ankal akjiandaa kupiga raundi mitaa ya frankfurt. hii ndinga ankal kavuta ila anasita kuishusha bongo maana jamaa wa trnanihii anawaogopa kweli. afanyeje?
ankal akiwa tayari kuvinjari


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2010

    mmmh kamichu acha hizo... tunajua ulaya huku unakodi tu gari lolote ni uwezo wako tu. hii mambo ya kusema ulishushe mmmmh unanifurahisha sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2010

    Hivi kumbe mablog na yenyewe yana pesa hivi.... basi nami nalianzisha langu www.kiyungifundikira.blogspot.ca karibuni sababu nami nahitaji usafiri, bado nadandia usafiri wa watu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2010

    kamichu unaendesha kweli au mapozi tu? manake watu wakija ulaya huwa wanaogopa sana barabara nyingi na kubwa magari ni yanakimbia haswa, tunaona hapa hapa kwenye blog yako unavyotuonyesha barabara za nyumbani ndogo so hebu tufafanulie hahaha
    nivizuri ulivyotoa hichi kichekesho kwa leo sasa lini unarudi tena marekani?

    ReplyDelete
  4. tehe tehe tehe
    michuzi utakula tikiti hapo!
    vaa mkanda wewe!
    hupo tanga-nyika hapo!

    au ni photo op!

    tehe tehe tehe

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2010

    Hongera Ankal Michuzi.Ila kwa nini usingenunua Right Hand ? Mimi nahisi Left HanD itakutesa sana huku bongo.
    Halafu huo mchuma unakula mafuta kweli ya 1700/= per little.!!.
    Nicholas,Amsterdam

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2010

    ankal wewe ni mfanyakazi wa serikali una TAX EXEMPTION chukua AUDI A6 hio usiogope hao TRA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2010

    TBL Oyeeee.

    Namimi ngoja nianzishe Blog yangu, sikubali. Najua nitapata wadhamini tu, kama TBL na wengineo kede kede.

    Jichunge sana na TOTOZ, si unajua tena? Isitoshe HIV rate iliyopo inatutosha Watanzania.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2010

    ooooyaaa we ankal seatbelt iko wapi?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2010

    Hapo ni wese tu matatizo na vidimbwi vya mitaani, ila mchuma poa. Ila kabla ya kutoka ktk "P" inabidi uvae mikanda kwani "askari" wa traffic police (!) hawatasikiliza kuwa wewe ni mdau , hujui lugha yao au kuwa mwana CCM!

    ReplyDelete
  10. Kimasomaso, ZanzibarJune 04, 2010

    Ankal, unadandia mapipa kama JK na wasaidizi wake ???!!!!??, ama kweli nyie wenzetu ndio mnaifaidi hiyo nchi kisawasawa.
    Kamua kamua Ankal, acha sie machokoraa tuendelee kuumia kwa ajili yenu.

    ReplyDelete
  11. Mambo Msiige, Tanangozi IringaJune 04, 2010

    Ankal, una leseni ya kuendeshea gari ya huko Germany? Kuwa mwangalifu na usijaribu kuingia highway watakumalizia hukohuko.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2010

    kaka angalia trafic wa huku hawapewi elfu mbili, kama ni mbaya inakuwa mbaya,

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2010

    ankal kijiweni watakukoma

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2010

    ANKO KWANI UNA LESENI YA KUENDESHA GARI ULAYA?AU UMEPIGA PICHA TUU..

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 04, 2010

    Ndinga yenyewe mbona left hand drive? Bongo watakugonga siku hiyo hiyo tu.

    Wambie wakuwekee right hand drive.

    ReplyDelete
  16. Mdau-RussiaJune 04, 2010

    Mh..Ankal kweli si mchezo...naona vitrip kila mwezi..!Lakini anko kurudisha gari nyuma(Reversing) si madereva tunatakiwa kutumia vioo vya pembeni(Side mirrors)..Mbona wewe umegeuka kabisa..teh tehe ee..!Ankal tupe bei ya michuma kama hiyo hapo..naona AUDI ya nguvu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 04, 2010

    Duh..Hongera Ankal..Kitu cha ukweli kabisa hicho

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 04, 2010

    Ankal !teh! teh !
    hili ndinga limekufit we acha tu!
    lakini FFU tutaombaga lift

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 04, 2010

    Ankal unaleseni ya ulaya au ya madafu? sio unagusagusa vyombo vya ulaya.vinaitaji leseni ya EU sio ya madafu watakupiga bao njiani..

