Afisa wa Idara ya Ufundi (TFF),Saad Kawemba akiongea na waambishi wa Habari waliofika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo ndani ya ofisi za TFF,wakati wa kukabidhiwa vifaa vya michezo kwa timu 8 zilizofuzu kucheza hatua ya robo fainali za mashindano ya Kili Taifa Cup.kulia ni kocha wa timu ya Ilala,Jamhuri Kiwelu "Julio"
Meneja wa kilaji cha Kilimanjaro,George Kavishe akimkabidhi viatu kocha wa timu ya Ilala,Jamhuri Kiwelu "Julio" kwa ajili ya timu yake iliyotinga hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kili Taifa Cup yatakayoanza kutimua vumbi kwa hatua hiyo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar,jumatatu ya tarehe 24.
Katibu wa Chama cha Soka cha Temeke,Bakili Makele akipokea viatu vitakavyotumika na timu ya mkoa wake katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya kili Taifa Cup toka kwa Meneje wa kilaji cha Kilimanjaro,George Kavishe,makabidhiano hayo yamefanyika leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za TFF,Ilala.
Muwakilishi toka Timu ya Mwanza,Ngawina Ngawina nae akipoke viatu kwa niaba ya timu yake toka kwa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George kavishe katika hafla fupi iliyofanyika leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF,Ilala
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akikabidhi viatu kwa Ramadhan Mahano ambaye ni Katibu Msaidizi wa IRFA,kwa ajili ya timu ya Iringa.timu zilizofuzu kucheza hatua ya robo fainali ni Ilala,Temeke,Iringa,Mwanza,Singida,Kilimanjaro,Arusha na Lindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2010

    viatu vya mchina!!Adi leo vitabu vyetu vinashindwa kujinunulia vifaa vya michezo!! kweli tunachekesha

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2010

    jamani wadau naomba kuuliza huyu kaka zuri hivi ni nani na je ameoa je bibi yake nani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...