Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania na Mfuko wa kusaidia Jamii Vodacom Foundation Mwamvita Makamba (pili kulia) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya kaskazini Mbuvu Kamando (kulia) na maofisa wengine wakiwasili kwenye uzinduzi wa kutumia madarasa mawili yenye thamani ya Shilingi Milioni 22 kwa Shule ya Sekondari ya Mtimbwani Mkoani Tanga . Mfuko huo ulijenga madarasa hayo ikiwa ni sehemu ya programu yake ya kukuza kiwango cha elimu nchini Makabidhiano haya madarasa yalifanyika mwishoni mwa wiki.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga Rachel Chuwa wa pili toka kulia,Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania na Mfuko wa kusaidia Jamii Vodacom Foundation Mwamvita Makamba (kushoto)Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom kanda ya kaskazini Mbuvu Kamando wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kutumia madarasa hayo mawili
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania na Mfuko wa kusaidia jamii Vodacom Foundation, Mwamvita Makamba, akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Mtimbwani, iliyoko Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, Mfuko wa Vodacom Tanzania ulikabidhi madarasa mawili yenye thamani ya Shilingi Milioni 22 kwa Shule ya Sekondari hiyo . Mfuko huo ulijenga madarasa hayo ikiwa ni sehemu ya programu yake ya kukuza kiwango cha elimu nchini Makabidhiano haya madarasa yalifanyika mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania na Mfuko wa kusaidia jamii Vodacom Foundation, Mwamvita Makamba, akiwasisitiza jambo baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mtimbwani, iliyoko Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, ambapo Mfuko wa Vodacom Tanzania ulikabidhi madarasa mawili yenye thamani ya Shilingi Milioni 22 kwa Shule ya Sekondari hiyo
Hili ni Moja ya darasa lililojengwa na Mfuko wa kusaidia jamii wa
Vodacom Tanzania( Vodacom Foundation)





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2010

    HAPO MWAMVITA AMECHOMEKEA CCM KWA KIAINA, VODA IANGALIE ISIJE IKAWA YA CLOUDS FM NA UCCM.

    ReplyDelete
  2. Davo GotiMay 17, 2010

    Hongereni Voda. Mkurugenzi wa Voda mbona kavaa ze fulana ya rangi za Tigo tena katika tukio la kivoda zaidi?! Au ndio Fair Play? Poa lakini.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2010

    Sahihisha jina la kaimu mkurugenzi, ni "NGUVU KAMANDO" na siyo mbuvu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2010

    Nguvu tunakumiss mazoezini Dar jumamosi asibui, all the best.Tupo pamoja

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2010

    samahan kwa umbeya hebu nisaidieni...huyu modo ndio mtoto wa mr makamba wa ccm..aka mcharuko wa ccm...?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2010

    kuna mambo mengi serekali lazima hione haibu hivi serekali hina shindwa kujenga shule nzuri tanzania kote. wangepunguza safari za kwenda ulaya ,mishahara yao na ufisadi. tusingekuwa na shule vibanda kwani hivi ni vibanda vya kusomea si shule. Africans hatupo serious .hivi nikipi tunachoweza kufanya kwa ufasaa ???

    ReplyDelete
  7. MANJI'S ARMYMay 17, 2010

    HEEE KUMBE MWAMVITA YANGA DAMU,WANYAMA WA MSIMBAZI HAWAIPENDI HII,LAKINI HABARI NDIO HIYO,YANGA OYEEE,SIMBA WAZEE WA MISRI MMMM!

    ReplyDelete
  8. muddy drogbaMay 17, 2010

    MDAU ULIYESEMA ETI KAVAA THE FULANAS RANGI YA TIGO HAPANA HIYO NI RANGI YA YANGA NA YEYE NI MWANACHAMA WA YANGA,SO ANAWAKILISHA CHAMA LAKE INGAWA MZEE MAKAMBA NI MNYAMA DAMU

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 17, 2010

    Huyo modo sijui mwavita kwa kweli amesuuza roho yangu,she is real real raealy cute...kama hajaolewa au ana mpango wa kumbwaga chini bwana yake niko tayari kutoa kifuta jasho kwa atakayenisaidia kumpata maana niko busy sana na kubeba box.

    ReplyDelete
  10. Davo Goti hiyo aliyo vaa mwanvita ni Jezi ya timu ya Africa ya kusini aka bafanabafana,ukizingatia Vodacom ni kampuni ya south africa upo hapo kwani huku kila ijumaa wafanyakazi wanavaa jezi hizo kuwasapoti timu yao upo sio rangi za Tigo

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 17, 2010

    Mwamvita siku hizi anapendeza. Yaani super model haswa. Halafu pia anafanya vitu vinavyoeleweka katika maisha. Kwa kweli kwa umri wake mdogo kuwa Mkurugenzi, si kitu kidogo. Hongera sana.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 17, 2010

    mhhh kaka MISUPU huyo Mwamvita nikimuona dah napata Kigugumizi.
    Mdau -Ukerewe!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 18, 2010

    BAFANA-BAFANA
    kazi kweeli

    kampuni za simu wizi mtupu!!kwa zamu tu

    ReplyDelete
  14. Hadj Drogba "mwana chelsea"May 18, 2010

    HATA MIMI NIKIMUONA HUYU MWANADADA SIO SIRI NAPATA KIGUGUMIZI CHA UKUBWA!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 18, 2010

    Jamani hiyo siyo yanga ni bafanabafana
    kwani hamjui voda com ni sauzi?Na sasa ndiyo kipindi cha fulanasi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...