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 04, 2010

    ah wp ankal. Hebu tuambie ukweli kama we ni papa mkubwa au mdogo maana hio Aud si mchezo mkwanja wake yakhee

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 04, 2010

    duh naona una reverse mwenyewe umegeuka mzima mzima sasa vioo vina kazi gani???

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 04, 2010

    ankal usitutie aibu hizo gari za ulaya zina camera nyuma ukiweka reverse automatical camera zinawaka , utakata shingo hiyo , hapo sio bongo , then barabarani unatakiwa uwe speed , ushazoe bongo foleni huku unaenda speed ya 5 KMPHS utaweza huko ??? fanya urudi tunakuhitaji huku tz sana , wasije wazungu wakakutoa kafara huko ...

    ndau
    kariakoo

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 04, 2010

    ankal kazi unayo hiyo gari ni left hand na barabara za ujerumani nazo ni left hand sasa ushazoe bongo , usije ukakutana na lori uso kwa uso , rudi fasta bongo

    ReplyDelete
  24. Acha hizo Michuzi, left hand tuachie wenye!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 04, 2010

    hiyo gari inakunywa mafuta kama kichaa ukiileta bongo na foleni zetu hizi utafirisika mapemaaa a.k.a UTAFULIA

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 04, 2010

    Ankal umependeza sana

    Kwanini unawaogopa hao Trnanihii? We njoo nalo utajukuja saidiwa kuwapiga changa la macho. Weye si mtoto wa mjini bwana....

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 04, 2010

    unaangalia nyuma ndio unaweka reverse gear au unaweka reverse gear ndio unaangalia nyuma?

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 04, 2010

    Looking nice ankal vuta mndinga huo Audi ni gari nzuri sana na ngumu kwa bongo inakufaa sana. Naona ni left hand lakini kwa bongo ni tambarare right?
    Hongera kwa mchuma wa nguvu!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 04, 2010

    Ankal Salam!! Hongera kw Hutus dochevele!! Ankal mi naomba tu unijibu mjomba wangu mbona nimetuma post hutaki kuitoa? Mi nilijua ankal unawakilisha watanzania, nikajua utatoa post yangu!! Lakini pia Kama unakuwa umeamua kutoirusha post ni vizuri basi ukamtumia email mtumaji ikamueleza kuwa bahati mbaya hutaweza kuirusha post yake kwa kadhaa wa kadhaa! Ni ustaarabu tu ili mtu Kama anaweza kufanya editing ya post yake ili akutumie tena basi afanye hivyo! Kuliko kuichunia na kukaa kimya mtu anaweza kuhisi wewe ni mbaguzi!! Pia ankal nakuomba usiogope kurusha posts ili mradi hazina matusi!! Tushirikiane ankal tuijenge nchi yetu, wewe una watoto nami pia basi tujaribu kuwatengenezea watoto wetuanarudi Tanzania ya kesho!! Ahsante na pia vekesheni njema dochevele. Ni Mimi Phillip kipokola!!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 04, 2010

    Haya wajuzi nipigieni hesabu.
    Mie nipo hapa ukerewe, na nina mdudu kama huu wa ankal,bei sterlingi sita alfu. Nataka kuushusha bongo, itanigharama kiasi gani,kwa ujumla kutoka ukerewe mpaka Ilala mbele ya kizingiti cha mjomba Ali

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 04, 2010

    Ankali mpaka hapo kama hujapata ticket basi tena sijui kama ulikumbuka kufunga mkanda?

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 04, 2010

    Ukicheki huo ufunguo unaonesha gari imezimwa. Inabidi uipige stati kwanza mkuu!

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 04, 2010

    wee mwanaume una visa?!!

    au ndo kuuza nyago kwa totozz za mjini,hahahaa hhahaa u made my day

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 04, 2010

    heheh gari la balozi wa tz ujerumani, kakuazima.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 04, 2010

    Mdau wa Ukerewe, Kwanza tupe adress ya Mjomba Ali Ilala, Tuanze kumrembulia macho mapema kabla kitu hakijafika!!

