Utapeli wa mawakala wa
kutoa mizigo airport na bandarini...

Ankal naomba uweke mada hii ijadiliwe.
Baadhi ya mawakala wa kutoa mizigo bandarini na uwanja wa ndege wa julius nyerere wamekua wakiikosesha serikali mapato mengi na pamoja na kuwaibia kitapeli wateja walioagiza mizigo toka nje.

Kinanchofanyika, mzigo wako unapofika agent utakae mtumia kuutoa atatayarisha documents zote, inapofikia stage ya kupata kinachoitwa assesment ya kiasi gani ulipie ndipo utapeli unapoanzia.
Agent atakulaghai huu mzigo wako unatakiwa ulipie mfano sh.5,000,000 (milioni tano) wakati huohuo anakuonyesha assesment yake ya kitapeli (fake) inayoonyesha 5,000,000 unadaiwa,haina tofauti mpaka na mihuri ya customs (wenyeye wanaziita za porini) atakwambia lakini nimeongea na customs officer anaweza kupunguza mpaka ulipie sh.1,500,000 ila yeye inabidi tumpe milioni 2,000,000 utaokoa 1,500,000, ukiwa na tamaa utanasa kwenye upuuzi huo. Akikukosa hapo, hata ufanye nini ukiwa ni mtu wa shughuli nyingi ( huwezi kwenda kulipia mwenyewe) atakupata kwenye kulipia hasa utakapompa pesa akalipie yeye bank , ile assesment yake halisi aliyo underinvoice ndio atayoilipia kiasi cha pesa ndogo mno kisha atarudi huko porini akatayarishe pay in slip ya kitapeli itayoonyesha amelipia pesa nyingi,zilizosalia anatia kibindoni, hata hizo pay in slip na mihuri ya benki huwezi tofautisha na zile halisi za benki.

Naomba niwatahadharishe waagizaji wenzangu tuwe makini mno na hawa maagent,wengi wana mchezo mchafu, inapofikia kulipia bora uwende benki ukalipie mwenyewe.

Pili TRA itoe elimu ya kutosha kwa walipa kodi kuhusu viwango vya kodi stahili kwa kila bidhaa inayoingia ile waagiza wasiangukie kwenye mikono ya walaghai wachache.

MDAU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2010

    NIKWELI KABISA ANKAL AIR PORT YETU INANUKA KWA RUSHWA NA WIZI MFANO MIMI NI MWANAFUNI LKN NINAPOKUJA NYUMBANI MIZIGO YAKO MARA ZOTE IMEKUWA IKIFUNGULIWA AMA KUPOTEA AMA KUOMBA RUSHWA NAPORUDI AMA KUSAFILI, PIA NIKITUMA KIMZIGO KIDOGO TU UTASKIA MALAKI YA SHILING UNALIPISHWA KAMA USHURU, MFANO NILISHAWAHI KUTUMA WINO WA PRINTA HUKU NIMENUNUA HATA ELFU KUMI HAZIFIKI ZA SHILING AIRPORT WALINILIPISHA USHURU LAKI MBILI, SASA NAULIZA USHURU WETU AIPORT HAUNA FORMULER? MAANA NI ASILIMIA NGAPI YA THAMANI YA KITU WANACHOTAKIWA KUTOZA USHURU?JE NAHAO WANAOENDA KUFANYA BIASHARA WANALIPIA KIASI GANI KUHAKIKISHA WANAPATA FAIDA?MASUALI WALIYONIAMBIA NI SAWA NA MDAU ALIVYOELEZA HAKUNA TOFAUTI

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2010

    Mhhhhhhhhhhh inatisha wadau.Jamhuri iko wapi na perishables[vyakula na nyama kutoka ughaibuni] zinapita kimyakimya bila vibali vya TFDA?
    Hapa kweli serikali haina macho au?

