Mh. Pinda alipokutana na viongozi amejadiliana nao kwa jinsi gani wameweza kuiletea maendeleo katika nchi yao.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Bi. Mwanaidi Maajar alimkaribisha Mh. Pinda na kutambulisha kwa maafisa wa Ubalozi pamoja na Kiongozi wa Jumuiya za Watanzania Bw. John Lusingu ambaye nae aliitambulisha Jumuiya nzima kwa Mh. Pinda.
Mwenyekiti wa TA nchi Uingereza Bw. John Lusingu alimueleza Waziri Mkuu mikakati na mipango ambayo Jumuiya hiyo inafanya kuweza kuwasaidia Watanzania waishio Nje ya nchi pamoja na wale waliopo nyumbani.
Mikatika hiyo ni kuhusu suala zima la Michezo, Kilimo, Usafiri, Habari, mfumo mzima wa huduma za mazishi na matatizo ya Watanzania yanayowakabili katika masuala mbalimbali.
Mh. Pinda alisema serikali ipo tayari kuwasaidia Watanzania wote watakaojitokeza kuelezea matatizo yao na hivi sasa serikali inaangalia wananchi wenye hali duni ili kuweza kuboresha maisha ya wananchi hao.
Serikali imevipa kimaumbele Elimu, Maji, Bandari, Barabara, na Umeme na inaangalia jinsi gani itakavyoweza kuboresha huduma hizo. Alisema Mh. Pinda.
Mh. Pinda alimsifia Balozi Maajar kwa jinsi gani ameweza kuwasaidia Watanzania wawe na Jumuiya na mchango wake mkubwa katika masuala mbalimbali ya kuwasaidia Watanzania waishio Uingereza.
Mh. Pinda ameichangia Jumuiya hiyo kiasi cha £2000 na kuahidi kuwa serikali itaangalia jinsi gani itakavyoweza kuwasadia katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Balozi Maajar alimshukuru Mh. Pinda kwa mchango wake wa kuja kuangalia maendeleo ya Watanzania na kuichangia Jumuiya hiyo.
Na Ally Muhdin wa
www.tz-one.blogspot.com
BOFYA HAPO KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPO KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...