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 04, 2010

    WEEEEEEEEEE HUWEZI KUPATA HIYO KWA £6000, YA KWAKO NI SI YA AINA HIYO, NA ITAKUWA INAMIAKA ZAIDI YA 8 NA KUENDELEA, CHINI YA MIAKA 5 UTAULIZWA ZAIDI YA £20000 NA SI YA AINA HII

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 04, 2010

    Mimi nakuomba ankal chonde chonde mtafute Da Sherry umjulie hali hata kama yuko shimoni mfate utupe ukweli maana wengine bado haijaingia akilini ile ishu, sasa hivi wewe ndo macho yetu huko tunakuaminia! naamini hata mama atafurahi na kuridhika akipata data kutoka kwako!

    SHIME SHIME ANKAL MSAADA KIZINGITINI HAPO!!

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 05, 2010

    Ankol hapo umetudanganya, uo mchuma umeingia tu car rental ili uzunguke nayo hapo mtaani wakati wa kurudi bongo unaurudisha, we mjanja hata macredit card ya reservation unayo. Ukweli hiyo ndinga hujaitungua umekodi. But u looking fantabulous

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 05, 2010

    Hii Mashine ni ya Abubakar Liongo.Nilishamuona nalo mwezi uliopita.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 05, 2010

    Hivi Michuzi ni wakati gani unawajibika? maana kila siku uko mitaani, unabomoa maisha tu na mshahara unapata, hivi nyie si ndio mnaosababisha nchi kurudi nyuma? Obama na wasaidizi wake hawazuki kama wewe na kina ... kama ni mikopo mnatatuta basi tungekuwa tumeshatajirika na kunifaika. Jamani mnachekea tuuu hata visivyofaa kuchekewa, basi ficha kidogo mizunguko yako

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 05, 2010

    ankali mambo vipi?
    halfu kaka michuzi a.k.a misupu watu wamekushtukia wewe ni m'goverment wale jamaa wa miwani mieusi 'usalama wa taifa wewe'
    mh ile baloon uloenda nayo mbeya je??
    hii blog ni danganya toto tu!!
    kuweni makini michuzi anapeleka ripoti tu!!
    mdau
    jiang chen

    ReplyDelete
  42. AnonymousJune 05, 2010

    Mdau wa jiang cheng Kumbuka hii blog ni ya watu wote hakuna kujali kazi unayofanya ama muajiri aliyekuajiri na siyo blog ya sirikali... naona sasa watu wanaanza kuichimba blog yetu ya jamii!!!Wadau tupo gado kuendeleza libeneke -- ikalaga baho na hayo mawazo ya kifisadi (dRU)

    ReplyDelete
  43. AnonymousJune 05, 2010

    Ankal, mbona mlango wa Abiria haujafungwa?

    ReplyDelete
  44. AnonymousJune 05, 2010

    Du umewapata kweli wabongo kwa hilo
    Namba ya gari ni NW-JM-70, maana yake ni kwamba hii gari inatoka kijiji kimoja hapa kinaitwa Neustadt an der Weinstrasse (NW ) kipo karibu na mji wa mannheim na kutoka Frankfurt ni kama kilometa 90 hivi na mwenye gari kama alipenda anaitwa majina yanayo anza na JM na amezaliwa mwaka 70 (kama alipenda kuweka hivyo ).
    Kwa hiyo hapa ujerumani kuna namba ya simu mtu yoyote yule anaweza kupiga simu hiyo na akiwa na namba ya gari NW-JM-70 ana ambiwa mwenye gari hiyo ni nani na anapewa mbaka adress yake,kama ni gari ya kukodi mtu una ambiwa kila kitu, na siyo hiyo tu mtu hapa ukifanya ajali na kukimbia,jamaa wakiona namba yako wanakufuata mpaka mlangoni, siyo mambo ya tz namba zimekuwa ngumu kiasi kwamba mtu kabla huja angalia namba mwenyewe katoweka.
    Mdau-Bonn

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 05, 2010

    haki ya Mungu ankal we ni fix uliingia humo ndani kupiga picha tu yani hata hiyo rivasi hukurudi ati ukaweka na koti juu ya kiti ili tuamiani duu kweli akili zako changanya na za mbayuwayu kwi kwi kwiiii ila kwa kweli ulipendeza saaana utadhani unaenda kufunga ndoa!

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 05, 2010

    ankali kwa sifa na uongo?unaongoza.....
    hapo unataka kurusha watu roho tu!
    vaa ile t'shirt basi''the best of u"
    jieng chen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...