    ReplyDelete
  3. TRA wanaoperate katika centuary ya 47" na hii ndio maana tunapoteza mapato ya nchi kwenye issue kama hii mtoa maoni aliyetoa. TRA system is unfufunctional katika centuary ya 21 napenda kutoa maoni kwa TRA na TZ government kuboresha huduma za CoDE kama ifuatavyo:-
    1. TRA needs to upadate the code system especially wanatakiwa code system ya malipo iwekwe wazi kwa wateja/ au walipa kodi ijulikane. Kwa mfano huku nchi za wenzetu ukipiga simu au ukabrowse kwenye internet ukajaza inform zinazotakiwa within 5 second utajua hiyo bidhaa yako intakugarimu kiasi gani!!! Lakini TRA b'se hakuna information standard za kodi zinazojulikana kwa walipa kodi ndio maana unaona kuna rushwa hapo. Let"s say kama kiwango cha kodi ya gari SUV labda ya mwaka 2007 ni 5milion inajulika na iko kwenye code system ya TRA na mteja anajua hilo nani atatoa rushwa?? u see wat i'm saying?
    2. TRA wanatakiwa kuelisha walipa kodi kama semina na kuwa wawazi na kutuo incentive wa wateja wanaotoa habari kwa employees wanaoomba rushwa, vilevile wanatakiwa watengeneze Website na kuwa updates kila mara yenye habari za garama za kodi kwa kila kitu ili hata kabla hujaangiza kitu chochote uweunaweza kujua itakugarimu kiasi gani kulipia kodi.
    3. TRA wanatakiwa kuwa na kitengo Public Relation hii itasaidia kuleta uhusiano wa wateja wake pamoja na vyombo vya habari.
    Na mwisho napenda kusema TRA AUTHORITY LABDA WANGEKUWA WANATATHIMINI NA KUJIFUNZA NA KWENDA NA MABADILIKO YA TECHNOLOGY YA SASA ITASAIDIA NA ITAPUNGUZA RUSHWA KWA KIASI KIKUBWA SANA.
    mdau: opulukwa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2010

    nilishawahi kuambiwa nilipe laki tatu kwa nguo zangu na shuka , viatu pea mbili na vitu vidogo vidogo ambavyo ilikuwa extra lugage, niliruhusiwa kilo 20 tu kwenye ndege,mpaka kutoa vitu vyangu ilichukua wiki mbili na nusu na nikawa nimetoa jumla karibu laki tatu na nusu. mlolongo mrefu wa watu wa kulipa hadi anaeenda kuangalia kama mzigo wako upo, atakaeutoa n,k

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2010

    TATIZO NI SERIKALI NA SERIKALI NI WATU PALE WALIPOPITISHA SHERIA YA KUWA MTU BINAFSI HARUHUSIWI KUTOWA MZIGO WAKE BILA KUPITIA KWA CLEARING AGENCY, HILO NI KOSA KUBWA SERIKALI IFUTE SHERIA HIYO NA IRUHUSU WATU KUAMUWA WENYEWE AMA KUTUMIA AGENCY AU AUTOWE MWENYEWE HAPO WIZI UTAPUNGUWA NA PIA KAMA HILO HALIWEZEKANI BASI MWENYE MZIGO NA KARANI WA CLREARING AGENCY WAWE BEGA KA BEGA HATUWA ZOTE NA SHERIA ZIWE WAZI KWANI KUNA HAJA GANI YA KUZIFICHA NA WATU WENGI WANAKUWA MBUMBUMBU NA SHERIA ZA NCHI JUU YA MIZIGO? NA KWA NINI KUWA NA MAKADIRIO NA SHERIA ZINASEMAJE, HUU UPUUZI WA KUKADIRIA KODI NDO DIRISHA LA WIZI, WATU TUDAI KWA SERIKALI HAYA MAMBO YAWE WAZI SI YA KUFICHANA ILI KUJENGA MWANYA WA WIZI

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2010

    yani yani ndugu yangu mimi nimeshalizwa hapo bandarini mara2 nilipotuma gari kutoka hapa Uk, Hicho ulichoandika ni kama vile unaelezea kilichonitokea mimi. tena mara ya mwisho ni juzi tu mwezi wa3 niliambiwa eti CIF wamesema $8500 kisha nikaambiwa wnaweza kuishusha hadi $5500 lakini hao jamaa wanataka Tshlaki6 na ni kweli ilibidi nilipe hiyo hela maana nilikuwa nimeshaanza kulipishwa storage. Kwa kweli ina uma sana maana serikali imeweka utaratibu kuwa ni lazima mtu umtumie wakala lakini kwa kweli hao mawakala ndio wezi na wanakwamisha mizigo hapo bandarini mno. Mi nathsni serikali inatakiwa ijaribu kubuni mbinu au system ambayo wenye mizigo wanaweza kufanya kila kitu wenyewe.
    Shukrani sana mdau kwa kuleta mada hii.
    Mdau Uk.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2010

    Mimi nadhani watu wote watumie tin numbers kulipia ili kukwepa mgogoo wote, maana itakuwa rahisi kuufuatilia na kujuwa kama ulicholipia ni sahihi kutoka TRA wenyewe.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 03, 2010

    Mimi nimeliwa kama milioni Tsh6.3m na mijizi ya TRA.

