka mlio ughaibuni na msio fika home mjionee mfano wa nyumba za kimila.

    Kubwa hapa ni huyo mtoto anaeteseka. Wengi mnaona nyumba ya bibi (TEMBE) na hammuoni kibinti hakina miguu wala mikono. Jitokezeni tumsaidie huyo mtoto. Anaishi kijijini sana na hana msaada wowote. Mjali na wenzenu mlio waacha nyumbani. Email; info@parenttz.org

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...