SERIKALI KUPOKEA MAANDAMANO YA VYAMA VISIVYOGOMA.

WAZIRI wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya anatarajia kupokea maandamano ya wafanyakazi kwa ajili ya kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) yatakayofanyika kesho asubuhi katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Maandamano hayo yatawashirikisha wanachama wa vyama vya wafanyakazi ambavyo havishiriki katika mgomo ulioitishwa na Shrikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA).

Akizungumza na Idara ya Habari(MAELEZO) leo jioni, Waziri Kapuya amesema maandamano hayo yataanzia eneo la Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) eneo la Gerezani.

Miongoni mwa washiriki katika maandamano hayo ni pamoja na wafanyakazi wa Benki za NBC na NMB, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE).

Aidha maandamano hayo yatapitia mtaa wa Sokoine, Azikiwe na Bibi Titi Mohamed kuelekea viwanja vya Mnazi mmoja ambapo Waziri Kapuya atayapokea majira ya saa tatu asubuhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...