    Sina hamu tena na biashara za Bongo, nimeamua kufunga ofisi kabla hawakuniua kwa ugonjwa wa moyo.

    asante mdau kwa kuleta hii habari.

    hapa nilipo nauguza majiraha.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 03, 2010

    Why everything has to be done in DAR, why not ARUSHA, TANGA AU MWANZA, and leave DAR alone, it is busy, CROWDED, and everyone need a piece of it(road networks), commuting to work, taking a flight and just simply getting from point A to B,

    if this could be done in outset of a less busy region, e.g. Tanga, Mwanza and other places, it could be of immense exposure and bring JOBS to other part of Tanzania, not just Dar es Salaam.

    Kila kitu Dar es Salaam,!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 03, 2010

    Hii ndio maana TUCTA wanataka kugoma hali ni ngumu kwa wafanyakazi wa idara za serikali na wafanyakazi wengine, vivyo kupelekea watu kubuni njia zisizo halali ili kuboresha vipato vyao, ndio maana rushwa kila kona katika Tanzania kwani mambo hayaendi. Usishangae kuona hiyo hali iko hivyo, maslahi madogo so watu wameona kufanya maujanja kiivyo kutaboresha maisha yao na baada ya kuona inawezekana wameshafanya kwamba ni sheria.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 03, 2010

    MLETA MADA ULICHOANDIKA NI KWELI TUPU,MAAGENT WENGI WEZI,WENGI WAMEMALIZWA KWA KUPOTEZA MALI ZAO NA MAAGENT FEKI,MIMI YAMENIKUTA KWA KUPOTEZA MAGARI KWA NJIA HIYO KESHO ATALETA STORY HII KESHO HII KESHO KUTWA HIKI ILIMRADI MUDA UNAKWENDA STORAGE ZINAPANDA,ALICHOKIANDIKA HUYU JAMAA NI KWELI HUU NDIO MTINDO WA MAAGENTI WENGI HIVI SASA.INATISHA SANAWATU MJIHADHARI NA MAWAKALA HAWA NJAA TUPU,HIVI SASA UNASHANGAA KAMPUNI NYINGI MFANO WATAKWAMBIA KUCLEAR GARI GHARAMA ZA AGENT BI DOLA 100 AU LAKI NA THELATHINI,UKWELI HIYO GHARAMA YA KUFANYA KAZI HIYO INGELIKUWA HATA DOLA MIA TATU,WEWE SI UTAONA AMEKUTOZA KIDOGO SASA SUBIRI NINI KINAKUJA WANATAKA HIKI,KESHO HIVI SIJUI FEDHA YA NINI BY THE END UTAJUTA..UKWELI NAFIKIRI BIASHARA HII YA CLEARING AND FOWAEDING IMEHARIBIKA KWA KUWA LESENI NI NYINGI NA KAMPUNI NYINGI MNO UTITIRA WAKATI KAZI NI CHACHE WATU WANAKUBALI KWA GHARAMA ZA CHINIWAKATI UKWELI HAWANA UWEZO WA KUFANYA KAZI ILA KUWAIBIA WATEJA

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 04, 2010

    MWACHIE NAFASI MZEE KITILYA AJIBU.SI MNAKUMBUKA ALIVYOITETEA TRA KWENYE DIASPORA.MIMI NAONA TZ ISAHAU MAENDELEO.TRA NDO SHINA NA LA MAPATO SIJUI TUTAKUWA SERIOUSE LINI

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 04, 2010

    Inasikitisha mpaka leo hii karne ya 21 ukiingia kwenye tovuti ya TRA huwezi kujipigia mahesabu ya kukadiria kodi utakayodaiwa kwa lolote wakati ni hesabu rahisi za kujumlisha na kuzidisha. Hata hesabu za mchango wa harusi ni ngumu kuliko za kodi ya gari.
    TRA najua mnasoma hii. Hii ni changamoto. Tengenezeni hata spreadsheet ya kupiga hesabu za kodi ya gari mtuwekee kwenye tovuti yenu. Niko radhi kuwasaidia kufanya kazi hiyo mkipenda. Tumeni maombi kupitia globu ya jamii.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 04, 2010

    niliibiwa mara nyingi hapo bandarini na nikalipishwa pesa za ajabu hapo TRA. inasikitisha sana. nilichoamua kufanya ni kuingiza mzigo wangu kupitia Holili. ni rahisi sana. no wizi, no njoo kesho.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 04, 2010

    hii inasababisha serikali kukosa mapato kwani huwezi kuendelea kufanyiwa upuuzi. nimesikiliza bbc jana. wanajitetea kuwa wananyanganywa wateja na kenya si kwa sababu ya huduma. hiyo ni kukimbia ukweli. hamsomi maoni na kwa hiyo hamjui nini cha kurekebisha. badilikeni bwana TRA. mnaudhi sana kwa mambo yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...