Mzee Juma Mkonko (kushoto) kutoka katika kijiji cha Mwenge,wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora akicheza na Nyoka wakati kundi lake likicheza ngoma aina ya Uyeye ambayo huchezwa na kabila la Wanyamwezi leo wakati wa maadhimisho ya siku ya utamaduni inayoendelea katika viwanja vya Mandela Mkoani Singida.
Wakina mama kutoka mkoa wa Singida na Dodoma wakishindana kusaga karanga kwa kutumia njia ya asili wakati wa maadhimisho ya siku ya utamaduni inayoendelea katika viwanja vya Mandela Mkoani Singida, Hata hivyo Bi.Ukende Zefania (kushoto) kutoka wilaya ya Ilamba aliibuka mshindi. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2010

    This is nice mbona hujaweka picha nyingi tuone tamaduni mbalimbali na mambo mengine waliyoyafanya huko?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2010

    Ankal,umenikumbusha mbali sana,ngoma hii ni nzuri sana kwa kuondolea stress.Hawa jamaa wanachekesha sana,nawakumbuka wacheza buyeye wazuri kama Kina Fupe,watu wa kanda ya ziwa wanaifahamu sana hii ngoma.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2010

    Mbona wamepozi kama wanacheza kiduku??? check miguu inavyonata.... hii kiduku mshikaji wangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...